Huu ni mpango wa NEC mahususi kuwahujumu Wapinzani. Katika mazingira kama hayo 'uwanja sawa upo wapi''?
Sishangai kwasababu Mkurugenzi wa uchaguzi alisema, vyama vieleze sera za mabarabara kununua ndege n.k.
Yaani mkurugenzi wa ''tume' huru anafundisha siasa za chama kikubwa halafu anakuwa refarii
Huyu ndiye atasimamia uchaguzi wa ''Tume huru' na uchaguzi wa huru na haki!
Haya huko Hai nako OCD anajisemea wazi yale ya kikaoni '' wewe huwezi kumshinda''
OCD ana matokeo tayari, anamsaidia Mpinzania asipoteze muda na mafuta. OCD anasubiri tarehe amtangaze yule aliyeshinda. Kasema wazi huwezi kumshinda!
Huku Msajili anasema vyama visiungane, masikini hakumbuki CCM na TLP na Cheyo.
Uchaguzi Tz.
Kosa kubwa la Wapinzani ni kuingia katika uchaguzi bila tume huru, sijui wanategemea nini!