Leo 16 September Mahakama inaendelea kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Leo 16 September Mahakama inaendelea kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Kwenye kesi ya uhaini ya mwaka 1969 na ile ya mwaka 1983 watuhumiwa waliotiwa hatiani hawakuhukumiwa adhabu ya kifo bali kifungo cha maisha japo hawakukaa zaidi ya miaka 10 kabla ya kuachiliwa huru.

Ina maana mahakama ina uwezo wa kuamua ihukumu adhabu gani kati ya kifo na maisha.

Tofauti ya wakati ule na sasa ni kwamba majaji wa enzi hizo walikuwa na mamlaka kamili kisheria na walikuwa huru kufanya kazi yao pasipo na shinikizo lolote kutaka kwa mtawala tofauti kabisa na hali ilivyo sasa ambapo mahakama zinafanya kazi kwa kufuata matakwa ya serikali iliyoko madarakani.
 
Wewe nawe unaonekana mweupe kabisa kichwani.

Mahakama ina mamlaka ya kumuita shahidi mahakamani aje atoe ushahidi ikiwa imeona ushahidi wake utasaidia maamuzi sahihi kufikiwa na mahakama.

Summons imetolewa na mahakama hivyo ni jukumu la mahakama kuhakikisha wito iliyotoa unatekelezwa na usipotekeleza ifauata arrest warrant na pia kuna kesi ya contempt of court.

Vitu vidogo tu unashindwa kuelewa.
Machawa wa mboga mboga ni tupu kichwani kwao, na sifa kuu ya uwe chawa wa Veggies basi uwe mpumbavu na mjinga.

Ni wa kuwapuuza tu.
 
Unatumaje barua adress makao makuu ya chama !!

At the same time chama umekifungia. !!

office zilikua zimefungwa. Hakuna wa kupokea barua .

Mnafanya vitu kitoto sana. STUPID 🚮
Baba levo alisha sema kucheza na chadema kwenye sheria ni kujitafuta balaa ,chama kina mawakili kila sehem , vipi wakaapo nakuunganisha nguvu moja ? Na kila wakili anaweka kifungu mezani na hoja ? Hii chama ccm kubalini yaishe .
 
Reference ipo km mashahidi hawato tii wito wa mahakama, kuna kanuni na taratibu zake, ila kwa umuhimu wa case hii, hatuhitaji hilo, tunataka mashahidi waje wenyewe mahakamani kutolea ushahidi wao..
Ndio maana nikasema wakamatwe na waletwe kwa nguvu, japo sio lazima.
Mwaka mmoja nilimwekea mtu dhamana mahakamani akawa anakaidi kwenda kwenye kesi yake nilitafutwa vibaya mno ,uzuri nilikua hospital nmelazwa ila huwezi hamini siku napewa discharge wajomba wale , kama sio hivyo ningefungwa, jamaa alikula miezi 6 kwa ujinga wa kutoheshim mahakama.

So mashahidi lazima wafike, kama wako nje ya nchi wakamatwe kwa order ya mahakama waje kutoa ushahidi
 
Mwaka mmoja nilimwekea mtu dhamana mahakamani akawa anakaidi kwenda kwenye kesi yake nilitafutwa vibaya mno ,uzuri nilikua hospital nmelazwa ila huwezi hamini siku napewa discharge wajomba wale , kama sio hivyo ningefungwa, jamaa alikula miezi 6 kwa ujinga wa kutoheshim mahakama.

So mashahidi lazima wafike, kama wako nje ya nchi wakamatwe kwa order ya mahakama waje kutoa ushahidi
Haswaa, wakamatwe kwa order ya arrest warrant.
 
Watu wakafikiri hawa watatokaje hapa, tuseme wamesafiri nje ya nchi, na asionekane hata mmoja kwenye shughuli yeyote mpaka pale tutakapowaambia.
 
Saa 3 kamili tayari watu wameshadika Mahakamani



Kaa tayari kwa updates


========

Leo September 16, 2026

Last time tuliishia sehemu ya 428

Sehemu ya 429

Mahakama imeanza.

Imepigwa high coooooourt

Majaji wameingia.

Mhe. Lissu nae ameingia kama kawaida makofi mengi yanapigwa mengi kwa ajili ya kumkaribisha Mwenyekiti Tundu Lissu.

Katuga anawatambulisha wenzake.

Jaji Ndunguru anasema tuendeleee.

Anasimama Mhe. Tundu Lissu anasema naomba kuzungumza kidogo na shahidi wangu naona amenitumia ujumbe hapa kabla hatujaendelea na nitamfuata.

Wanaenda kuzungumza Mhe. Lissu na Mhe. Heche pale kwa dakika kama tatu. Wanaongea na kutikisa vichwa wamekubaliana wamemaliza na Mhe. Lissu anarejea kwenye kizimba chake.

Majaji wanazungumza kama dakika tano sijui wanajadili nini?

Mhe. Lissu: Shahidi kuhusu suala la Utekaji na ripoti ya SADC.

Heche: Hilo suala la Utekaji ukurasa wa 6 wa ripoti hiyo unazungumzia masuala ya Utekaji.

Katuga: Ukurasa wa 6 hakuutaja wakati wa kutoa ushahidi huo.

Mhe. Lissu: Tusipotezeane muda toa neno ukurasa wa 6.

Heche: Suala la Utekaji lipo kwenye ripoti ya SADC ukisoma utaona.

Mhe. Lissu: Ulisema maneno ya utekaji, kukinukisha kwamba sio kila mahali nilitumia hayo fafanua?

Heche: Nilimaanisha maudhui ni yaleyale kuzungumzia mfumo wa Uchaguzi. Choice of words tu ndio lilikuwa ni suala linalotofautiana.

Mhe. Lissu: Kuhusu Uchaguzi wa Tarime ukasema haukuwa huru na haki na hivyo hupaswi kuwa Mbunge na haukuwa na mamlaka hayo ya kukataa kuwa mbunge au hukuwa na huo uwezo?

Katuga: Hatukuuliza hivyo.

Mhe. Lissu: Rekodi zituongoze.

Jaji: Sikuwa na uwezo wa kukataa kuwa Mbunge

Heche: Ufafanuzi wangu ni kwamba returning officer ndio anatangaza Mbunge.

Mhe. Lissu: Mkurugenzi wa Uchaguzi akawa mgombea na sasa ni Mbunge wa Butiama na ukasema haikuwa sahihi. Fafanua?

Heche: Nilisema kwamba kanuni za CCM zinataka mwanachama wake ili agombee anapaswa kuwa na uanachama wa miaka mitano. Kwahiyo naamini alijiunga na CCM akiwa bado ni Mkurugenzi wa Tume maana asingeweza kuruhusiwa kugombea ikiwa takwa la miaka mitano bado hajakidhi.

Mhe. Lissu: Tume ya Chande uliulizwa kuhusu wewe au Chama kuitwa. Na ukaoneshwa na mabarua mengi lakini ukasema hukuitwa. Fafanua. Usiingize mambo mapya Wakili wa Serikali atanuna.

Heche: Mimi sikupokea barua yoyote ya Mwaliko kutoka tume ya Chande na kuhusu Chama hakikupokea maana kilikuwa kimefungiwa.

Katuga: Kuhusu chama isiingie maana hakusema hivyo.

Mhe. Lissu: Tusomewe record inasemaje?

Jaji Ndunguru: Alipoitwa na tume ya Jaji Chande. Barua ilikuwa ameandikiwa Katibu Mkuu na haikuandikwa kwa Chama.

Heche: Haikuwa addressed kwa Chama.

Mhe. Lissu: Uliulizwa na maswali kuhusu Chama kwenda Bungeni na kutoa maoni kuhusu muswada wa Sheria. Kuhusu kuwaondoa wakurugenzi kusimamia uchaguzi.???

Heche: Bado watumishi wa umma ndio wanasimamia Uchaguzi na mapendekezo yetu yalikuwa ni Tume kuwa na Wafanyakazi wake kuanzia ngazi ya kitaifa hadi chini na sio watumishi wa umma.

Mhe. Lissu: Kuhusu Thabo Mbeki Foundation na Mwalimu Nyerere Foundation tofauti yake. Fafanua

Heche: Thabo Mbeki Foundation inafanya kazi nchi zaidi ya moja tofauti na Mwalimu Nyerere Foundation ambayo inafanyakazi Tanzania tu ndo maana nilisema yenyewe ni International.


Sehemu ya 430

Mhe. Lissu anasema amemaliza maswali ya Re Examination.

Job Mrema amesimama na kusema tunaleta chini ya kifungu cha 156(4) cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6. Mahakama itumie mamlaka yake ili tuweze kumrecall na kufanya further cross examination na kwa mujibu wa kumbukumbu siku ya jana alitoa ushahidi wake hapa Mahakamani kuhusiana na shauri hili na akiwa chini ya kiapo alitoka Mahakamani na kwenda kuzungumza na kuzalisha ushahidi mwingine.

Tunaona ushahidi huo utaisaidia Mahakama kutenda haki na alikwenda kusema akiwa chini ya kiapo. Tupewe nafasi tumuulize maswali kuhusu ushahidi huo aliousema na Naomba kuwasilisha.

Anasimama Mh. Lissu amekunja sana uso. Majaji wanasema kaa kwanza mshitakiwa. tunataka kujua mambo kadhaa.

Jaji Ndunguru anauliza sasa mtu akiapa Mahakamani kwahiyo akienda hata nyumbani anakuwa chini ya kiapo? Hebu tusaidie kuelewa.

Watu wanacheka sana

Job Mrema: Waheshimiwa Majaji kiapo amelala nacho kwasababu alipoapa alikuwa nacho, akifika hapa anaambiwa kiapo chapo kinaendelea. Kwahiyo shahidi huyu afanyiwe further cross examination, sisi tumeangalia ni kwamba moja ya sababu yuko kwenye kiapo na kiapo chake hakijasitishwa, shahidi huyu akiwa bado kwenye kiapo. Amezalisha ushahidi.

Jaji Ndunguru anateta na wenzake hapo.

Jaji Ndunguru: Tulikuwa tunaangalia off record. Cross Examination inatokana na examination in chief sasa kama kitu kimeongelewa huko kwani kipo hapa Mahakamani??? Hilo pia la kwamba kiapo ameenda nacho hadi nyumbani hiyo tafsiri yako haiko sahihi, Ushahidi uko Mahakamani na mnamuuliza mambo yaliyosemwa Mahakamani. Hayo mengine hayapo Mahakamani. Kwahiyo ombi hilo halina mashiko.

Mhe. Lissu anasimama anasema Waheshimiwa Majaji niliomba summons kwa ajili ya mashahidi kwahiyo nataka kujua majibu kuwa mashahidi hao wako wapi na tunakwendaje mbele. Pia siwezi kumuweka shahidi kizimbani kabla sijamuandaa, kwahiyo lazima nikutane nao na niwaelekeze cha kufanya ili wakija kugeuka hapo kizimbani basi niwashughulikie sawasawa.

Eneo la kuwaandalia Mashahidi na kukutana nao ni hapa hapa Mahakamani kwasababu sina eneo lingine ambalo naweza kukutana na mashahidi wangu. Siwezi kwenda ofisini kwao wala gerezani so nilazima tuonane na kupanga hapa hapa Mahakamani.

Jaji Ndunguru anasema tulitegemea utuambie kuwa una shahidi au hauna maana ni mashahidi wako na Mahakama ilishatoa summons kwahiyo tutabreak ili msajili atupatie feedback.

Tukutane saa tano na dakika aroboini.


Sehemu ya 431

Tumerejea Mahakamani.

Imepigwa high court Majaji wanaingia muda huu ili tupate mrejesho wa nini kinaendelea kuhusu wale mashahidi wengine.

Anasimama Katuga anasema Corum yao ni ile ile na mshitakiwa yupo na shauri linaendelea kwa utetezi na sisi tuko tayari.

Anasimama Mhe. Lissu anasema baada ya maelekezo ya Mahakama nimewasiliana na Mhe. Msajili wa Mahakama hii amekuja kuniona na kuniambia kuhusu utekelezaji wa amri ya Mahakama kuhusu kuwaita hao Mashahidi watatu.

Mhe. Msajili amenitaarifu kuwa Mashahidi wote watatu walipelekewa wito Dodoma, hata hivyo haikuwezekana kuwaserve nakala za summons kwasababu wote watatu wapo nje ya nchi. Mhe. Msajili amesema kati ya hao watatu mmoja ambae ni Kamishna Wa Polisi Ramadhani Kingai, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai anatazamiwa kurudi nchini leo.

Na Msajili ameniahidi kwamba siku ya Ijumaa kamishna wa Polisi Kingai atakuwepo Mahakamani ili kutekeleza huo wito wa Mahakama. Wale wengine wawili Jenerali Jacob Mkunda na Wambura IGP hawajulikani watarudi lini?

Katika Mazingira haya napendekeza Mahakama iahirishe shauri leo hadi ijumaa saa nane na nusu Mchana ili ile session ya asubuhi niweze kuitumia kushauriana na huyo shahidi ambae atakuja, ikiwa ni pamoja na kuchukua maelezo yake.

Na natumaini Waheshimiwa Majaji by saa nane na nusu tutakuwa tayari kuendelea nae na kuhusiana na waliobaki itabidi tusubiri tumalizane na huyu tuliyenae ili tufanye maamuzi baadae na hao wengine. La mwisho ninafahamu jinsi ambavyo ratiba ya shauri hili iko tight na naomba niwafahamishe kuwa na sisi twende kwenye final submission ili muweze kukaa baadae kutafakari na kuamua kesi hii.

Vyovyote itakavyokuwa kama watatii wito wa Mahakama ni imani yangu kwamba hatutachukua muda mrefu.Na wasipokuja kabisa hilo litakuwa mikononi mwenu maana nyie ndio mmetoa wito wa wao kuja kutoa ushahidi, Mimi ya kwangu ni hayo Waheshimiwa Majaji.

Katuga kwa masikitiko hatuna pingamizi la kupinga ahirisho na Mahakama ilipoongeza session hii hadi Tar. 18/09

Jaji Nduguru anasema sisi tuliongeza 14 working days.

Katuga: Basi tunaomba Mahakama imsisitize Mshitakiwa Mashahidi wake waweze kufika. Watu wanasonya

Jaji Ndunguru: Sasa jamani hao si mashahidi wa Mshitakiwa mnaguna nini? Mshitakiwa anajua namna ya kufuatilia. Hebu uwe unawaelekeza.

Katuga: Pia kuhusu ombi lake la kwamba wasipokuja hao mashahidi anaiachia Mahakama hilo hawezi kuiachia kwasababu yeye ndio mashahidi wake na Mahakama imeshatoa summons kwahiyo atasema anaiomba nini Mahakama?

Jaji Ndunguru: Anacheka kwamba the court is not your nini ile huwa mnarushiana humu.Majaji wanateta hapo kidogo.Jaji

Ndunguru: Tukutane Ijumaa saa nane kamili mchana.
Inapoonekana huyu jaji Ndunguru naye amejaa uCCM mwingi tu. Mashahidi wamekuwa summoned na mahakama. Wasipotii wito, mahakama ndiye yenye mamlaka ya kuwakamata na kuwaleta kwa nguvu. Sasa Lissu (mshitakiwa) anawezaje kuwaamrisha wafike mahakamani wakati yupo jela? Hii nchi ina mijaji yenye akili za kiquma sana
 
Back
Top Bottom