Ukiwa ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za Bongo wala huwezi kushangazwa na hukumu hii. Na kwa jicho la ndani ukiwa mfuatiliaji mzuri wa siasa za bongo ni kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa wahusika kuachiwa kwa makosa mengine yaliyobaki kwa kile kinachoitwa ' Mwendesha mashtaka hana nia ya kuendelea na kesi hizo'.
Serikali kwa mara nyingine ijitathmiini katika uwezo wa Idara na Taasisi zake kutayarisha kesi na mashahidi kwani zimefeli hivyo kushindwa ku-i-move Mahakama Kuu kuwa kulikuwa na kesi ya kusikilizwa kwa kutumia mizania ya kisheria.
Je tatizo ni kukosekana wanasheria wa serikali walioiva ? Je mfumo haki jinai (criminal justice system) yaani Polisi, TAKUKURU, DPP na Mahakama za chini zinakosa rasilimali watu wabobevu wa kuchunguza, kuandaa na kusikiliza tuhuma / kesi toka mwanzo wa mchakato mzima wa kutoa haki Au kesi hii ilikuwa kuna shindikizo?
Jaji wa mahakama kuu amesema rufaa ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai kisha kusingiziwa ameiba simu aina ya Tecno na pesa laki tatu na sitini na kufungwa miaka 30 jela Lengai Sabaya itaanza kusikilizwa 13/12/2021 mfululizo mpaka haki itakapopatikana. === Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Butamo...
www.jamiiforums.com
06 May 2022
Arusha, Tanzania Hukumu ya Jaji Ezedekia Kisanya wa Mahakama Kuu ya Tanzania :
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemuachia huru aliyekuwa DC wa Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamekata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 kwenda jela kila mmoja kwa sababu mbalimbali kwakuwa Mrufani namba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri na kutokufanya hivyo kunawanyima haki yao msingi.
Jaji Ezedekia Kisanya amesema kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ikiwemo kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili.
Jaji amesema Lengai Ole Sabaya na wenziwe, watakuwa huru endapo watakuwa hawana kesi nyingine kwenye Mahakama yoyote
Mkuu, Utawala wa Haki Jinai Kwa Ujumla Umejikita Katika Kanuni Kuu Zifuatazo:-
i. Lazima kuwepo na sheria inayoainisha kwa uwazi kwamba matendo flani yanapofanywa na watu kuwa ni jinai.
ii. Sheria hiyo lazima pia ianishe adhabu kwa matendo hayo ambayo ni makosa ya jinai.
iii. Wajibu wa kuthibitisha shitaka dhidi ya mshitakiwa ni wa yule anyelalamika, na kwa Tanzania ni Jamhuri, hivyo upande wa mashitaka unapaswa kuthibitisha shitaka lake dhidi ya mshitakiwa pasipo kuacha shaka.
iv. Mtuhumiwa atachukuliwa kuwa hana hatia mpaka itakapodhibitika hivyo.
v. Mtu yoyote hatapelekwa gerezani pasipo kufikishwa kwanza Mahakamani.
Maeneo yote manne yana matatizo katika msingi wa Haki Jinai Tanzania.
.
Na ndio maana kuna muda niliandika kwamba chain ya Jinai mpaka inafika mahakamani inahusisha vyombo vingi katika kuanzia upande wa Upelelezi wa Kesi mpaka kuunda kesi.
Nimeona ndugu zake wanalia sn.Wamkanye mtoto wao,na wamfunde suala la kuumiza watu na kuwapa vilema.Kwanza akitoka aombe radhi na akome kutafuta vyeo kwa kuumiza watu.
Kama wanafanya mchongo atoke,basi saa hii huku uraiani atakutana na "asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu"
Loohh... huna information ndugu. Ana kesi nyingine ya uhujumu uchumi ambayo haina dhamana na inasubiri hukumu tarehe 30 mwezi huu May. Amerudi ndani kusubiri hukumu hiyo. Baada ya hizi za Arusha, kuna kesi zinaandaliwa na TAKUKURU Kilimanjaro.
Mkuu unachosema ni kweli kabisa kwamba watu waangalie hukumu inasema nini, kwa bahati mbaya zama hizi si zile za Mahakama tulizokuwa nazo.
Hakuna shaka yoyote kwamba mahakama zetu zimepoteza credibility na integrity.
CJ aliposimama na kusema hukumu zizingatie mihimili mingine alipigilia msumari wa mwisho.
Confidence na Mahakama zetu imekuwa eroded katika kipindi hiki. Mfumo mzima
Lakini si mahakama tu, DPP naye aliposimama kumkingia kifua Makonda ilieleza jambo
Ni watu wangapi, masikini, viongozi, maarufu au matajiri waliowahi kukingiwa kifua na DPP
Ni kwa mantiki hiyo Sabaya alikiri kushiriki na kutumwa na wakubwa hawezi kuachwa aozoe magereza.
Kuna kundi la vijana waliokuwa na kazi maalum, lina siri nzito sana vifuani mwao.
Mahakama inatumika kama JIKI
Jamani mifumo yetu yote imeoza, ndio maana tunataka katiba mpya kuihuisha.
Mahakama ni mmjoa wa mifumo iliyopoteza imani ya umma
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.