Penzi ni kikohozi, tunaandika kama mzaha lakini madhara yake ni makubwa sana.
Hii inawahusu zaidi wavulana kwa sababu wao ndio wenye maamuzi ya kuoa.
Ewe kijana sikiliza kwa makini ukimpata mwenza wa kuishi na kujenga naye familia hakikisha ni wa imani yako na kama ni imani tofauti basi hakuna mjadala cha kwanza mwanamke ndio abadili imani aje kwako au wewe ubadili imani umfuate mwanamke.
Unaweza usinielewe kwa upofu wa mapenzi utasema mtafunga ndoa bomani, bomu unalolitengeneza ni zaidi ya atomic.
Wazungu ni watu waliostaarabika siku nyingi hizi dini kwao walishagunduwa ni utapeli tu hawana shida, lakini kwa Africa ambako bado tupo kwenye mchakato wa kutoka unyani ili kuwa binadamu kamili dini zina nafasi kubwa sana.
Ukitaka kujuwa ulevi wa dini angalia Tanzania na ulaya, huwezi kukuta ulaya upuuzi wa viongozi wa dini kupewa kipaumbele kwenye shughuri za serikali.
Mwenye masikio na asikie, ukiona huwezi kwenda kwenye imani ya mwenza wako vunja hayo mahusiano mapema utaumia lakini utapowa maisha yataendelea na utapata mwingine.