Uchaguzi 2020 Lazaro Mambosasa ametoa tamko kwa wanaopanga kupinga matokeo ya Urais

Uchaguzi 2020 Lazaro Mambosasa ametoa tamko kwa wanaopanga kupinga matokeo ya Urais

Maelekezo yapo straight kabisa. Uchaguzi umeshaisha. Tumetoa maoni yetu kipindi cha kampani ili kufanya maboresho. Kampeni zimeisha. Uchaguzi umeisha. Wananchi wamemchagua JPM , ni jukumu la kila raia kutoa ushirikiano kwa JPM kama Rais wetu.

Kwa yeyote Mtanzania anaejaribu maandamano kwa mitandao au kwa vikundi anakwenda kinyume na sheria za nchi, Jamhuri haitosita kutumia nguvu kwa maslaha mapana ya Taifa.

Vijana msirubunike, don’t trust anyone, hao mnaopanga nao wapo watu wetu, utashangaa familia yako haikuoni tena, acheni hayo mambo. Fanya kazi kwa bidii, soma kwa bidii, wapende wazazi wako , itoshe kusema hivo

Kama mnataka maandamano, hakikisha Mbowe, Lema, Tundu, yule Muha Wote wanakaa Front page nyie mkiwa nyuma ili Jamhuri ianze na hao walio mbele.

Tarehe 5 au Jumatatu tuta muapisha Rais. Tunaomba maisha yaendelee na amani itawale. Tumesikia shida zenu na tutatatua baadhi ya changamoto at the earliest.
Sisi ni binadamu huru, tunahitaji kupaza sauti yetu kama hatujaridhika. Kama mtatuua tuueni.
 
Sawa kaka nyie pambaneni, ingieni mabarabarani, andamaneni bila kikomo ila chondechonde msitulazimishe na sisi wengine kuingia kwenye hizo fujo

Mwizi tuacheni tu dada tuko vizuri wala hatuhitaji msaada wala sympathy ya yeyote mwenye shirika na mwizi.

Tutamfurusha kuliko panya buku.
 
Huo wizi hauwezi kuachwa hivihivi hakuna atakayekubali wizi wa mchana na ushahidi upo hakuna kulala yeye atoe matamko tu lakini sisi wananchi ndiyo wenye mamlaka hatujatoa mamlaka kwa wizi wa hivo tangu tanzania izaliwe haijawahi kushuhudia wizi wa hivo ni aibu lazima tukatae wizi na hao wote walioshitiki kwenye wizi tutahakikisha wanatajana hadi aliyewatuma Nyerere alishasema tukiogopa tutatawaliwa na madikiteta basi tuone mwisho wake kama hizo silaha zitashinda nguvu ya umma. Kama wanafikiri wamekata internet VPN iko kila mahali
Ingieni barabarani mbona,bado mikwara mbuzi
 
Mwizi tuacheni tu dada tuko vizuri wala hatuhitaji msaada wala sympathy ya yeyote mwenye shirika na mwizi.

Tutamfurusha kuliko panya buku.
brazaj dada yako nakupenda. Chochote unachofanya kipime kwanza
 
Ccm waiba kura ndo wenye akili? Hakuna wakati mtaitawala hii nchi kwa majuto Kama awamu ya tano.
Mlisema hatutashinda saiz mmeweka mpira kwapani ,mnasema tutatawala kwa majuto,nenda kesho kaandamane tundulissu awe raid[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sisi ni binadamu huru, tunahitaji kupaza sauti yetu kama hatujaridhika. Kama mtatuua tuueni.

Hakuna Binadamu aliyekuwa huru. Usiamini vitu ambavyo havipo. Wala hakuna haki.

Kama ni haki uliipata tumboni kwa Mama.

Hakuna haki katika mwili na nyama. Hata Mungu hajaweka haki kwenye maisha ya Binadamu. Kuna watu ni wazuri wa sura, kuna watu ni wabaya wa sura. Kuna watu ni maskini na fukara, kuna watu ni matajiri, kuna watu wanazaliwa wakiwa vilema, kuna watu hawajui maana ya kilema. Kuna watu hawajapewa neema ya uzazi kuna watu wanafunga vizazi, kuna watu wanazaliwa vipofu na viziwi, kuna watu wanazaliwa vyote vinafanya kazi . Kwa muktadha huo, unaposema haki na huru una maanisha nini ?

au ni wapi umeshawahi kuona haki, please mom, be realistic na itizame dunia kwa jicho pana kisha utagundua kwamba Only you neee to flow with the motion .

Sisi tunasema jaribuni kutoka na misheni imeshaanza kuwabaini wote walio nyuma ya zoezi la maandamano. Mtawakost vijana wasio na hatia.

Fanyeni kazi.
 
Dada haya maji marefu si saizi yako kabisa.

Wewe endelea kuburudika na VPN ya beberu tu.

Huyu mwizi tutapambana naye sisi. Tukimaliza hutahitaji VPN tena.
Kwani mtaandamana lini? Mkuu
 
brazaj dada yako nakupenda. Chochote unachofanya kipime kwanza
Usijali dadaangu.

Wananiudhi sana hawa wanaokufanya dadaangu wewe mama D ulazimike kutumia hadi ma-VPN kuwasiliana nami kakaako.

Kwa ajili yako dadaangu wala usikonde hata wakiniuwa ninayofuraha kufa nikikupigania wewe.

Ni heri nife nikikupigania kuliko kuishi nikiona unanyanyaswa. Na huo ndiyo ulio uzalendo.
 
Ha ha ha maalim alijaribu hizo hatua kumi dah, alichokipata hana hamu babu wa watu.
 
Back
Top Bottom