Leo tuwaenzi na kuwakumbuka wazazi wetu waliotangulia mbele za haki

Leo tuwaenzi na kuwakumbuka wazazi wetu waliotangulia mbele za haki

R.I.P mummy and daddy
binti yenu wa pekee naendelea vizuri zaidi ya jana
haikuwa rahisi ila bado napambana
mngekuwepo ningewasimulia mengi sana yaliyojiri tangu mniache nikiwa na miaka 3
Ila ngoja nsiwachoshe...endeleeni kupumzika huko mlipo naamini kabisa mnaniombea
 
Nilimpoteza Mzee wangu nikiwa na miezi 10, kutokea hapo nimelelewa na Mama pekee.

Bahati mbaya kabla sijapata kazi naye akafariki bila kuonja hata elfu 1 yangu.

Graduation ya form six na chuo kikuu zote nimezifanya bila uwepo wao.

Kuna wakati huwa nahisi huyu Mungu anapendelea. Kwanini awachukue Wazee wangu wote asiniachie hata mmoja wakati kuna wenzangu wana wazazi wote ama hata mmoja tu.

Anyways, safari ni yetu sote but it really pains 😭😭😭

Wale wenye Wazazi msiache kuwaombea na tafadhalini jaribuni kuwajali hata kwa kidogo mlichonacho.
Mimi huwa sipendi sherehe zinazo nihusu kwa 7bu za kutokuwa na mzazi hata mmoja.
Kipindi ninaoa,niligoma kabisa kufanya sherehe kwani nilijua itakuwa chungu kwangu kuwaona wengine wana jimwaya mwaya ukumbini ilihali hakuna mazazi wangu,machozi yange jaa pipa.
 
R.I.P mummy and daddy
binti yenu wa pekee naendelea vizuri zaidi ya jana
haikuwa rahisi ila bado napambana
mngekuwepo ningewasimulia mengi sana yaliyojiri tangu mniache nikiwa na miaka 3
Ila ngoja nsiwachoshe...endeleeni kupumzika huko mlipo naamini kabisa mnaniombea
Pole bff ni maumivu makali tunapitia, mimi nikiona mada km hizi nakimbia kabisa sitaki kukumbuka hapa leo nitalia Sana’a 😔😔
 
Back
Top Bottom