Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Lema: Mh. Rais, Vyama vya siasa sio uadui

Hayo muulize Nabii Lema, yeye ndio alikuwa anasema kwa mbwembwe na kejeli kuwa Rais atakufa kabla ya 2020, leo analia lia kwa sababu ya kuto kusalimiwa tu. Unafiki utamuumiza Lema.

Kwa taarifa yako kile alichosema Lema dhidi ya rais hivyo ni vijembe vya kisiasa. Kwa mtu anayejua siasa za ushindani bila mihemko ilikuwa ni jambo la kawaida sana. Ila kwa kuwa jamaa hajui siasa za ushindani na vijembe vyake ndio maana unaona anasema wabunge wa chama chake wasisalimiane na wa upinzani. Huo ni ushamba wa kisiasa na kiburi cha madaraka, pia nitawashangaa wabunge wa ccm kama wanaweza kupangiwa mambo ya kijamii na mtu mwingine kwa ajili ya tabia zake binafsi.
 
E]
Shida kubwa ya Watz ni kutofanya kile tulichotumwa na Mwenyezi Mungu kufanya. Watz tunapenda sana kujituma wakati ukweli ni kwamba Muumba wetu alituumba kila mmoja wetu na jukumu lake hapa duniani/nchini/familia.
Amini amini nakuambia Mh. G. Lema ni landmark ya kukombolewa kwa taifa letu. Kama imefikia hatua ya mtu wa chama A anapigwa biti kutaka au kwenda kumuona mtu wa chama B mwenye matatizo,hakika hiyo haitatuacha salama kabisa. Naamini huu ni mwanzo wa kufunguka akili kwa wale ambao wamepigwa biti na kwa wengine wa upande wa pili. Sasa hapo kweli kuna salama?
 
Baba mtakatifu John Paul II, dec 28 1983, alimtembelea gerezani Mehmet Ali mtu aliyetaka kumuua kwa kumpiga risasi.

http://i.amz.mshcdn.com/dDkGdlz8qBU...p-content/uploads/2015/09/popeassassin-12.jpg

Jamani watanzania tukemee kauli aliyotoa mkuu kwa nguvu zetu zote kabisa, wakristu hasa wakati huu wa kwaresima tunahimizwa kuwajali,kuwatembelea, kuwafariji wenye mahitaji ( wagonjwa, wafungwa n.k) bila kujali wanaumwa nini au wako jela kwa kosa gani.
 
Maisha katika awamu hii ni mazuri kuliko kipindi chochote - Polycap Pengo .
 
Mna wakati mgumu sana upinzani safari hii msipo simama pamoja na kuweka tofauti zenu pembeni sijui hali itakuwaje
I can see this dangerous situation ahead of us. But we as Christians and servants of God have nothing else we are obliged to do more than praying our excellency the honourable President. He needs God's wisdom like what provided to Suleiman
 
Na upinzani munawajibu wa kuhubiri haya uliyoyasema kwa wanachama wa wapenzi wenu, Chadema mna wanachama na wapenzi wenye chuki kwa serikali na dola kwaujumla. Kila mmoja anamuhitaji wenzake kwa njia moja au nyingine.
Kuchukia serikali mara nyingi huwa ni ukosoaji wa approach ya serikali kwenye mambo mbalimbali. Na actually, kuichukia serikali au lichama fulani haiwezi kuwa sawa na himizo la kuchukiana wananchi wenyewe kwa wenyewe!
 
Mmh! Mpaka roho imeniuma binafsi kwakweli. Inamaana kama inefikia mahali wabunge kwa kutojali itikadi za vyama vyao wanataka kuungana kufanya kitu flani kwa maslahi ya taifa ni nongwa? Huku tunakoelekea Mungu atuvushe salama maana naona ishara ya kiza Nene kwa hakika.

Sioni tofauti ya kumjulia hali mtu aliyetoka jela na yule aliyefiwa, maana kukaa jela unatengashwa na familia zako,ndugu jamaa na marafiki zako ni kama kikitenganisha kichwa na kiwiwili! hii yote miwili ni sawa na misiba tu.

Baba anapofikia mahali anawazuia watoto wake kwenda kuwasalimia majirani kwa sababu tu wana itikadi tofauti hali hii huzaa chuki, mwendelezo wa ubaguzi na hata kususiana kwenye shughuli muhimu za kijamii kama misiba, sherehe nk.

Kuna kila dalili kua akifariki kiongozi au kada wa CCM atazikwa na wenzake wa CCM, akifari kada wa CHADEMA/CUF/NCCR basi tazikwa na wenzake, hili halina ubishi tusubiri muda ni ushahidi mzuri wa matendo.

Ziko wapi busara za viongozi wa dini kukemea haya? Wanaogopa kitu gani? Hawaoni kua ipo siku ikitoea chuki miongoni mwa jamii wao ndio wataulizwa mbele za Mungu baba? Wanasubiri nini kukemea haya yasiwe yanajirudia?

Ziko wapi busara alizotuasa baba wa taifa Mwl Nyerere juu ya kulijenga taifa la watu wenye Upendo,amani umoja na mshikamano?Ni nani asimame kunukuu maneno yake katika kukemea viashiria vyenye harufu ya kutubagua sisi wanandugu wa damu moja?

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.
 
Na upinzani munawajibu wa kuhubiri haya uliyoyasema kwa wanachama wa wapenzi wenu, Chadema mna wanachama na wapenzi wenye chuki kwa serikali na dola kwaujumla. Kila mmoja anamuhitaji wenzake kwa njia moja au nyingine.
ukikosoa serikali unawekwa na serikali kwenye kundi la maadui wake!. wapinzani wanalo awamu hii..........
 
Mmh! Mpaka roho imeniuma binafsi kwakweli. Inamaana kama inefikia mahali wabunge kwa kutojali itikadi za vyama vyao wanataka kuungana kufanya kitu flani kwa maslahi ya taifa ni nongwa? Huku tunakoelekea Mungu atuvushe salama maana naona ishara ya kiza Nene kwa hakika.

Sioni tofauti ya kumjulia hali mtu aliyetoka jela na yule aliyefiwa, maana kukaa jela unatengashwa na familia zako,ndugu jamaa na marafiki zako ni kama kikitenganisha kichwa na kiwiwili! hii yote miwili ni sawa na misiba tu.

Baba anapofikia mahali anawazuia watoto wake kwenda kuwasalimia majirani kwa sababu tu wana itikadi tofauti hali hii huzaa chuki, mwendelezo wa ubaguzi na hata kususiana kwenye shughuli muhimu za kijamii kama misiba, sherehe nk.

Kuna kila dalili kua akifariki kiongozi au kada wa CCM atazikwa na wenzake wa CCM, akifari kada wa CHADEMA/CUF/NCCR basi tazikwa na wenzake, hili halina ubishi tusubiri muda ni ushahidi mzuri wa matendo.

Ziko wapi busara za viongozi wa dini kukemea haya? Wanaogopa kitu gani? Hawaoni kua ipo siku ikitoea chuki miongoni mwa jamii wao ndio wataulizwa mbele za Mungu baba? Wanasubiri nini kukemea haya yasiwe yanajirudia?

Ziko wapi busara alizotuasa baba wa taifa Mwl Nyerere juu ya kulijenga taifa la watu wenye Upendo,amani umoja na mshikamano?Ni nani asimame kunukuu maneno yake katika kukemea viashiria vyenye harufu ya kutubagua sisi wanandugu wa damu moja?

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.
Mbona ilianza mda tu?!
c2e9cab3f17c0351e0ccc4cb41abd99b.jpg
 
Kama kawaida yetu chadema kuendeshwa kwa matukio...la baishite limewatoa sasa mmepata kauli ya Rais mmepata pa kutokea...

Suala la kuhubiri upendo ni la kila mtu....sio la Magufuli peke yake. Huwezi kujifanya bingwa wa kutabiri kwa kumsemea kifo Rais halafu acheke kwa kufurahi kuwa 2020 atakuwa amekufa...hii kauli mbona machademaa hamkuipinga?

Ni wazi chadema na wanachama wenu mmekuwa mkionesha chuki ya dhahiri kwa viongozi wa CCM kiasi cha kuingilia faragha zao kuwa Makonda kwanini hajapata mtoto na kumkejeli kwa kukosa mtoto wakati ni kazi ya Mungu kukupa mtoto au la....huu ni upendo?

Kuna watu wenye chuki kama nyie? Mtu akirudisha mapigo kwa njia ileile mnatoa mapovu.

Halafu kuna anaye wazidi kwa kauli mbovu hasa Lemaa....mtu unaongea kama sio kiongozi bana. Okey, nashukuru naona umetoka getezani walau ukiwa umejifunza kitu. Basi uendelee hivyohivyo na kuhubiri upendo na sio chuki.

Wananchi tusiwahubiri kana kwamba tunaishi jahanamu wakati hio Serikali unayotukana ni watu kama wewe....wanakasirika na uwepo wa demokrasia hauwazuii kukasirika.

Tuhubiri upendo, mshikamano na umoja. Masuala ya watu wanayonena ndani ya vikao vyao hayatuhusu. Labda kama statement hio Rais angeizungumza hadharani....
Wewe hujui unalolitetea, huyu ni Rais wa nchi analolisema ni maagizo kwa viongozi na umma !!

Hawa jamaa wamejaa chuki ajabu , Mimi binafsi nimewahi kupenya kwenye vikao vyao ngazi ya wilaya fulani nilishuhudia mshereheshaji wao akiwaambia uchaguzi si jambo la huruma na kucheka ikibidi kuua ua mradi chama kishinde. Sasa haya yanatokea kwa mheshimiwa inaakisi maagizo toka juu kwa watendaji ,jambo ambalo si fair
 
Mh Rais Magufuli nakusalimu.

Nimetoka Magereza hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

Mh Rais, nimeona kwenye vyombo vya habari leo kuwa kwamba wale Wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa Magereza kuwa ni wasaliti wa chama cha CCM, Mh Rais wengi walinisalimia, Wachungaji, Masheikh, Wabunge na Viongozi mbali mbali, sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yoyote haswa wakati wa matatizo.

Mh Rais, nimeogopa sana kwa kauli hii yako, je Taifa linakwenda wapi, hivi kweli sisi Wabunge ni maadui? Kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu, basi bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya .

Dhambi hii ikikomaa basi ni hakika kwamba lugha za udini, ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa, ni muhimu sasa tukajenga utamaduni wa kuhimiza mshikamano wa Kitaifa bila kujali itikadi kama kweli tunawapenda masikini na wanyonge wa nchi hii.

Nawaomba Wabunge wenzangu walionijali wakati niko magereza wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu, ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa kauli juu ya kauli yako.

Mh Rais wakati wa Msiba wa Christina Lissu dada yake na Mh Tundu Lissu nilikuona katika msiba ule wewe na Mama yetu Mke wako, je Mh Rais na wewe ulikuwa unasaliti Chama chako?

Mh Rais neno la Mungu linasema, Wapendeni maadui zenu, waombeni wanaowauzi , wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu.

Mungu akubariki sana, natumaini Mh Rais sitakamatwa leo kwa ujumbe huu mfupi.

Godbless J Lema (MB)

Mh. Lema umeandika vizuri, ila umemalizia kwa woga sana. Sasa kama kila mtu anaanza kumwogopa hivyo, hadi nyie wabunge, sisi wananchi tutafanyaje. Kumplease mtu pasipohitajika ni udhaifu sana.
 
Inamaana mtu wa ccm asioe wa cdm? Tutaachiana hata soda kwenye meza. Yangu macho.
 
Back
Top Bottom