Lazaro Nyalandu: Tatizo kubwa la CHADEMA ni Uongozi wa juu, CCM imejaliwa mfumo

Lazaro Nyalandu: Tatizo kubwa la CHADEMA ni Uongozi wa juu, CCM imejaliwa mfumo

Mkuu ukihoji demockrasia ya chadema upo sawa kabisa. Lakini ukumbuke ni kama Jana tu kiongozi mmoja wa ccm kasema idadi kubwa ya wabunge waliopita ccm hawakushinda ktk kura za maoni.
Ninachotaka kusema hapa mkuu ni kwamba tunahaki ya kuhoji demokrasia ktk vyama vyetu lakini isiwe ni kwa sababu flank kasema.
Hawa viongozi wanaohama vyama wengi wanakuwa hawaaminiki kabisa.
Tuhoji demokrasia objectively kwa kuangalia uhalisia wa mazingira ya vyama vya siasa na namna ya uendeshaji wake.
 
Hao chadema walikuwa sahihi kumtosa! Na ushahidi wa yeye kuto kuaminika kama kada mwenzake Lowasa, ndiyo huu wa kurudi kwake nyumbani. Ingawa pia siungani nao kwa huu utaratibu wao wa kuwapokea makada wa ccm, na kuwapa vyeo vya kamati kuu na vile vingine vya kanda, na mwisho wa siku wanaishia tu kuwaacha kwenye mataa.

Ifikie wakati Chadema iwekeze kwa wanachama walio safi, badala ya kuendeleza tabia ya kuokoteza makombo kutoka ccm!
Hao wanachama Safi huko chadema mnawatoa wapi? Mbinguni?
 
Uchaguzi wa mwenyekiti Kanda ya Kati mnafanya lini?

Kwani pakacha linapovuja nafasi za uchafu uliovuja huzibwa?

Umemsikia pamoja na kufurukuta kote hakuisha kukumbushwa, lini anarejea nyumbani? Hakuwahi kutakikana huko!

Kweli akufukuzaye hakwambii toka.

Hiiiiii bagosha!

Kwa hakika alikuwa kapotea maboya.

Hivi kweri mbona hamshangilii kuwa mmepata jembe sasa la kulimia kweri kweri?
 
Akiwa 360 Clouds ameliongea hili leo na yuko live mpaka sasa,anasema tatizo lipo kwenye uongozi. Amesema wanachama wa chini kabisa hawana tatizo kabisa ,matumaini yao yanaharibiwa na uongozi wa juu.

Angalizo: Mbowe uongozi wako umeshindwa vibaya sana, achia ngazi

==================

“Nilipoenda nchi ya ugenini (CHADEMA) wimbo ulikuwa haumbiki kwa namna ambavyo nilikuwa naangalia matukio, ilipotokea Mheshimiwa Rais anaumwa kuna baadhi ya viongozi walijitolea wakasema huyu hafai aondoke tufurahi, ilikuwa inanikwaza kupita kiasi”

“Niliposafiri kwenda Chato kuzika mashambulizi ambayo yalikuwa yananipata, hayakutoka kwa wana-CCM, hayakutoka kwa wana-CHADEMA wa kawaida, yalitoka kwa baadhi wenye msimamo mkali, unamshambuliaje mtu alieenda kuzika kiongozi wake wa nchi?"

“Wakati wa matatizo ya Lissu mimi binafsi sikujali kwamba ni CHADEMA, nilimuona ni Mtanzania ni kiongozi mwenzangu kule Singida, nakumbuka hata Mhe Rais alienda pia kumuona. Lakini wanachama wa CCM kuanzia Rais hadi viongozi hakuna aliepiga simu au kututukana”

“Kuna mitihani ilitokea kwenye uchaguzi, kulikuwa na chaguzi za aina mbili, moja ilikuwa kupigiwa kura kwenye kamati, tunaenda kwenye Baraza Kuu. Kwenye Kamati Kuu Nyalandu alipata 100%, nilimgaragaza kweli kweli, kilichotokea viongozi wakasema Nyalandu asije akawa kama Lowassa”

“Uchaguzi wa mgombea ubunge Singida Kaskazini, wajumbe wamefika usiku ule kuanzia saa kumi na mbili watu wananipigia simu wananiambia mbona mgombea Urais wako hakutaki anasema kidogo umkoseshe kugombea Urais kule Dar es Salaam”

“Wana-CHADEMA watu wa kawaida wengi ni watu wazuri, ni watu ambao wanatamani nchi bora, ambacho wanawazidi wana-CCM wewe itisha mkutano watakuja kwa mguu, watatoka walikotoka, watajitolea katika hali ambayo hutoamini”

“Siasa sio matusi, siasa sio kukoseana heshima, sio kutukana kiongozi wa nchi, siasa sio kuwatukana wale unaotofautiana nao, ni kusema hoja zako mbadala”

“Chama Cha Mapinduzi kimejaliwa mfumo, kilivyotengeneza itifaki ya chama, namna ambavyo walitengeneza mfumo wa kutoa dukuduku zako, mfumo wa kuchaguana. Kina strength ya mfumo, naamini imani ya watu tukipeleka kwa public, mwananchi wa kawaida anatoa kura” -
Hii wataalamu wa soka tunasema amepiga BOKO, Leo Nyalandu amebokoa. Anasema;
1.Alipokwenda Nairobi kumwona LISSU hakulaumiwa na viongozi wa chama chake? Huu uongo anausema hadharani na vifungu vya biblia ni mahiri kunukuu japo hajui kifungu gani kunaendana na tukio lake.!! Anamdanganya Nani kama hata Wabunge waliokwenda gereza la Kisongo Arusha kumwona Lema walivyorudi wakalazimika kujiuzulu uongozi wa Kamati kwa maelekezo ya Mwenyekiti wa Chama? Labda amesahau au anajisahaulisha.
2.Anasema alipokwenda Chato kuzika alilaumiwa na viongozi wa CDM? Chama kilichotuma viongozi wakubwa zaidi yake kinawezaje kumlaumu kiongozi mdogo kwa kufanya walichofanya wa juu yake? Yaani mkeo na binti yako wanakuwakilisha kwenye harusi ya mtoto wa Dada halafu wakichelewa kurudi unamfokea binti yako na kumkumbatia mkeo? Hizo akili au ni tope?
3.Anasema tatizo la CDM ni uongozi na siyo wanachama wa kawaida? Hao viongozi wamechaguliwa na hao wanachama wa kawaida, au kuna mapinduzi ya kijeshi yalifanyika kuwasimika viongozi wa CDM?

Kama hakuwa na hoja waliomshauri akae kimya walikuwa sahihi.
 
Hadi leo ni miaka 15 tokea wapo chadema muulize yule twaha wa bavicha au mdude kwa nini hawajawa wajumbe wa kamati kuu
Hadi leo ni miaka 15 tokea wapo chadema muulize yule twaha wa bavicha au mdude kwa nini hawajawa wajumbe wa kamati kuu
kwani unataka wanachama wote wawe wajumbe kamati kuu
 
CHADEMA hapa tayari mmekwama na mmeonyesha huko kwenu HAKUNA demokrasia.

Nyalandu kumbe alimgalagaza Lissu ila mkatumia nguvu kumtoa, sasa uchaguzi mliufanya ili iweje?

Kwanini mlimpa fomu nyalandu agombee huku mkiwa na Mtu wenu tayari?

Kumbe Lissu kelele zote zile Hadi kwenye kamati kuu alipigwa na nyalandu?

Anasema pia viongozi wa chadema mlimtukana kisa kwenda kwenye msiba wa Magufuli, CHADEMA hamna maana kabisa. Nyalandu anaendelea kuwaumbua

Nyalandu kwa haya unayosema, nimekusamehe yote na bora ulivyorudi CCM kwa mama.

Nyalandu nimegundua ni Mtu makini sana.

Kwa hio kawa kama Lowasa au hajawa kama Lowasa?
 
Lissu aligalagazwa vibaya Sana na nyalandu, Kamati kuu wanajua
Sawa kwenye kamati kuu. Je kwenye mkutano mkuu ilikuwaje. Kikwete alimgaragaza Mkapa hivyo hivyo. Lakini kura ziliporudiwa nini kilichofuata ?!
 
Hapo kachemka balaa labda hakunywa chai asubuhi
Nyalandu anasema ,wajumbe walikuwa 30,yeye alipata kura zote,na Lissu alipata kura 24,
Jamami kwani ukiwa ccm ndiyo unajitia akili zote?
 
Back
Top Bottom