Leo tarehe 14 September, Shahidi John Heche ameshafika tayari mahakamani

WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 19.

KUHOJIWA NA NASSORO KATUGA

Nassoro Katuga: Ulijua au hukujua kuwa kilichofanya wamchukue Bwana Tall ni kwa sababu ni mwanachama wa CHADEMA?

Heche: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Unasema aliyemchukua humjui?

Heche: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Baadaye ulieleza kuwa ulikamatwa hapa nje?

Heche: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Ukashtakiwa kwa kuvuka mpaka?

Heche: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ni kweli ulienda Kenya au hukwenda?

Heche: Sikuvuka.

Nassoro Katuga: Ni kweli ulitaka kwenda au hukutaka?

Heche: Nilitaka kwenda.

Nassoro Katuga: Ulieleza katika ushahidi wako kwa nini ulizuiliwa?

Heche: Sikueleza.

Nassoro Katuga: Ni kweli ulisema ulipelekwa hadi Dodoma, ukalazwa Mtumba peke yako?

Heche: Sahihi.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ulitaka uwekwe selo na nani?

Heche: Sikutaka kuwekwa na mtu.

Nassoro Katuga: Unaogopa kulala peke yako na wewe mwanaume?

Heche: Hapana.

Nassoro Katuga: Hivi shahidi, katika kukamatwa kwako huko unapotuambia, uliwahi kuchukuliwa passport yako?

Heche: Ilichukuliwa.

Nassoro Katuga: Ilichukuliwa lini?

Heche: Nafikiri tarehe 18 Oktoba 2025.

Nassoro Katuga: Ilirudi vipi kwako?

Heche: Chama kiliandika barua kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, nikarudishiwa kwa mtu anayeitwa Kamishna wa Mipaka Jirani.

Nassoro Katuga: Unajua kuwa Ofisi ya DPP kupitia National Service Act ina jukumu la kuratibu kupeleka kesi za jinai?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Ni kosa gani kukuta Mawakili wa Serikali kituo cha polisi?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Katika ushahidi wako kuna sehemu yoyote ukisema hawa akina Katuga walideal na mimi?

Heche: Sikujua.

Nassoro Katuga: Unajua au hujui kuwa kesi ya jinai haina limit kwamba baada ya miaka mitano unaweza kushtakiwa?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Uliulizwa kuhusu kesi ya Oktoba 29, hukuwahi kushtakiwa. Na kuhusu hiyo ya ugaidi ukasema hujawahi kushtakiwa, ni kutisha-tisha tu?

Heche: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Unajua ama hujui kuwa Mawakili uliowaona pale walikuwa wanacoordinate kesi za tarehe 29 Oktoba?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Unajua au hujui kama washtakiwa tuliowahoji pale walikutaja wewe kuwatuma Oktoba 29?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Unajua ama hujui ushahidi uliokusanywa kwenye hayo mafaili unaeleza mlikaa vikao na jinsi mlivyopanga kuratibu matukio ya tarehe 29 Oktoba?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Ni ushahidi wako kwamba ulipohojiwa kuhusu ugaidi ulikataa?

Heche: Nilikataa, maana sikutoa maelezo

Nassoro Katuga: Ulitoa maelezo Polisi au ulikataa?

Heche: Nilikataa ndiyo.

Nassoro Katuga: Sasa shahidi, unasema ulisikiliza hotuba ya Jaji Chande. Je, kwenye hotuba hiyo ulisikia kauli ya kuwa Oktoba 29 ni matukio yaliyopangwa?

Heche: Nilisikia.

Nassoro Katuga: Je, ushahidi mbili za wakati wa coordination kupitia ushahidi wa watuhumiwa kuwa wewe ulihusika katika kupanga na kuratibu, na hotuba ya Chande kwamba matukio yalipangwa, vinafanana au havifanani?

Heche: Kwa hiyo mimi ni mshitakiwa?

Lissu: Jibu swali kaka.

Nassoro Katuga: Je, ushahidi mbili za wakati wa coordination kupitia ushahidi wa watuhumiwa kuwa wewe ulihusika katika kupanga na kuratibu, na hotuba ya Chande kwamba matukio yalipangwa, vinafanana au havifanani?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Shahidi, nilikusikia ukisema hujui au huna kumbukumbu ya viongozi wengine wa CHADEMA kama waliwahi kushtakiwa?

Heche: Ndiyo nilisema.

Nassoro Katuga: Unamfahamu Zitto Zuber Kabwe?

Heche: Namfahamu.

Nassoro Katuga: Unajua kuwa Zitto Zuber Kabwe alishtakiwa kwa kuchapisha taarifa za mauaji ya Kigoma? Alishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam inayoketi Kisutu na hakukutwa na hatia.

Heche: Sijui. Nilikuwa naongelea viongozi wa CCM.

Nassoro Katuga: Unamfahamu Daniel Yona?

Heche: Simjui.

Nassoro Katuga: Unamfahamu Basil Pesa Mbili Mramba?

Heche: Simfahamu.

Nassoro Katuga: Na bado unajiona wewe ni shahidi?

Heche: Ndiyo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Kwahiyo hao mawakili wa Lisu nao wanaweza kwenda bank na kuchukua taarifa za kibenk za hao mashahidi aliowataja kama CDF,IGP nk?
 
Wewe una panic haraka sana.

Kama unadhani hivyo ndivyo, basi usingekuja hapa kuzungumzia habari za Heche!

Bye, ushakata moto.
Wow 😂 I see what you are trying to do here!

Mimi niliyepaniki sijakushambulia, wewe ambaye haujapaniki umenishambulia. Umeelewa nini?

Nenda urudi leo haujajipanga. Na huwezi kujipanga sababu unajaribu kutetea uovu. Utetezi wako lazima uwe mgumu kama wale mashahidi wa siri.
 
Unaomba kibali Mahakamani...
Na muhusika wa account anapewa taarifa...

Kibali kinatoa Sababu mahususi...

Sasa hii kesi ya Lissu, Mawakili wa Serikali walikuwa na Sababu Gani ya kuomba miamala ya Heche ?
Huoni ni siasa...hili blog za CCM ziandike Heche anapokea Hela kutoka CCM...
 
Kwahiyo hao mawakili wa Lisu nao wanaweza kwenda bank na kuchukua taarifa za kibenk za hao mashahidi aliowaja kama CDF,IGP nk?
Umekuja kujibu nilichouliza au umeleta swali juu ya swali?

Kwenye hii kesi Lisu hana mawakili
 
Mawakili wanahoji heche maswali so personal nahata hayahusiani na kesi ya uhaini ya lissu
Lisu ameuliza kuhusu uenguaji wa wagombea wa chadema kwenye chaguzi kadhaa zilizopita huko nyuma...vipi maswali hayo yana uhusiano gani na kesi yake ya uhaini?
 
Nikajipange wapi!.

Heche ni kiongozi wa public, tuhuma dhidi yake zinatolewa public, ana wajibu wa kutoa majibu yake kwa public.

Hapa sio suala la kutetea uovu au kujipanga, ni suala simple la kuonesha uwajibikaji wa kiongozi kwa wale anaowaongoza.

Sijui kwanini mnateseka sana kwa jambo dogo hivi!.

NB.
Don't say nimekushambulia, sipo vitani hapa.
 
Umekuja kujibu nilichouliza au umeleta swali juu ya swali?

Kwenye hii kesi Lisu hana mawakili
Anao na zaidi ya mara moja ameiambia mahakama anaomba ajadiliane na mawakili wake. Atakosaje mawakili wakati yeye yuko magereza na wao ndio wanaweza kumpatia baadhi ya taarifa anazozitaka kwa ajili ya mwenendo wa kesi? Unachanganya kaumua kujitetea mwenyewe, na kuwa na mawakili. Fanyia kwanza kazi ukweli huo, kisha uje ujadili hayo mengine boss.
 

Swali zuri sana tunduizi, tutegemee wakati wa cross examination atakayofanya Tundu Lissu kwa John Heche suala hili nyeti linalogusa umma mpana wenye akaunti benki litaibuka
 
Heche angesema nawafahamu halfu aseme walishtakiwa kwa ubadhirifu au aseme walishitakiwa kwa mambo ambayo hayahusiani na mapambamo ya siasa.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN HECHE MAHAKAMANI.

KUHOJIWA NA NASSORO KATUGA

Nassoro Katuga: Shahidi, uliwaambia Waheshimiwa Majaji kwamba Mbunge akipata madhara ya afya atatibiwa nchini kwa bima yake, na akipata referral Bunge ndiyo watamtibia?

Heche: Sikusema. Inategemea na hali yake.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, hapa nchini kwetu ukitaka kwenda kutibiwa nje ni kweli lazima uwe na referral?

Heche: Wapo watu binafsi wanaenda nje bila kupata referral.

Nassoro Katuga: Kwa mtu ambaye anatibiwa na Serikali, anaweza kwenda nje kutibiwa kwa kujiamulia au lazima atimize taratibu za hospitali zetu?

Heche: Napitia katika hospitali zetu.

Nassoro Katuga: Ni sahihi kwamba mlipaji wa Serikali ni lazima ajiridhishe na taratibu kabla hajalipa fedha za matibabu ya nje?

Heche: Upo sahihi kiasi na haupo sahihi kiasi.

Nassoro Katuga: Ili mtu akatibiwe nje, nini utaratibu wake? Ni lazima pawe na referral au siyo lazima?

Heche: Kuna upendeleo muda mwingine.

Nassoro Katuga: Unajua au hujui kuwa Mwenyekiti alikuwa na referral kwenda nje?

Heche: Sijui, ila alipelekwa na ndege iliyokodiwa na chama.

Nassoro Katuga: Uliambia Mahakama hii Mheshimiwa Lissu alivuliwa ubunge akiwa nje?

Heche: Ni sahihi.

Nassoro Katuga: Unajua au hujui kitendo alichofanya Spika, kama Lissu hakuridhika, alikuwa na uwezo wa kwenda Mahakamani kupinga?

Heche: Najua.

Nassoro Katuga: Unajua ama hujui kama Lissu alipeleka shauri Mahakamani?

Heche: Sijui, ila mahakama hizi...

Nassoro Katuga: Pamoja na hii bado unasema Lissu alionewa?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Shahidi, nakumbuka vizuri ulisema kuwa ulisoma taarifa za waangalizi wa uchaguzi?

Heche: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Unajua au hujui kama Majaji wa shauri hili wanaweza kutumia ripoti kama rejea ya kesi?

Heche: Sijui.

Nassoro Katuga: Ulitaja taarifa ina kurasa ngapi?

Heche: Sikusema.

Nassoro Katuga: Kwa kumbukumbu zangu, ulisema wewe ndiyo ulitafsiri ripoti ya SADC?

Heche: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Ni kweli wewe ulisema kuwa wamesikitishwa na matukio ya utekaji kabla ya uchaguzi?

Heche: Si kweli. Sikusema hivyo kwenye SADC. Nilisema katika UN.

Nassoro Katuga: Mahakama ikikuta kuna sehemu kuwa SADC walisikitishwa, Mahakama ikuone kama muongo na iufute?

Heche: Hapana, siyo muongo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, ni kweli unasema hukusema? Tukikuta katika ushahidi wako, Mahakama ikuone ni muongo?

Jaji Ndunguru: “Walisikitishwa na utekaji kabla na baada ya uchaguzi.”

Nassoro Katuga: Umesikia maneno ya Mahakama? Hayo maneno yapo?

Heche: Nimesikia, nimesema.

Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji wachukue lipi, ulisema au hukusema?

Heche: Nimesema.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji, wewe unasema ukitafsiri kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili. Ni maneno yako kwamba SADC ilisikitishwa na utekaji kabla na baada ya uchaguzi. Tunaomba unukuu sasa kwa Kiingereza, tuone kama ulitafsiri vizuri.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sikumbuki. Labda nipate ku-refresh.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama hii ndiyo hiyo inayofanana na taarifa ya SADC unayosema.

Heche: Naona kama ya kwangu, sijui labda ndani.

Nassoro Katuga: Haya, watafutie Waheshimiwa Majaji sehemu ambayo SADC wamesema walisikitishwa na taarifa ya utekaji kabla na baada ya uchaguzi.

Heche: (Anapekua)

Mahakama ipo kimya.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…