Leo 16 September Mahakama inaendelea kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Leo 16 September Mahakama inaendelea kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

TUJIKUMBUSHE

CHAPTER 16 - Tupitie tuone yaliyomo
Section 39, Subsection (2):

Mtu yeyote ambaye, akiwa na utii kwa Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au mahali penginepo, ana nia ya kutenda au kusababisha kutendwa, au ana nia ya kuchochea, kushawishi, kutoa ushauri au maelekezo kwa mtu yeyote au kundi la watu kutenda au kusababisha kutendwa kwa kitendo, tendo au lengo lolote kati ya yafuatayo, yaani

(a) kifo, ulemavu au kujeruhiwa, au kufungwa gerezani au kuzuiliwa uhuru wa Rais;

(b) kumwondoa Rais madarakani kwa njia zisizo halali kutoka katika wadhifa wake wa Urais au kutoka katika hadhi, heshima na jina la Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;

(c) kupindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa njia zisizo halali; au

(d) kutisha au kuogofya Mhimili wa Serikali (Utendaji), Bunge au Mahakama ya Jamhuri ya Muungano,

na akaonyesha nia hiyo kwa kuchapisha maandishi au nyenzo yoyote iliyochapishwa au kwa kitendo au tendo lolote la wazi, anakuwa ametenda kosa la uhaini na akitiwa hatiani, atahukumiwa adhabu ya kifo.
Lissu siyo sehemu ya Serikali ya Jambhuri ya Muungano wa Tanzania.Lissu siyo Mwanaccm wala hahusiki kwa lolote katika vikao mbalimbali vya CCM.Lissu ni CHADEMA chama hasimu wa CCM.Kesi hii inawalazimisha ccm na serikali yake watafute namna ya kumweka Lissu mfukoni mwa ccm ili anyongwe.Cha ajabu uchawi wao ccm hauna madhara hata kidogo labda kwa kina Polepole ,Ndugai,Tulia Acksoni na Emmanuel Nchimbi huko unafanya 100%
 
MKUU WA MAJESHI ANATAKA KUTUPA TAULO.

Taarifa ni kuwa jana zilisambazwa meseji vikosi vyote, briged zote, division pamoja na ditach zote za Jeshi kuwa wasipokee barua yoyote kutoka mahakamani, yaani summons.

Kwa hiyo kuna uwezekano Mkuu wa Majeshi asije kuhudhuria mahakamani kwa sababu elimu yake unga unga mwana, pia anakashfa kibao jeshini. Hata uteuzi wake wanajeshi hawakukubali. Wanasema wanatamani sana afike kizimbani wamjue kiundani, maana kuna pesa ambazo ni posho za wanajeshi waliosimamia ulinzi tarehe 29 Oktoba hawajailipwa mpaka leo.

Kifupi, Mkuu wa Majeshi haji kutoa ushahidi kuogopa dodoso la Lissu.

Sisi wananchi tunataka afike mahakamani, kama hataki futeni Kesi haraka.
Maadam wewe ni verified member, nina sababu ya kuamini ulichosema. Wacha tuone.
 
Wale mashahidi watatu nao wasisubiri hadi walazimishwe. Waonane na mshtakiwa mapema ili wapange mikakati ya pamoja.
Bahati nzuri jana Lissu aliikumbusha mahakama kwamba leo iwalete mashahidi wake ili akae nao wajue wanaendaje hivyo ni imani yetu mida hii watakuwa wameshatinga viungo vya Posta kuhudhuria court proceedings.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 1.

Leo September 16, 2026

Mahakama imeanza.

Imepigwa high coooooourt

Majaji wameingia.

Mhe. Lissu nae ameingia kama kawaida makofi mengi yanapigwa mengi kwa ajili ya kumkaribisha Mwenyekiti Tundu Lissu.

Katuga anawatambulisha wenzake.

Jaji Ndunguru anasema tuendeleee.

Anasimama Mhe. Tundu Lissu anasema naomba kuzungumza kidogo na shahidi wangu naona amenitumia ujumbe hapa kabla hatujaendelea na nitamfuata.

Wanaenda kuzungumza Mhe. Lissu na Mhe. Heche pale kwa dakika kama tatu.

Wanaongea na kutikisa vichwa wamekubaliana wamemaliza na Mhe. Lissu anarejea kwenye kizimba chake.

Majaji wanazungumza kama dakika tano sijui wanajadili nini?

Mhe. Lissu: Shahidi kuhusu suala la Utekaji na ripoti ya SADC.

Heche: Hilo suala la Utekaji ukurasa wa 6 wa ripoti hiyo unazungumzia masuala ya Utekaji.

Katuga: Ukurasa wa 6 hakuutaja wakati wa kutoa ushahidi huo.

Mhe. Lissu: Tusipotezeane muda toa neno ukurasa wa 6.

Heche: Suala la Utekaji lipo kwenye ripoti ya SADC ukisoma utaona.

Mhe. Lissu: Ulisema maneno ya utekaji, kukinukisha kwamba sio kila mahali nilitumia hayo fafanua?

Heche: Nilimaanisha maudhui ni yaleyale kuzungumzia mfumo wa Uchaguzi. Choice of words tu ndio lilikuwa ni suala linalotofautiana.

Mhe. Lissu: Kuhusu Uchaguzi wa Tarime ukasema haukuwa huru na haki na hivyo hupaswi kuwa Mbunge na haukuwa na mamlaka hayo ya kukataa kuwa mbunge au hukuwa na huo uwezo?

Katuga: Hatukuuliza hivyo.

Mhe. Lissu: Rekodi zituongoze.

Jaji: Sikuwa na uwezo wa kukataa kuwa Mbunge

Heche: Ufafanuzi wangu ni kwamba returning officer ndio anatangaza Mbunge.

Mhe. Lissu: Mkurugenzi wa Uchaguzi akawa mgombea na sasa ni Mbunge wa Butiama na ukasema haikuwa sahihi. Fafanua?

Heche: Nilisema kwamba kanuni za CCM zinataka mwanachama wake ili agombee anapaswa kuwa na uanachama wa miaka mitano.

Kwahiyo naamini alijiunga na CCM akiwa bado ni Mkurugenzi wa Tume maana asingeweza kuruhusiwa kugombea ikiwa takwa la miaka mitano bado hajakidhi.

Mhe. Lissu: Tume ya Chande uliulizwa kuhusu wewe au Chama kuitwa. Na ukaoneshwa na mabarua mengi lakini ukasema hukuitwa. Fafanua. Usiingize mambo mapya Wakili wa Serikali atanuna.

Heche: Mimi sikupokea barua yoyote ya Mwaliko kutoka tume ya Chande na kuhusu Chama hakikupokea maana kilikuwa kimefungiwa.

Katuga: Kuhusu chama isiingie maana hakusema hivyo.

Mhe. Lissu: Tusomewe record inasemaje?

Jaji Ndunguru: Alipoitwa na tume ya Jaji Chande. Barua ilikuwa ameandikiwa Katibu Mkuu na haikuandikwa kwa Chama.

Heche: Haikuwa addressed kwa Chama.

Mhe. Lissu: Uliulizwa na maswali kuhusu Chama kwenda Bungeni na kutoa maoni kuhusu muswada wa Sheria. Kuhusu kuwaondoa wakurugenzi kusimamia uchaguzi.???

Heche: Bado watumishi wa umma ndio wanasimamia Uchaguzi na mapendekezo yetu yalikuwa ni Tume kuwa na Wafanyakazi wake kuanzia ngazi ya kitaifa hadi chini na sio watumishi wa umma.

Mhe. Lissu: Kuhusu Thabo Mbeki Foundation na Mwalimu Nyerere Foundation tofauti yake. Fafanua

Heche: Thabo Mbeki Foundation inafanya kazi nchi zaidi ya moja tofauti na Mwalimu Nyerere Foundation ambayo inafanyakazi Tanzania tu ndo maana nilisema yenyewe ni International.

Part 430 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Leo mshtakiwa anamalizia tu cross examination kwa shahidi wake wa nne (John Wegesa Heche). Baada ya hapo ndiyo wanakuja wale mashahidi wengine muhimu watatu waliobakia.
Kuweka sawa ni Re-examination mkuu maana cross-examination iliisha jana.

Ni matumaini yetu bila shaka CDF, IGP pamoja na DCI watamtetea ipasavyo mshitakiwa vinginevyo wakigeuka kuwa hostile witnesses basi wajiandae kuwa cross examined na itakuwa mbaya zaidi kwao bora wawe upande wa mshitakiwa ili kufunika madudu ambayo yanaweza kuanikwa hadharani.
 
Back
Top Bottom