Leo 16 September Mahakama inaendelea kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Leo 16 September Mahakama inaendelea kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Lissu alipoomba mashahidi waitwe na mahakama alicheza kama Libasse. Kina Mnyika hawajaitwa na mahakama hivyo hata wasingekuja isingekuwa issue. Sasa hao walioitwa na mahakama wasipokuja siyo kwamba wamemmaliza Lissu bali watakuwa wameidharau mahakama.
Pia wakija lazima wakutane na Lissu na awape maelekezo ya kipi cha kuongea na wakiamua kuwa hostile witnesses basi amesema atawashughulikia.
Hawa bi mashahidi muhimu sana maana hawa wana madudu mengi sana na hawana sifa za kuwa kwenye hizo nafasi.
Wakija watakuwa na kiburi ili waoneshe Lissu alihusika na October 29 na hapo ndio wataning'inizwa maana watapigwa maswali mpaka waseme nani alitoa amri ya kupiga watu risasi.
Lissu ana akili sana. Halafu mara zote ni mtu wa kutangulia mbele.
 
Walifika wao wenyewe pindi tu walipotajwa kuhusika na ushahidi, vipi hawa wa 3 ambao hawafiki wenyewe, mahakama si inatakiwa iwape wito? Wanataka kukimbia nini? Jukumu ni la mahakama, wasilete masikhara kwenye jambo la msingi.

Nasemaje, Tusichezeane.
Mashahidi wako unataka mahakama ikusaidie kuwaleta?
 
Ni nani kati ya hao yuko nje ya nchi? Mbona umma hauna taarifa? Halafu majaji na mawakili wasilete upuuzi wao, ndio maana yaanambiwa ni majaji ya CCM halafu yanang'aka, yanachokataa nini wakati wanajionesha wazi kabisa hapa.

Mahakama mfanye mfanyavyo muwalete hao mashahidi ndani ya viunga vyenu, msiletee huo upuuzi wenu wa kumuagushia mshitakiwa, wakati jukumu na wajibu wenu kuwapa summons na wasipotii kanuni na taratibu zifuate.

Tusichezeane.
 
Hii nchi inafurahisha sana. Inawezekana kweli CDF, IGP na DCI wote kuwa nje ya nchi? Wameenda kutalii, au!

Na huyo Kingai aliyeahidi kuja Ijumaa ataweza kukubaliana kweli na masharti ya Lissu? Kwamba akijibu kinyume na matakwa yake (Lissu), anamshughulikia! Hivi haoni hatari itakayomkuta!

Ningekuwa ndiyo mimi, ningeendelea kujificha..
 
Top 3 key players wa maCCM,patachimbika kwa kweli.Mh.Lissu ni kama Dr wa Upasuaji hakosei penye mshono.
Anapasua kwenye kichwa cha jipu dadeki wamepoteana ila si wapo watupe za chini ya kapeti km wapo ofcn kwaooooooo.

Nimeamini macho yanauma yaani wameogopa macho ya wananchi wasiokuwa hata na fimbo dadeki.
 
Back
Top Bottom