Lema: CHADEMA tubadili mbinu, njia ya chuki haitusaidii

Lema: CHADEMA tubadili mbinu, njia ya chuki haitusaidii

Tatizo la Chadema ni na vyama vyote vya siasa ni moja, ni lile lile kama la dini. Ulianza ukatoliki waprotestant wakajitenga na kuanza kuwaona wakatoliki waovu, wabaya. Papa akaanza kuitwa mpinga kristo, waprotestanti wakijiona wako sahihi.

Baadaye wakaja walokole wakawaona wakristio wengine ni wabaya, after all hawaneni kwa lugha, halafu wanakunywa pombe.

Walokole wakaeenda wee saa hizi tuna manabii na mitume matapeli wanapiga pesa na kumiliki utajiri wa ajabu ndani ya ulokole. Kila mtu mwenye common sense anaanza kuona hakuna cha mkatoliki, mprotestanti wala mlokole, dini zote ni watu wale wale na mapungufu yao.

Njoo kwa vyama vya siasa sasa.

Hivi Chadema, Lema, Lissu na kenge wengine ndani ya hicho chama wana guts gani za kuanza kumnyooshea kidole kenge wengine. Kenge ni kenge tu. Lema hana moral authority ya kusema hiki ni sahihi hiki sio sahihi. Wanasiasa na binadamu kwa ujumla tujifunze kuwa humble na kusema machache.

Na kwa namna Chadema inavyojipeleka itakuwa kosa la millenia kwa nchi hii kuwapa hawa watu nchi watuongoze.
 

"Njia ya mbele hii ni ngumu kuliko hii ya sasa ila wananchi wanaweza kuzuia hiyo njia isiwaumize viongozi wao, wananchi wako tayari?

Sasa nikizungumza hivyo kwenye mikutano wanaanza ooh Lema umeanza kuwa muoga, sio kuwa kuoga pengine nimeanza kuwa na hekima, nimegundua kuwa njia ya chuki haitoki" amesema Lema.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Godbless Lema, amesema hayo leo Novemba 1, 2026 jijini Arusha, katika mkutano wake maalumu na waandishi wa habari.

Lema ameongeza kwamba "Nyie wananchi ambao ndugu zenu wanauawa halafu mnaogopa hata kupiga kelele, tunasema maelfu ya watu wamekufa, wameuawa, juzi kulikuwa na ibada, hayo maelefu yalikuwa wapi?" amehoji Lema.
Stupid Lema. Kwa hivyo aliyeuwa vijana 500 hakuwa na chuki ?. Aliyefungua kesi ya uhaini kumtesa Mh Lissu hakuwa na chuki? Aliyemuua kada wa CHADEMA Mzee Ally Kibao kikatili hakuwa na chuki? Akae kimya kama Hana cha kuongea. Kwa hivyo CHADEMA wawe na upendo ila aliyemteka Mwaipaya Nairobi aendelee na ujinga wake.
 
Huyo jamaa anasema aliongea na Mbowe harusini akamwambia ameachana na siasa halafu yeye akaenda kuwaambia viongozi wamuondoe Mbowe kwenye magroup na Kamati Kuu ya chama kwa maongezi waliyofanya harusini.

Wewe unaona kuna kiongozi hapa?
Alitaka kuwaingiza kwenye shida, si angemshauri aandike barua? Yeye anaenda moja kwa moja kuwaambia wamtoe, ili waonekane hawana sifa ya kuwa viongozi.
 
Lema Kwa upande wake yuko sahihi shida chama chao kina viongozi ambao hawa hataki siasa biashara. Lema Bado yupo Jana Leo Kuna lisu na heche
Yaani wanafanya siasa serious.
kama mnakumbuka magufuli alimwita mbowe na wenziwe wahuni. Kazi yao ilikuwa kuichachafya serikali iliitooe chochote kwao harafu kimyakimya wanaiunga mkono serikali.na hayo ndo yalikuwa maisha yao,huku wafuasi wao wakiteseka
Yaani wanajifanya wakali kwenye majukwaa LAKINI kumbe wana lao jambo

Lema tambua zama zime badilika Watz wengi wanauelewa WA kutosha, zile siasa za danganya toto zimepitwa na wakati . Ukitaka kuamini angaliaene wenzenu kwenye mikutano wanavotumia nguvu kuwapata watu wakuhidhuria mikutano yao Tena na usafiri juu LAKINI Bado Kuna baadhi ya wananchi hawaendi

Mwisho wa siku kwenye uchaguzi hawaendi kupiga kura
Angalau wenzenu wana tume na majeshi yote ya kwao nyinyi mna nini . According to chacha.
Muwe sirius. misiwachanganye wafuasi wenu watawakimbia
 
NI ngumu sana kumuamini mwanasiasa.
Sidhani kama suluhu ya matatizo ya Tanzania italetwa na wanasiasa na hizi sarakasi zake.

ndani ya viunga vya Hodeidah port - Yemeni
Mku matatizo ya Tanzania yatakuja kutatuliwa simu watanzania tukijitambua na kukua namna ya kutafta namna ya kuyatatua..
Lakini kuwategemea watu kama hao wanasiasa hapana.
 
Tatizo la Chadema ni na vyama vyote vya siasa ni moja, ni lile lile kama la dini. Ulianza ukatoliki waprotestant wakajitenga na kuanza kuwaona wakatoliki waovu, wabaya. Papa akaanza kuitwa mpinga kristo, waprotestanti wakijiona wako sahihi.

Baadaye wakaja walokole wakawaona wakristio wengine ni wabaya, after all hawaneni kwa lugha, halafu wanakunywa pombe.

Walokole wakaeenda wee saa hizi tuna manabii na mitume matapeli wanapiga pesa na kumiliki utajiri wa ajabu ndani ya ulokole. Kila mtu mwenye common sense anaanza kuona hakuna cha mkatoliki, mprotestanti wala mlokole, dini zote ni watu wale wale na mapungufu yao.

Njoo kwa vyama vya siasa sasa.

Hivi Chadema, Lema, Lissu na kenge wengine ndani ya hicho chama wana guts gani za kuanza kumnyooshea kidole kenge wengine. Kenge ni kenge tu. Lema hana moral authority ya kusema hiki ni sahihi hiki sio sahihi. Wanasiasa na binadamu kwa ujumla tujifunze kuwa humble na kusema machache.

Na kwa namna Chadema inavyojipeleka itakuwa kosa la millenia kwa nchi hii kuwapa hawa watu nchi watuongoze.
Sahihi.
 
Alitaka kuwaingiza kwenye shida, si angemshauri aandike barua? Yeye anaenda moja kwa moja kuwaambia wamtoe, ili waonekane hawana sifa ya kuwa viongozi.
Inashangaza sana. Mtu mwovu au muongo anapojitetea ataongea maneno mengi ya kweli ili kukupumbaza ila msikilize makini utapata ujue uovu wake.
 
nimekua nikishauri hili swala kwa miaka 17 mfululizo nikijaríbu kuwashauri chadema,wabàdili mbinu,wajenge chama,waeneze matawi ya chama hadi vijijini huko,tatizo wangdhani siasa za uhasama zitawaingiza ikulu,kutukana,kuzushia vifo viongozi walioko madarakani ni kupoteza muda tu,,wao wajenge chama,waeleze sera zao kwa wananchi na kwa lugha ya kistaarabu,wananchi watawaelewa tu,hakuna mtu ataunga mkono watu wanaochochea vita vya wenyewe kwa wenyewe,watu wanataka utulivu,waendelee na maisha yao na family zao
 
Ila CHADEMA wanapitia mapito mengine kutokana msingi wa waanzilishi wake .kilikuwa chama cha kaskazini na SACCOS. ya kujipatia Pesa na mademu.
Mbowe aliposhondwa imekuwa nongwa sana kwasababu Kuna watu milija yao imekatwa .Walio zoea hayo maisha Sasa wanapata tabu sana.
Kinachowauma lema sugu na genge lao wakati huu Pesa zipo inje inje lakini Heche na wenzake hawataki
 
nimekua nikishauri hili swala kwa miaka 17 mfululizo nikijaríbu kuwashauri chadema,wabàdili mbinu,wajenge chama,waeneze matawi ya chama hadi vijijini huko,tatizo wangdhani siasa za uhasama zitawaingiza ikulu,kutukana,kuzushia vifo viongozi walioko madarakani ni kupoteza muda tu,,wao wajenge chama,waeleze sera zao kwa wananchi na kwa lugha ya kistaarabu,wananchi watawaelewa tu,hakuna mtu ataunga mkono watu wanaochochea vita vya wenyewe kwa wenyewe,watu wanataka utulivu,waendelee na maisha yao na family zao
Hivi kuna chama kilichojengwa tanzania kuliko chadema
 
Anayoyasema yenye hoja yapi??
Hoja ya Utayari wa kupigania kinachopiganiwa.

Hoja ya Lema ni kuwa kuna idadi ndogo yenye utayari na idadi kubwa isiyo na utayari. Hii idadi kubwa inasubiri idadi ndogo ijitoe kafara isiyo na matokeo yanayotosha kupata kinachopiganiwa. Madai yake ni kuwa he is now matured enough to understand that.

Binafsi naona ana hoja ila hoja yake haisafishi usaliti wake kama upo.
 
Chuki ugonjwa Chuki ugeuka Pepo chafu Shetani mwisho Pepo linakutuma kutenda jambo baya mwisho majuto ni mjukuu

Ndiocho Chadema wanachopitia kupitia project yao ya Chuki Chuki matusi kwa watawala mwisho wanadakwa majuto mjukuu utasikia free nyumbu free nyumbu‼️

Swali kwani lazima kutukana watawala ndio kufanya Siasa ✍️
 
Mbona hatusikii kukamatwa wanachama wa ACT na vyama vyengine
Lkn pia hatusikii ACT na vyama vyengine kutukana viongozi wetu

Sasa Chadema matusi
ndio Siasa kuu!!!

Wakidakwa bado kelele nyingi hoh sio Demokrasia wanatukamata free yule free yule

Ujinga mtupu :BanHammer:

Fanyeni Siasa kama vyama vyengine vya Siasa
Tuone kama kuna mtu atakimbia popote kuishi kiwasiwasi kama zigo la Bangi 🤠
 
Inashangaza sana. Mtu mwovu au muongo anapojitetea ataongea maneno mengi ya kweli ili kukupumbaza ila msikilize makini utapata ujue uovu wake.
Kumwamini Lema inabidi utulie sana, kuna maeneo ni kama hayupo pamoja na wenzake, kuna maeneo unamwona anakipenda chama... Kumwelewa labda uwe unaujua ukweli.
 
Back
Top Bottom