Hata mimi sikubali mtu yeyote yule, awe mwizi, changudoa, muuaji, shoga, mtoa mimba, msema uongo auwaweNisiongee mengi video ya interview yake pale star tv hio apo chini.
===
Lema aliulizwa na Aloyce Nyanda kuhusu ushoga katika kipindi cha StarTV amesema yeye anaamini katika biblia na kama dunia nzima itaamini katika biblia basi suala la ushoga halitakuwa tatizo.
Hata hivyo amesema haukubaliani na sheria au mtu yeyote anayetaka kumuua mtu kwa kuwa ni shoga. Amesema kitu mtu anachokifanya katika maisha yake ni kitu chake.
Yote niliyoandika yamo katika BIBLIA hiyo hiyo unayoquote, ukipunguza na kuongeza maandiko utakavyo ukiongozwa na Roho ya Mpinga kristo, kujenga HOJA ya kumkataa Yesu na kufufuka kwake.
Siwezi kubishana nawe sababu unatumia akili Yako ya kibinadamu kufungua codes za BIBLIA ambazo ni za kiroho.
Ili uelewe NENO lililo katika BIBLIA, shart kwanza umwamini NENO, ambaye ndiye Mwana wa Mungu ktk mwili wa YESU kristo.
Bt sitodiriki kuanzisha ligi na Mpinga kristo,
Shetani ambaye ni baba Yako, anayajua sana BIBLIA na alimsomea Yesu vifungu vya BIBLIA hii hii Ili kujinufaisha binafsi Ili kumjaribu.
So upumbavu ni kudhani unaweza kumchunguza Na kumjua Mungu aliyeandikwa kwanye BIBLIA Kwa AKILI zako za Theology za kibinadamu bila msaada wa Roho mtakatifu.
Mwambie Lema hivi Yeye ni Mkristo...na Kitabu chake kitakatifu cha Biblia ....Walawi 20.13 mwambie inamtaka kuwa bahasha na shoga wote wauae kama haamini Biblia Mwambie atuambie Yeye ni Imani Gani
Maelekezo ya Mwenyenzi Mungu Mtakatifu yanasema Hivyo na Yeye anapingana na Mwenyenzi Mungu Mtakatifu anayemuamini shida Nini?
Mwamini YESU kristo kuwa BWANA na mwokozi wa Maisha Yako,Hivi kweli wewe ni mkristo ??
Bwana Yesu Kristo alieleza mizani na alama za imani kama ifuatavyo:
1. Mkiwa na imani ya punje ya haridali, mtauambia mlima huu, ondoka hapa nenda kule, nao utaondoka; wala halitakuwapo neno lisilowezekana kwenu. (Mathayo17:20; 21:21; Marko 11:22-23, 9:23, Luka 17:6, 12, 13).
2. Bwana akasema: “Kama mngekua na imani kiasi cha chembe ya haridali mngeuambia mkuyu huu,ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.” (Luka 17:7).
3. Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambia mkiwa na imani , msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, ngo'ka ukatupwe baharini, litatendeka. na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea. (Mathayo 21:21-22)
4. Amin, Amin, nawaambieni, yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwani mimi naenda kwa Baba. (Yohana 14:12-13).
5. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lolote nanyi mtatendewa. (Yohana 15:7).
6. Tena nawaambia, wawili wenu mtakapopatana duniani katika jambo lolote watakalo liomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. (Mathayo 7:3-12)
7. Ombeni nanyi mtapewa.... (Mathayo 7:3-12).
Katika mizani hii ya imani ya Wakristo, tumejua kwamba Mkristo atatambulika kwa alama zilizotajwa hapo juu. Tena hizi ni alama za imani ndogo sana ya chembe ya haridali. Lakini kama Mkristo atakuwa na imani kubwa ataweza kuonesha miujiza mikubwa zaidi.
Vilevile Mkristo mwenye imani ni yule ambaye ataweza kuonesha miujiza na hasa sawa na ya Bwana Yesu bali mikubwa zaidi kuliko yake. Sasa kwanza tutafute miujiza ya Bwana Yesu katika Biblia, tumeona baadhi yao kama ifuatavyo:
1. Kuponya wagonjwa (Mathayo 8:16, 9:22, na 15:21).
2. Kuponya walemavu (Mathayo 8:1-3).
3. Kuponya mabubu. (Mathayo 9:3-7; 12-22).
4. Kuponya mwenye kupooza upande mmoja (kiarusi) (Mathayo 8:5-13. 9:1-7, 12:22).
5. Kumponya mwenye kifafa. (Mathayo 17:14-19).
6. Kuponya mkono wenye ukoma. (Mathayo 12:15).
7. Kuponya mgongo uliopinda (Kibyongo) (Luka 13:10).
8. Kuwafufua wafu. (Mathayo 9:24).
9. Kugeuza maji kuwa pombe. (Yohana 2:1-9).
10. Chakula kidogo kitoshe watu elfu tano. (Mathayo 14:13-21).
11. Kutembea juu ya maji. (Mathayo 14:22-23).
12. Kuzuia tufani . ( Mathayo 8:23-33).
Hapa nimetoa baadhi ya mifano tu ya miujiza ya Bwana Yesu.
Kama huwezi kuonesha miujiza ya aina hii au alama ya imani yao sawa na Biblia, basi mambo mawili yanathibitika.
A. Bwana Yesu pia hakuonesha mujiza wowote bali ni hadithi za kutungwa tu zisizo na ukweli ndani yake.
B. Siku hizi Mkristo yeyote hana imani sawa na chembe ya haridali, bali nyote mumeshapotea tayari na hamuna alama au dalili yoyote ya imani.
Hali hizi zote mbili ni mbaya sana na za kutisha.
Na dawa yake ni moja tu kwamba uingie katika dini ya Mwenyezi Mungu, ISLAM, baada ya kutambua umoja wa Mungu na Mtume Muhammad s.a.w. waila utaendelea kufedheheka siku hadi siku.
TAMBIO:
Ninawapa Wakristo tambio (challenge) kwamba kama mnayo imani sawa na chembe ya haridali, mtuoneshe miujiza iliyotajwa hapo juu.
Mkristo mmoja au wawili au mjumuike nyote, tunataka kuona miujiza tu ya imani yao, hata Pope au Wachungaji wenzako wajitokeze
Wapi moto ulishindwa[emoji23][emoji23] leta evidence
Kwani Mungu ndivyo alivyokuambia??? Andiko lililesa hili ni la walawi tu ??
Wahindu huruhusu mjomba kuoa mpwa wake. Ndugu wa mama anaweza kuoa binti yake. Sheria ya Musa amani iwe juu yake inakataza jambo hili. Uislamu pia unakataza.
Agano jipya hata halishughulikii suala hilo, kwani halishughulikii 95% ya masuala yoyote ya kijamii huko nje! Si chochote ila hadithi na simulizi ambazo hata zinapingana kuhusu Yesu, kusulubishwa kwake na kufufuka kwake.
Swali langu hapa ni:
Iwapo Mhindu mpagani anakubali ukristo, basi je, bado anaweza kuoa mpwa wake (binti ya dada yake), kwani Agano Jipya halikatazi jambo hilo?
UNAJUA HUYO KAJIBU KISHERIA ZAIDI. UGANDA WAMEPITISHA MSWADA WA KUPINGA USHOGA NA ADHABU ZAKE. KWAMBA NA SISI HATUNA SHERIA ZA KUPINGA USHOGA.
Mwamini YESU kristo kuwa BWANA na mwokozi wa Maisha Yako,
Ndipo umwombe akupe Roho mtakatifu atakayekusaidia kumjua Mungu na NENO lake.
Miujiza pekee haitokupa Mbingu.
(Wafilipi 2:10,11).Yesu ndiye Mungu atakayekuja duniani kuuhukumu Ulimwengu juu ya DHAMBI, na Kila goti litapigwa Mbinguni na Duniani mbele zake na Kila ulimi utakiri ya kuwa YESU ni Mungu Kwa Utukufu wa Mungu baba.
Yesu alikuja Kwa wote wenye dhambi, bila kujali dini zao.
Islam, christians au Pagani wote wanamwitaji Yesu awaokoe, Mohammed Hana Mbingu ya kukupeleka, atatupwa Jehannum pia ikiwa hakumwamini Yesu.
Unaamini Yesu alifufuka kutoka Kwa wafu?]
Nikusikilize wewe au Bwana yesu mwenyewe ???
Ukaendelea kumsingizia uongo Bwana Yesu kwa kusema
Yesu alikuja kwa watu wote wenye dhambi ,
Bahati mbaya mimi si muisraeli labda wewe mwenzangu ndiye Muisraeli wa Chato
Umeniambia nimwamini Yesu kristo ni mwokozi wa maisha yangu lakini
Bwana Yesu mwenyewe kinyume na maneno yako ,
anasema ;-
1. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli , Mathayo 15:24
Bwana Yesu Anaendelea kusema
2. Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
Mathayo 19.28
3. Bwana Yesu anaendelea kusema
Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa.
Yohana 17.9
Ukamalizia na Maneno ya Paulo Wafilipo 2:10-11
Tuanzie na
Wafilipi 2:8-9
Naye alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. Kwa hiyo Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
Wafilipi 2:8-9 NIV
Je, Mungu alikufa?
Je, Mungu Anaweza Kufa?
Ikiwa Yesu alikuwa Mungu tangu mwanzo Kwa nini alihitaji Mungu kumfufua?
Ikiwa uliniambia Mungu alikufa, inamaanisha kuwa Biblia hiyo hiyo inadanganya inapotuambia Mungu hafi
1 Timotheo 6:16
Unaamini Yesu alifufuka kutoka Kwa wafu?
Yesu huyo huyo uliyequote akiwambia wanafunzi watahukumu kabila 12 za Israeli, ndo huyo huyo amewambia wanafunzi wake kuwa Enendeni ULIMWENGUNI kote mkaihubiri INJILI Kwa Kila kiumbe, mkibatiza Kwa Jina langu, Unadhani maandiko yanapingana?
Kifo tafsiri yake ni nini?
Jina la Mungu ni lipi ,Anaitwa nani?
Huwezi kuuelewa ukristo kama hujauishi na kuusoma,nakushauri okoka jifunze ukristo,ukitaka ujifunze ukristo kupitia compare and contrast utakua unapoteza muda wako sana
Wakristo tunaheshimu sheria hasa amri 10 za Mungu hiyo ndiyo torati ambayo hata Kristo alikuja kuitimiliza,na katika amri hizo kumi tunapata kuona upendo kati ya Mungu na wanadamu na wanadamu kwa wanadamu.
Naona ulitamani sana kuona wakristo wanabeba mawe na kuponda wazinzi na mashoga hadi wafe,kumbuka utume wa kristo ulikua ni tubuni mkaokoke ili muurithi ufalme wa Mungu,kristo haku eneza chuki dhidi ya wenye dhambi ndio mana alikula na kuketi pamoja na wenye dhambi.
Ukristo ni dini ya amani na upendo ikilenga zaisi mabadiliko ya rohoni yenye athari chanya kimwili.
Ila wewe unaetembea na wake za watu tukuache,Mbunge wa kawe, ametangaza kupeleka HOJA bungeni Ili kuongeza kibano Kwa Mashoga na wafiraji Ili tufikie Hatua walizofikia ug, japo Kwa uchache.
Yaani viboko hadharani, kifungo mix,nk nk.
Naunga mkono HOJA 100%.
Unaquote maandiko kuhusu kufufuka Kwa Yesu hapo hapo unadai yameongezwa.]
Sio kuamini tu , Swali ni Yesu mwenyewe ndani ya Biblia alisema nimefufuka ?? au watu wanampakazia ??
Kama Yesu huku anawaambia wanafunzi wasiende , halafu anakuja kuwaambia nendeni .
Kauli zinazonukuliwa kwa kudai kuwa ni ushahidi kuwa Yesu mwenyewe alitaka mafunzo yake yakafundishwe kwa ulimwengu wote yamo katika Injili ya Mathayo 28.19-20, Injili ya Luka 24.46-49 na Marko 16.15.
Je, imekuwaje?
Yesu ni kigeugeu?
Mbona huku anawakataza wanafunzi wake wasende kuwahubiria ila kabila kumi na mbili za Israili, na huku anawaambia nendeni kuwahubiria Injili ulimwengu mzima.
La, Yesu si mbabaishi, wala si kigeugeu.
Hebu natuziangalie vilivyo hizo amri mbili, moja ya kuwa mafunzo yake wasifunzwe ila wana wa Israili tu, na ya pili ni hii ya kuwa watu wote wafunzwe dini.
Vipande vyote vitatu tulivyonukulu mwishoni havitaji mambo ya Yesu alipokuwa na maisha yake ya uhai wa kidunia, lakini vyaeleza mambo yaliyotukia baada ya "kufufuka kutoka wafu" kama inavyosimuliwa na Injili zote tatu.
Yajuulikana kuwa Injili ya mwanzo kuandikwa ni Injili ya Marko.
Hizo nyingine ziliandikwa baadae, na labda ujuzi wao ulitegemea hiyo hiyo Injili ya Marko.
Yajuulikana vile vile kuwa maneno yote yaliyohusu kufufuka Yesu kutokana na wafu, pamoja na hayo maamrisho ya kwenda kuihubiri Injili "kwa kila kiumbe", kinyume na maamrisho yake yote ya kuwa asihubiriwe ila Muisraeli tu - maneno hayo yote hayakuwamo katik Marko ya asli, bali yaliongezwa baadae.
Encyclopaedia Brittanica, nakla ya 11, jalada 17, sahifa 730, yasema ya kuwa kipande chote hicho kiliongezwa baadae, yamkini mwanzo mwanzo wa karne ya pili, kuchukua maneno yaliyopotea, au yaliyoonekana kuwa ni mapungufu.
William Neil akiandika katika tafsiri ya Biblia iitwayo Harper's Bible Commentary anasema:
"Kama lipo jambo lolote katika uchunguzi wa Injili ambalo juu yake wataalamu wamekubaliana, ni kuwa kufika hapa (yaani Marko 16.8) Injili ya Marko inakoma. Sehemu iliyobaki ya sura (yaani 16.9-20) ndio hiyo iitwayo "Kimalizio kirefu" cha Injili. Kimalizio hicho hakionekani katika nakla za miswada ya zamani, na ambacho ni nyongeza iliyopachikwa katika karne ya pili kutokana na maongezo ya Mathayo, Luka na Matendo...ushahidi wa kale kabisa ulioandikwa juu ya Kufufuka (Yesu) haumo katika Injili bali katika barua ya kwanza ya Paulo kuwapelekea Wakorintho 15.3-8."
Maneno hayo ya Paulo aliyowaandikia Wakorintho na ndio mara ya kwanza kutajwa kufufuka kwa Yesu ni haya:
Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maaandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; badaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.
1 Wakorintho 15.3-8
Ikiwa kipande chote tangu mstari 9 mpaka mstari 20 katika sura 16 ya Injili ya Marko, kimepachikwa, basi kisa chote cha kufufuka Yesu kimebuniwa. Mwenye kubuni kisa hichi ni Mtakatifu Paulo. Hivyo ndivyo tunavyoweza kuagua kutokana na kuisoma Biblia, kwani maandishi ya kwanza hayamo katika Injili bali yamo katika barua ya Paulo kwa Wakorintho.
Amesema Craveri katika Maisha ya Yesu:
"Paulo alijihakikishia mwenyewe kuwa ijapokuwa Yesu ni kweli alikufa, lazima awe amefufuka, akiuwacha mwili wake wa kidunia nyuma ili avae mwili wa 'kiroho'...Paulo alichanganya mawazo yake mwenyewe ya kikafiri kafiri ya Yesu kuwa na maisha mapya kwamba ni malipo yake kwa mema yake, pamoja na imani ya Kiyahudi ya kuwajibika mapatano na Yehova (Mungu) na agano la pili. Kwa hivyo Paulo akafunza kuwa ndiyo haya khasa yaliyokuwa ni kazi ya Yesu, na hicho ndicho cheo chake machoni mwa Mungu: kafara ya nafsi yake kwa utakatifu wake na kutokuwa na dhambi kwake ili afutie kwa pamoja makosa ya wote."
Ikiwa basi msingi wa hadithi nzima ya kufufuka Yesu hadi ya ubora wake ni kuwa ni ya shaka shaka - licha ya kuwa ni wazi kuwa ni ya uwongo - hapana njia ya kuamini ya Kuwa Yesu wakati wo wote katika historia aliwahi kuamrisha watu "Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu," kwa sababu haya hakuyasema ila baada ya huko kunakoambiwa ni kufufuka.
Unaquote maandiko kuhusu kufufuka Kwa Yesu hapo hapo unadai yameongezwa.
Neno la Mungu limethibitishwa.
Kuhusu kufufuka Kwa Yesu ni HAKIKA.
Maandiko yameandika, Pia ROHO MTAKATIFU ambaye ni Roho wake Yesu analithibitisha neno Hilo.
Yesu Yu hai, ana mamlaka juu ya KIFO.
Mwamini YESU utaokoka, usipoamini, umekwisha kuhukumiwa.
Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.
Amen
Ewe Mpinga kristo, una HAKIKA Yesu hakutabiri juu ya kufa na kufufuka kwake?HAKUNA aya hata moja ya Biblia inayomtaja mtu yeyote aliyeona sura ya Yesu hasa wakati akifa pale msalabani.
Yesu alidhaniwa tu kuwa ni Yesu aliyeuawa msalabani, lakini baada ya siku chache Yesu huyo akaonekana yu hai, wala hakurudi kama pepo (ghost)!
Kung'ang'ania kuwa ni Yesu aliyeuawa pale msalabani ni utani mgonjwa, hususan tukizingatia ushahidi wote huo hapo nyuma, vipofu na hata kuwafufua watu.
Kwa upande mwingine twaambiwa eti kumtesa Yesu kwa kumpiga, kumchoma kwa ncha kali, na kumpigilia misumari mtini eti ilitosha kumuuwa Yesu.
Hii haiingii akilini kimantiki labda kwa kuiamini tu kiupofu (blindly).
Isitoshe, Yesu angalisubuliwa kweli, ingekuweko aina moja tu ya msalaba aliouliwa. Lakini Catholic Encyclopaedia peke yake ina aina 40 za misalaba.
Kwa sababu zisizo dhahiri, msalaba ule wa vipande viwili vinavyosigana yaani +, ndio umependelewa zaidi na Waingereza wakauita "Cross", ingawa neno la awali la msabala kwa Kigiriki ni "Stauros" ambalo halina dhana ya vipande viwili ila kimoja tu.
Biblia chche tu kama ile ya Mashahidi wa Yehova ndio imetaja waziwazi kuwa Yesu aliangikwa kwenye mti (stauros) na usulubisho kwao wao sio "cricifixion" bali "stafixion".
Dhehebu jingine limesema Yesu aliangikwa kwenye mti wenye umbo la T. Ke bado Wakristo wengine wanauabudu msalaba huo wa alama ya kujumlisha +.
Gazeti la Newsweek la Aprili 4, 1994 liandika: "Kifo cha Yesu - Fikra mpya za siku zake za mwisho". Limesema kuwa, kama Yesu kweli aliuliwa msalabani, basi lazima iweko aina moja tu ya msalaba.
Katika gazeti hilo hilo, Padri wa Kikatoliki Raymond Brown kaandika kitabu chake, "The Death of the Messiah (Kifo cha Masihi)". Doubleday na wanaseminari wenziwe 2000 amesema kuwa hadithi za Yesu kuhusu kuhubiri, kuponya wagonjwa, kufanya miujiza, hizo zaweza kuwa kweli; lakini hadithi nyingine (kama ya kusulubiwa Yesu) hazina usahihi wa kihistoria (historical accuracy).
Hii anasema ni kwa sababu waandishi wote wa Injili hawakuwa mashahidi wa macho (eye witnesses) kushuhudia hata moja ya yale wayoyaandika mnamo miaka 35-70 baada ya Kristo; na mpaka leo hatuna hakika ni nani hasa aliyeandika Injili zote hizo, ambazo kila inatofuatiana na yenzie.
Yesu asingekosa kutabiri kuuliwa kwake msalabani, akatabiri juu ya kuteswa tu:
"Mt 23:35 Hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habil, yule mwenye hakika hata ... Zakaria ... mliyemuua kati ya patakatifu".
"Lk 22:15 ... Nimetamani sana kula pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa"
Ewe Mpinga kristo, una HAKIKA Yesu hakutabiri juu ya kufa na kufufuka kwake?
Mbona maandiko yapo wazi!!!!
Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.
Amen
Soma hapa ewe Mpinga kristo,
(Luka 9:22, Luka 18:31-33, Luka 24:7).
Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulubiwa, na kufufuka siku ya TATU.
Fahamu hili, Kuna pande mbili tu, Uwe mwana wa Mungu Kwa kumkiri YESU kuwa BWANA na mwokozi au uwe mwana wa Ufalme wa Giza.
Si Rahisi mtu anayeaminishwa kuwa majini yameumbwa Ili yamwabudu mungu akaamini kirahisi juu ya kufufuka Kwa Yesu.
Kubali kumwamini Yesu, Mapepo yakutoke Ili Yesu aingie maishani mwako.
Soma hapa ewe Mpinga kristo,
(Luka 9:22, Luka 18:31-33, Luka 24:7).
Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulubiwa, na kufufuka siku ya TATU.
Fahamu hili, Kuna pande mbili tu, Uwe mwana wa Mungu Kwa kumkiri YESU kuwa BWANA na mwokozi au uwe mwana wa Ufalme wa Giza.
Si Rahisi mtu anayeaminishwa kuwa majini yameumbwa Ili yamwabudu mungu akaamini kirahisi juu ya kufufuka Kwa Yesu.
Kubali kumwamini Yesu, Mapepo yakutoke Ili Yesu aingie maishani mwako.