TUJIKUMBUSHE
CHAPTER 16 - Tupitie tuone yaliyomo
Section 39, Subsection (2):
Mtu yeyote ambaye, akiwa na utii kwa Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au mahali penginepo, ana nia ya kutenda au kusababisha kutendwa, au ana nia ya kuchochea, kushawishi, kutoa ushauri au maelekezo kwa mtu yeyote au kundi la watu kutenda au kusababisha kutendwa kwa kitendo, tendo au lengo lolote kati ya yafuatayo, yaani
(a) kifo, ulemavu au kujeruhiwa, au kufungwa gerezani au kuzuiliwa uhuru wa Rais;
(b) kumwondoa Rais madarakani kwa njia zisizo halali kutoka katika wadhifa wake wa Urais au kutoka katika hadhi, heshima na jina la Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;
(c) kupindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa njia zisizo halali; au
(d) kutisha au kuogofya Mhimili wa Serikali (Utendaji), Bunge au Mahakama ya Jamhuri ya Muungano,
na akaonyesha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi au nyenzo yoyote iliyochapishwa au kwa kitendo au tendo lolote la wazi, anakuwa ametenda kosa la uhaini na akitiwa hatiani, atahukumiwa adhabu ya kifo.