Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Hello!

Naona Lema ameanza kwa gia ya matusi kwa wanaojiita bodaboda. Lema amesema bodaboda sio kazi ila ni laana.

Hivi hizi si ni dharau kwa vijana wa bodaboda? Yaani watu wanaendesha familia kwa kazi hiyo halafu anakuja mtu anawadharau na kutukana eti wamelaaniwa?

Nyie wafuasi wa CHADEMA mnaposhabikia watu muwe mnajitambua. Hawa kina Lema wamekuwa wabunge hapo Arusha miaka 10, waliwafanyia nini cha maana?

Ujinga kama huu wa CHADEMA ndio kina Ruto walikuwa wanawadanganya Kenya badala yake hakuna cha maana anafanya; ameongeza tax, ameondoa ruzuku kwenye mafuta maisha yako juu, anakopa na alisema hatokopa, anaomba misaada ya chakula hadi Ukraine, mfumuko wa bei ndio usiseme nk.

Ujinga kama huu wa upinzani ulifanyika hata Malawi, kawaulize Wamalawi kama kuna nafuu wamepata, the likes ya Zambia.

Ukiwasikiliza CHADEMA huwa wanaota ila hawana strategy ya kile wanachoota, uje uwaulize watawatoa vipi Watanzania kwenye umaskini kama wanavyodai wakati hawana hata sera inayoeleweka.

Toka nimeanza kuwasikiliza CHADEMA zaidi ya Katiba Mpya na mambo ya Majimbo hakuna jipya, maana hizo political tools sio nyenzo za kuondoa watu kwenye umaskini.

Mwisho, ukiwasikiza ACT Wazalendo unaona content ila ukiwasikiza CHADEMA unaona ulalamishi na kuorodhesha matatizo ya Watanzania bila suluhisho.

Watanzania stukeni mnafanyiwa ngazi za kutengenezea watu maisha.

 
Duh aiseee nandio waliokodiwa kwa wingi kwenda kumpokea
Shangaa Sasa na wewe,mavijana mengi ni majinga yanatumiwa na machadema huku hawana Cha kuwasaidia..

Si Bora Rais aliyeamua kuwasaidia Kwa kuwatafutia mashamba Moja kwa.moja watawezeshwa Kila kitu kuliko Hawa wanaotumiwa kama condom na Chadema
 
Indonesia,Kenya,Uganda, Rwanda na kwingineko zinakofanya kazi bodaboda kwa majina tofauti tofauti nako ni laana?

Haya bwana Nabii wa Chadema na Machame!
Bodaboda na Bajaji na Machinga wakiwekewa utaratibu mzuri na miundombinu na wawe operational maeneo Fulani Fulani ni kazi ya kuingiza kipato..

Huko Vijijini ni usafiri muhimu sana,kwanza sijajua inakuaje laana.
 
Wewe ni mpumbavu wa kiwango cha juu sana tena akili yako ni matope unafikiri Lema hana akili kutamka hivyo??Leo wanaodanga ni wasomi tena wasomi kweli kweli unafikiri wanapenda kuwa hivyo?Hata boda si wote wamependa kuwa boda boda bali wamelazimika kutokana na huduma mbovu ya Serikali ya ccm.
 
Back
Top Bottom