Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

Tatizo hii kesi haiusiani na icho unachotaka kifafanuliwe..
Very nice. Nakubaliana nawe.

Lakini kwa manufaa ya umma, ni muhimu kitolewe maelezo ili kufunga mjadala.

Haitakiwi kuwa na kiongozi anayetuhumiwa muda wote halafu yeye yupo kimya tu kama bubu.

Kiongozi yeyote anatakiwa kuwajibika kwa wale anaowaongoza, ikiwemo kuonesha usafi wake, sio kunyamaza anasubiri kutetewa na chawa wake.

Hii tabia ndio inazidi kuleta mashaka kumhusu huyo kiongozi.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI.

SEHEMU YA 17.

MAJAJI WAMEREJEA

Mawakili wa Serikali wapo.
Mshtakiwa yupo.
Shahidi alitoka kidogo, lakini alikuwa kizimbani.

Jaji Ndunguru: Tuendelee upande wa mashitaka.

Wakili Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, Mahakama Kuu, kolamu ipo kama ilivyokuwa awali. Tupo tayari kuendelea.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa.

Jaji Ndunguru: Shahidi.

Shahidi: Shahidi amerejea.

Lissu: Nipo tayari kuendelea.

MASWALI YA NASSORO KATUGA

Nassoro Katuga: Shahidi, naomba tuendelee. Tunaendelea kuona ushahidi wako kama wa kuaminiwa au la.

Ulisema Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA hulipwa?

Heche: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ule Prado umenunua kwa Tsh milioni ngapi?

Heche: Nimenunua kwa milioni 160.

Nassoro Katuga: Ile Double Cabin?

Heche: Milioni 80.

Nassoro Katuga: Crown ulitutajia Tsh ngapi?

Heche: Sikumbuki, ni tangu nikiwa Mbunge.

Nassoro Katuga: Ile Mitsubishi Canter ni Tsh ngapi?

Heche: Milioni 60.

Nassoro Katuga: Uliinunua ukiwa Makamu Mwenyekiti?

Heche: Nikiwa Makamu.

Nassoro Katuga: Tangu umekuwa Mwenyekiti umesema hulipwi chochote.

Heche: Silipwi chochote, lakini nina kazi zangu.

Nassoro Katuga: Shahidi, kwanza pole kwa kufiwa na mdogo wako. Lakini lazima tuulize; pamoja na kifo siyo jambo zuri kwa mwanadamu. Hebu waeleze Waheshimiwa Majaji, mdogo wako umesema anaitwa nani?

Heche: Soma, si uliandika.

Nassoro Katuga: Sema mdogo wako anaitwa nani.

Heche: Suguta.

Nassoro Katuga: Wakati mdogo wako anateswa ulikuwepo?

Heche: Sikuwapo.

Nassoro Katuga: Wakati anachomwa na singe ulikuwepo?

Heche: Alisema RPC.

Nassoro Katuga: Jibu swali, ulikuwepo au hukuwepo?

Heche: Wapi?

Nassoro Katuga: Wewe umesema mdogo wako alichomwa na singe. Je, wakati anachomwa na singe ulikuwepo?

Heche: Alisema RPC.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo, wakati anachomwa singe na polisi, ni ushahidi wa RPC?

Heche: Ni sahihi alisema yeye.

Nassoro Katuga: Katika harakati zako, umewaambia Waheshimiwa Majaji kuwa alichomwa na singe sehemu gani—mdomoni, kifuani au shingoni?

Heche: Sikueleza.

Nassoro Katuga: Ni kweli ulisema polisi walitaka kumtupa?

Heche: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Ulikuwepo eneo walilotaka kumtupa?

Heche: RPC alieleza.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulifanikiwa kuhojiana na huyo anayedaiwa kumuua mdogo wako.

Heche: Nilishawahi kumuuliza.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 

TOKA MAKTABA :
Baada ya mahakama ya ICC kukataa kusikiliza kesi nchi Kenya au Arusha Tanzania na kusisitiza washtakiwa kufika ICC The Hague, kutokana na kuwa ICC The Hague imeshindwa kushawishika na kesi hiyo nzito kuendeshwa nchini Kenya au Tanzania.

Je kupitia kesi hii ya uhaini ya Tundu Lissu kina Hamza S. Johari mwanasheria mkuu anaweza kumnusuru Samia Hassan na wenzie wasiende wala kuitwa ICC The Hague kama mahakama ilivyoamua katika kesi hii ya Uhaini ya Tundu Lissu ?


2013
Uhuru Kenyatta, Ruto and Sang case: "Ask the Court" programme, 18 June 2013, who else Jean-Pierre Bemba ..


View: https://m.youtube.com/watch?v=ILKF61cvk3YIn this edition of the "Ask the Court" programme: Didier Preira, Deputy Registrar of the International Criminal Court (ICC), answers questions concerning the decision of ICC Trial Chamber V(A), on 18 June 2013, to conditionally grant the request of William Samoei Ruto to be excused from being physically present continuously throughout the trial, scheduled to start on 10 September 2013

FAST FORWARD SEPTEMBER 2026
 

Wakati ule
Wapinzani walikuwa ndio kina William Rutto na
Uhuru Kenyata
Ndio walitakiwa uko ICC Sababu za Uchochezi wao ulipelekea VIFO vya Wakenya 1000+

Kipindi kile cha Machafuko
RAIS wa KENYA alikuwa
MWAI KIBAKI 👈

Tanzania Wachochezi ndio
uyu mh Lissu yupo Lupango leo
Ndio katangaza hadharani kukinukisha kuzuiya
Uchaguzi Nk ✅️

Tz WAPUMBAVU wanataka kafanya propaganda kuwausisha na VIFO watu wasiousika

Na kuwaacha Wachochezi mbele ya Macho yao CHADEMA WAONGO KWANZIA VIONGOZI MPAKA WAFUASI WAO 😡😡😡
 
Mmemuhoji kwenye vikao vya chama akakataa kutoa ufafanuzi?
Mimi sio kiongozi wa Chadema, i think tunafanana tu, wote tunaishia kelele zetu humu humu.

Nachotaka atoe taarifa public ni kwasababu, Chadema kinaitwa chana cha watanzania.

Hata michango wanayopokea inatoka kwao, sasa kuna ubaya gani kiongozi wao akijitokeza mbele yao akajibu yale anayotuhumiwa nayo?

Tena kama ikitokea akajibu wazi kwa public, naamini hapa ndio atakuwa amekata mzizi wa fitna, watu tayari tutakuwa na majibu yetu, sio rahisi kuja kuvurugwa tena mbele ya safari.

Lakini madhara ya kujibia kwenye vikao, ikitokea upande mmoja haujaridhika, basi naamini hizi kelele zitaibuka tena mbele ya safari, hivyo mwaka wote huu tuwe tunaishi kwa malalamiko yao tu.
 
Huwa inatokoka ripoti kutoka BOT...au Benki husika kwamba Kuna miamala hatuna Imani nayo...

Polisi kitengo Cha fedha haramu ndio wahusika wakuu katika kuwa na hizo documents....

Sasa wakili wa Serikali anapataje hizo documents?...Maana Polisi haruhusiwi kuzigawa ...ni confidential
 

Tunao Wabunge wengi tu kwasasa Masikini wa kutupwa
Kuwa Mbunge miaka ya 2015 huwezi kudai hawezi kuwa Masikini leo ❗️

Lkn zaidi Nassoro Katuga najua Umemwelewa vizuri kataka kutuonesha namna HECHE ni muwongo ❗️
yupo apo
sio kumiliki Magari mangapi ✍️
 
Unampangia muulizaji maswali aulize maswali yanayokufurahisha wewe?

Kwenye cross-examination unauliza namna yeyote unavyotaka ilimradi umwondoe shahidi kwenye mstari ili kupima ukweli wa kile alichokisema kama kina ukweli ama laa..
 
Unayajua maisha wanayoishi waliowahi kuwa Wabunge wa Chadema Mh. Ainess Kiwia (Ilemela) na Machemlo (Ukerewe)? Kawauliza kama wana hata baiskeli! Ahahahahaha!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…