Habari Wanajukwaa;
Kama tunavyo fahamu leo Mahakama kuu Mkoani Arusha imempa ushindi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya hai, Lengai Ole Sabaya, dhidi ya Jamhuri katika kesi yake ya unyang'anyi wa kutumia silaha aliyokuwa amehukumiwa miaka 30 Jela.
Sabaya ameshinda rufaa hii bila ya kuwepo hashtags, harakati au kelele zozote katika mitandao ya Kijamii kama Twitter, Instagram au Facebook. Hii nitofauti na kesi kadhaa za Watu maarufu zilizofanana na hizo kama kesi ya Mh. Mbowe, Kutopea kwa Azori Gwanda, Kutekwa na kupigwa kwa Mdude Chadema na n.k
Katika kesi kama ya Mh. Mbowe, kunako mtandao wa Twitter kulichafukwa na hashtag za #MboweSiGaidi na nyingine kama hizo ila kwa Sabaya ameshinda hii rufaa kimya kimya bila longo longo.
Mimi nimejifunza kuwa siyo kila kelele inayopigwa kwenye mitandao ya Kijamii inaweza leta mabadiliko, kwa Maana Mh. Mbowe alitoka kwa amri ya DPP na siyo kwa hashtags za Twitter. Pia nimejifunza kuna Mawakili wako smart sana katika kuhudumia Wateja wao bila ya mbwebwe kama wale Mawakili maarufu waliokuwa wanasimamia kesi ya Mh Mbowe!
We umejifunza nini kwenye rufaa ya hii kesi?