Lema: Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa au wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo nitaomba radhi

Lema: Nikimuona mtoto wa Waziri Mkuu Majaliwa au wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo nitaomba radhi

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi...
Sidhani kama amekuja kwa lengo la kukijenga chama chao huenda kuna ajenda ya kukidumaza hicho chama.

Je, yeye Lema amewahi muona mtoto wa Waziri mkuu anashona viatu?

Je, anaweza kutuonesha mtoto wa Rais Mwinyi ambaye ni Mwl.wa S/Msingi?

Kwa mantiki yake ni kuwa kazi zote zinazofanywa na watu wa kipato cha chini ni laana kwa kuwa hakuna watoto wa viongozi wakuu wa Nchi wanaozifanya.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi...
Angeshauri sasa kazi gani ndio inayofaa au ni namna gani ya kuifanya hii ifae. Maana bodaboda wamekuwa msaada mkubwa sana hasa sisi tunaoishi uswahilini wamekuwa wakipeleka wagonjwa wetu mahospitali hata usiku wa manane na pia wamekuwa wakituwahisha kwenye mishe mishe zetu.

Sasa kama mtu anasema hii kazi haifai kufanywa na watu anataka ifanywe na nani? Sidhani kama yeye huwa anatumia huu usafiri.

Kazi yeyote mtu anayoifanya kwa furaha na hakuombi ugali wako muheshimu, kwa hiyo omba omba ndio kazi ya heshima?
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi...
Je, Lema anataka wafanye kazi zipi za maana? Au nao waanze kutumia domo kaya kupiga kelele ili wawe wabunge?Au wakawe wezi wa magari? Tunaomba jibu Lema.
 
Lema aache dharau aisee ni ujinga kudharau kazi za watu
Hajadharau

Sisi kama Bodaboda tumemuelewa na huo ni ukweli, hakuna mtu aliyekuwa na malengo yakuja kuwa Bodaboda

Ni kazi yenye msoto sana na kuishi katika risk, hao mamwela wa CCM wamekuwa kero tukiwa road

Bado uhai wetu upo rehani kwa manyemela wanaotuwinda kuja kutuibia pikipiki zetu.

Ni kazi ambayo wengi tunafanya ili tufanikiwe tuje kuachana nayo.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Lema amesema endapo atamuona mtoto wa Waziri mkuu mh Majaliwa au mtoto wa Rais Mwinyi anaendesha Bodaboda ndipo ataomba radhi...
Lema aache ushamba. Mtoto wa PM ataendaje kuendesha boda boda? Ndiyo maana kwenye jamii kuna matabaka.

Kuna waendesha boda boda na kuna Wahandisi, kuna walimu na mama ntilie, kuna wabunge na wapiga kura, kuna watawala na watawaliwa.

Sasa mtoto wa pm ni privileged hana sababu ya kuwa boda boda, lakini hiyo haifanyi kuendesha boda kuwa siyo kazi. Atulize hicho kichwa chake au wamempa crack huko Canada?
 
Tukitoka kwa bodaboda tuje kwa
Walimu
Manesi
Watunza rekodi
Askari
Madereva
Na wengine wengi na pia tujue watoto wa mbowe lisu lema
Rais wangu Spunda Rungwe
Raisi Samia
Raisi kikwete wanafanya kazi zipi

..Mzee Mwinyi mwanae ni Raisi kule Znz.

..Mzee Mkapa mwanae ni Katibu Mkuu wa wizara.

..Mzee Kikwete mwanae ni Naibu Waziri.

..Mama Samia mwanae ni Mbunge.

..Sasa viongozi wa aina hiyo ndio wanatushauri wenetu wawe bodaboda.
 
Watu wanakomaa kuwa Ni Ajira. Wanadai kuwa inatakiwa uwe na akili kubwa umuelewe Lema.

Ingawa huu usafiri upo maeneo ya kimasikini hata Asia wamejaa
 
Back
Top Bottom