Leo nimemwona Mwandambo Daah! Mpaka nimelia. Nimesikitika Sana

Leo nimemwona Mwandambo Daah! Mpaka nimelia. Nimesikitika Sana

Enough boys. Wewe ndo unajiharibia zaidi unapomjibu huyo. Just ignore him, wengine hatujakuzoea hivyo Taikon, kama mtu ameona hajaridhika na andiko lako anaweza pita kimya, sijaona sababu ya kukushambulia kwa maneno ya kipuuzi.

Watu kama hawa pia ni muhimu kuwajibu ili wapone.
MTU aliyetoka background ya heshima na kueleweka hawezi kutoa matusi ya namna hiyo.

Nimemuacha baada ya kugundua Hana tusi jingine zaidi ya uchafu aliofundishwa wa Aina moja.
Kama angekuwa ni mtu wa matusi asinge base na hilohilo tusi moja.

Kingine, Sisi watibeli hatuna rangi moja. Hatuzoeleki.

Ingawaje najua unazungumzia suala la heshima😀
 
Mpo salama Wakuu!

Leo acheni tuu! Msinione nimekuja nimenyong'onyea. Mambo niliyokutana nayo yanaumiza Sana.

Mara ya mwisho kulia machozi ni kwenye Msiba wa Bibi Yangu Kipenzi. Mwaka Juzi yaani miaka miwili iliyopita.

Mimi ni wale wanaume tunaoamini Mwanaume hapaswi kulia. Na ikitokea Amelia basi ujue ni tukio kubwa sana. Ameumia Sana.

Lakini Leo bila kuamini, bila kujua, nikashindwa kujizuia. Nilijikuta Nalia Mimi.

Kwanza nimemkuta mwanaume mmoja akiwa anacheza pekeake barabarani, huku anajichetua. Anajichetua, anabenjuka kisha anajichekesha akiona cheko haliji anajikenuisha Meno nje mashavu yametuna.

Huyu ni nani?
Watu wanamshangaa wengine wakimtupia maneno ya dhihaka lakini yeye mwenyewe hajali machoni lakini rohoni anajisikia vibaya.

Punde akili Yangu ikastaki, NI yeye! Ndio nilimkumbuka. Ni eye mwenyewe.
Huyu si Mwandambo huyu?

Kwanza moyo wangu ulishikwa ganzi, mdomo ulibaki wazi, sikuamini! Sikuwa na sababu ya kuamini.

Nachoka Mimi nachoka.
Nachoka Mimi nachoka.
Dede dede! Dede dede

Mamaa! Moyoni nikasema Mungu wangu hii ni nini tena.
Nikashangaa machozi yanatoka. Hee! Mtibeli unafanya nini?
Huwezi amini ati nilijikuta Nalia kwa kwikwi.

Sasa nikaanza kujitetea nafsini, akili Yangu moja ikiiambia akili nyingine kwa nini nalia kwa kwikwi.

Unajua nini? Huyu Mzee alibeba Imani kwa waliomuona huko mtandaoni. Kuibuka kwake kulikuwa nyongeza muhimu katika njia ya matumaini ya ukombozi.

Vijana, wanawake, watoto, na wazee walianza kumpa mioyo yao.
Ni wanaume wachache wa umri wake waliojitoa kimasomaso kujitokeza kuwapa ari wanaharakati.

Akili nyingine ikaniambia, sasa nini kimetokea? Mbona anacheza hapa kama mwehu? Unahakika ni yeye au umemfananisha?

Usiseme hivyo Mosley! (Mara nyingi Mtibeli anapokuwa katika mabishano ya kinafsi akili moja Ile akili ya kikafiri anaitambua kwa jina Mosley)
Huku Ile akili yenye mambo chanya nikiita Teruso. Kumaanisha ndani ya nafsi Yangu, mtibeli amegawanyika kwa ndani kwa Jina la Mosley na Teruso.

Tuendelee;
Nikamwambia Mosley, nyamaza! Wewe hujui kitu. Mwaka Jana nilienda Moshi kwa Mama, nilishangaa mama Yangu akinukuu kauli ya Mwandambo, nachoka miye nachoka, nachoma miye nachoka.

Pia nilienda Morogoro kwa Mama Mkubwa, nikakuta hali iko hivyohivyo.
Baada ya uchaguzi nilikuwa Kahama nako nikakuta kauli ya mwandambo.
Wewe utaniambia Mosley huoni kinachoniliza?

Mosley akatulia, kisha akanisogelea zaidi humohumo Akilini akaniambia, wewe ni mpumbavu! Mjinga! Mjinga wa mwisho kabisa. Bora ungekuwa hata mjinga wa Kwanza.

Nikamwambia, watu walimwamini Sana. Walimpenda.
Hujui tuu! Huwezi kunielewa.

Kisha mawazo Yangu yakahamia machoni tena, nikamwona Mwandambo akijishika tumbo alafu ananyanyua mguu mmoja alafu anaanza kukatika,
Nyanyanya! Nyakunyaku nyaku!
Kisha anajishika tumbo lake huku akiendelea kukatika huku sura yake akiikunja na kukenua Hali inayofanya aonekane kama amekula Limao hivi au pengine ndimu za handeni.

Muone! Tazama Mosley! Unamuona?
Mosley akanijibu, kwani anawatoto au familia?

Mosley linakuwaga na maswali katili Sana. Hali inayonifanya nilie nilie! Kwikwi inakomesho.

Unajua nini?
Najua hujui
Ila katika vitu nakuombea kwa Mungu ndugu msomaji usije ukakutana na Mwandambo lazima chozi likutoke. Utasononeka Sana.

Sasa jamaa mmoja akaniambia, yupo huko mitandaoni huko Facebook. Nikamwambia na huko anafanya hivi?
Nikiwa napenga kamasi jepesi la maombolezo, hakutaka kunijibu alichofanya alinisogezea usoni simu yake na hapo ndipo macho Yangu yalishindwa sasa kukataa na kuzuia machozi tena.

Nililia! Nililia mimi! Sijui kama nitalia kama nilivyolia. Daah!

Niliondoka pale bila kujua.
Nikatembea nisijue nilikuwa naburuzika, napaa au natambaa, nilijikuta nipo mtaa wa tatu napigiwa kelele wewe mjinga wewe utagongwa wewe. Unataka utuchafulia Barabara hapa.

Daah! Nachoka mimi.
Nimemaliza ila machozi kwa muda huu sina. Yamekauka. Na kwa jinsi nilivyolia kule kwa mwandambo mpaka machozi yajikusanye hapa itachukua miaka.

Nduki!

Mtibeli katika moja na Mbili
Mjinga mkubwa umenipotezea muda wangu nakazana kusoma kumbe ni mahandasi tyuu
 
Hoja ni kwamba umebahatika kumuona mwandambo hizo nye nye nye ni abracadabra.
 
Jambo likiwa linarudiwa rudiwa ujue tatizo ni wewe, jifunze kupunguza mambo yasiyo ya msingi kwenye bandiko lako, kama kuna mtu unajifunza kutoka kwake uandishi jaribu kuongeza mentors.

Huwaga sichukui ushauri kwa mtu yeyote hata wangekuwa wengi. Tena watu hao hawana ujuzi wowote wa kile ninachokifanya.

Hao washauri wanachotakiwa kufanya kama hawataki kusoma kazi zangu waache. Siwezi shauriwa udereva na MTU ambaye hajawahi kuendesha hata baiskeli
 
Back
Top Bottom