Leo ni leo asemaye kesho muongo. Polepole kuongea na Watanzania saa mbili kamili usiku! Usikose!

Leo ni leo asemaye kesho muongo. Polepole kuongea na Watanzania saa mbili kamili usiku! Usikose!

Niwe mkweli, kuingia mitini kwa Polepole Leo bila taarifa yoyote kazingua Sana. Alitakiwa atoe taarifa ya kuhairisha Mkutano wake. Leo watu wengi wamefurika kumsuburia Polepole halafu hajatokezea.

Kazingua big time hata kama ni kwa bahati mbaya.

Tusubiri kujua nini kimemsibu, watu hukolimbwa, futungo si watu wazuri.

Awe salama Polepole akuje kutufahamisha kulikoni.

Angalizo:

Kwa waliosoma Cuba, wahuni si wa kuwapa notice ya masaa 24 kabla ya tukio. Huko mi kuwa dogosha mno futungo katikati ya mapambano na kabla ya kuvuka mto!
 
Ndio maana nasema you guys mnamchukulia polepole ni just a loser guy …..he knows all the next move za Vijana wa lumumba intelligence ya kihuni…. He planned his gestures way back

Hayupo TZ YOU SHOULD clearly know that na hawawezi kumtract…. Hatuna smart people kwenye intelligence zetu ikiwa Kigogo tu alikuwa hapo Osterbay na hawakuweza kumjua hadi sasa waje kumjua polepole

Maisha ya sasa hata kama
Ni raia wa kawaida usiishi kizembe
Kuna entities nyingi private siku hizi zinatoa training za ki intelligence and military connation
Kuna post fulani ya Evalist Chahali ya wiki iliyopita alielezea kwa ufupi kuletwa Waisrael ili kudukua account za watu,
Hamphrey Polepole achukue hatua zote,
Hivi viongozi wa Hezbollah na Yule kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah huwa anatoa hutuba live kupitia vyombo vya habari?
 
Hivi wanaweza kupita nae wakati ni ccm mwenzao,aisee kila mtu atafikiwa kwa muda wake,mm nilijua cdm tu ndio watakao fikiwa milele,mungu mkubwa
 
Cha kushangaza zaidi wanaotumwa kufanya Doria Mitandaoni na kukesha wakizunguka Mwananyamala ni Watoto wa Masikini, ambao Wazazi wao hawakuhusika na Ufisadi wala Mauaji.(Polepole anaishi Mwananyamala Komakoma baada ya kutoka Morogoro)

Hofu imetanda kwa Watawala waliofanya Uhalifu, Maana wanaend kuanikwa hadharani.

Vikao vya Uteuzi wa Wagombea Ubunge wa CCM Katika uchaguzi ambao hautakuwepo vimezimwa na kishindo cha Polepole, huku Mkata Swichi akipigwa na Butwaa.
Kazi unayo bwana mdogo. Na lazima itakuwa inakulipa sn mana si kwa umbea ulionao
 
Copy & Paste from Setfree

Wapendwa, leo kuna tukio la kustaajabisha lililotokea katika nchi fulani. Tukio hilo linafanana sana na kile ambacho Biblia inatufundisha kuhusu kuja kwa Bwana Yesu Kristo. Katika nchi hiyo, kuna mwanasiasa mwenye utata, anayeitwa Lopelope. Alitangaza kwamba leo saa mbili atalihutubia taifa hilo "live." Watu walijiandaa kumsikiliza tangu asubuhi, wakakaa tayari mbele ya simu zao na kompyuta, wakitarajia kumuona "online" saa mbili kamili. Lakini kilichotokea ni tofauti kabisa – saa mbili ikapita, saa tatu ikapita, bado hajatokea. Hatimaye mitandao iliyokuwa imepanga kurusha "live" hotuba yake ikakata matangazo. Watu wakaingiwa na hasira na kuanza kulalamika: “Kwanini Lopelope hajatokea?”

Ndugu zangu, tukio hilo ni mfano halisi wa fundisho la Bwana Yesu. Biblia inasema:
“Kesheni basi kwa maana hamjui siku wala saa atakapokuja Mwana wa Adamu.” (Mathayo 25:13)
“Basi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.” (Luka 12:40)

Yesu hajasema ni lini atarudi. Watu wengi wanataka kujua tarehe na saa, lakini hakuna anayeijua isipokuwa Baba wa Mbinguni (Mathayo 24:36). Kazi yetu siyo kujua tarehe, bali ni kukesha na kujiandaa kila wakati.

Fikiria waliokuwa wanamngojea Lopelope: walikuwa macho, walijiandaa mapema, lakini wakachoka, wakavunjika moyo kwa sababu hakutokea kwa muda walioutarajia. Vivyo hivyo, watu wengi leo wamepunguza bidii ya kumngojea Yesu kwa sababu wanaona kana kwamba amekawia.

Yesu atakuja ghafla, kwa siku na saa wasiyoitarajia watu, kisha kufumba na kufumbua atawanyakua wote waliotubu dhambi zao na kumwamini, na kuwapeleka mbinguni.

Kwa mantiki hiyo, Yesu anaweza kuja hata leo usiku. Hivyo tujiweke tayari kama wale wanawali wenye busara (Mathayo 25). Itakuwa kilio na kusaga meno kwa watu wasiokesha, maana wataachwa duniani; na dunia yote itapatwa na dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu.


Copy & Paste from Setfree
 
Back
Top Bottom