Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Hayo muulize Nabii Lema, yeye ndio alikuwa anasema kwa mbwembwe na kejeli kuwa Rais atakufa kabla ya 2020, leo analia lia kwa sababu ya kuto kusalimiwa tu. Unafiki utamuumiza Lema.

Kwa taarifa yako kile alichosema Lema dhidi ya rais hivyo ni vijembe vya kisiasa. Kwa mtu anayejua siasa za ushindani bila mihemko ilikuwa ni jambo la kawaida sana. Ila kwa kuwa jamaa hajui siasa za ushindani na vijembe vyake ndio maana unaona anasema wabunge wa chama chake wasisalimiane na wa upinzani. Huo ni ushamba wa kisiasa na kiburi cha madaraka, pia nitawashangaa wabunge wa ccm kama wanaweza kupangiwa mambo ya kijamii na mtu mwingine kwa ajili ya tabia zake binafsi.
 
E]
Shida kubwa ya Watz ni kutofanya kile tulichotumwa na Mwenyezi Mungu kufanya. Watz tunapenda sana kujituma wakati ukweli ni kwamba Muumba wetu alituumba kila mmoja wetu na jukumu lake hapa duniani/nchini/familia.
Amini amini nakuambia Mh. G. Lema ni landmark ya kukombolewa kwa taifa letu. Kama imefikia hatua ya mtu wa chama A anapigwa biti kutaka au kwenda kumuona mtu wa chama B mwenye matatizo,hakika hiyo haitatuacha salama kabisa. Naamini huu ni mwanzo wa kufunguka akili kwa wale ambao wamepigwa biti na kwa wengine wa upande wa pili. Sasa hapo kweli kuna salama?
 
Baba mtakatifu John Paul II, dec 28 1983, alimtembelea gerezani Mehmet Ali mtu aliyetaka kumuua kwa kumpiga risasi.

http://i.amz.mshcdn.com/dDkGdlz8qBU...p-content/uploads/2015/09/popeassassin-12.jpg

Jamani watanzania tukemee kauli aliyotoa mkuu kwa nguvu zetu zote kabisa, wakristu hasa wakati huu wa kwaresima tunahimizwa kuwajali,kuwatembelea, kuwafariji wenye mahitaji ( wagonjwa, wafungwa n.k) bila kujali wanaumwa nini au wako jela kwa kosa gani.
 
Maisha katika awamu hii ni mazuri kuliko kipindi chochote - Polycap Pengo .
 
Mna wakati mgumu sana upinzani safari hii msipo simama pamoja na kuweka tofauti zenu pembeni sijui hali itakuwaje
I can see this dangerous situation ahead of us. But we as Christians and servants of God have nothing else we are obliged to do more than praying our excellency the honourable President. He needs God's wisdom like what provided to Suleiman
 
Na upinzani munawajibu wa kuhubiri haya uliyoyasema kwa wanachama wa wapenzi wenu, Chadema mna wanachama na wapenzi wenye chuki kwa serikali na dola kwaujumla. Kila mmoja anamuhitaji wenzake kwa njia moja au nyingine.
Kuchukia serikali mara nyingi huwa ni ukosoaji wa approach ya serikali kwenye mambo mbalimbali. Na actually, kuichukia serikali au lichama fulani haiwezi kuwa sawa na himizo la kuchukiana wananchi wenyewe kwa wenyewe!
 
Mmh! Mpaka roho imeniuma binafsi kwakweli. Inamaana kama inefikia mahali wabunge kwa kutojali itikadi za vyama vyao wanataka kuungana kufanya kitu flani kwa maslahi ya taifa ni nongwa? Huku tunakoelekea Mungu atuvushe salama maana naona ishara ya kiza Nene kwa hakika.


Sioni tofauti ya kumjulia hali mtu aliyetoka jela na yule aliyefiwa, maana kukaa jela unatengashwa na familia zako,ndugu jamaa na marafiki zako ni kama kikitenganisha kichwa na kiwiwili! hii yote miwili ni sawa na misiba tu.

Baba anapofikia mahali anawazuia watoto wake kwenda kuwasalimia majirani kwa sababu tu wana itikadi tofauti hali hii huzaa chuki, mwendelezo wa ubaguzi na hata kususiana kwenye shughuli muhimu za kijamii kama misiba, sherehe nk.


Kuna kila dalili kua akifariki kiongozi au kada wa CCM atazikwa na wenzake wa CCM, akifari kada wa CHADEMA/CUF/NCCR basi tazikwa na wenzake, hili halina ubishi tusubiri muda ni ushahidi mzuri wa matendo.

Ziko wapi busara za viongozi wa dini kukemea haya? Wanaogopa kitu gani? Hawaoni kua ipo siku ikitoea chuki miongoni mwa jamii wao ndio wataulizwa mbele za Mungu baba? Wanasubiri nini kukemea haya yasiwe yanajirudia?


Ziko wapi busara alizotuasa baba wa taifa Mwl Nyerere juu ya kulijenga taifa la watu wenye Upendo,amani umoja na mshikamano?Ni nani asimame kunukuu maneno yake katika kukemea viashiria vyenye harufu ya kutubagua sisi wanandugu wa damu moja?


Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.
 
Na upinzani munawajibu wa kuhubiri haya uliyoyasema kwa wanachama wa wapenzi wenu, Chadema mna wanachama na wapenzi wenye chuki kwa serikali na dola kwaujumla. Kila mmoja anamuhitaji wenzake kwa njia moja au nyingine.
ukikosoa serikali unawekwa na serikali kwenye kundi la maadui wake!. wapinzani wanalo awamu hii..........
 
Mbona ilianza mda tu?!
 
Wewe hujui unalolitetea, huyu ni Rais wa nchi analolisema ni maagizo kwa viongozi na umma !!

Hawa jamaa wamejaa chuki ajabu , Mimi binafsi nimewahi kupenya kwenye vikao vyao ngazi ya wilaya fulani nilishuhudia mshereheshaji wao akiwaambia uchaguzi si jambo la huruma na kucheka ikibidi kuua ua mradi chama kishinde. Sasa haya yanatokea kwa mheshimiwa inaakisi maagizo toka juu kwa watendaji ,jambo ambalo si fair
 


Mh. Lema umeandika vizuri, ila umemalizia kwa woga sana. Sasa kama kila mtu anaanza kumwogopa hivyo, hadi nyie wabunge, sisi wananchi tutafanyaje. Kumplease mtu pasipohitajika ni udhaifu sana.
 
Inamaana mtu wa ccm asioe wa cdm? Tutaachiana hata soda kwenye meza. Yangu macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…