Licha ya Maisha kukosa furaha kwa binadamu ; kwa nini watu bado wanapambana kuzaliana (kuongeza watu wengine)

Liulize hilo ChatGPT ikiwa hatupo hasara inakua ya nani?
 
Umeongea kitu kikubwa sana

Mimi nikiona mtu anateseka kwasababu amekosa huduma au chakula huwa inaniumiza sio.poa

Ubnafisi unatusumbua
Kiuhalisia nikiona omba omba machozi yanaitoka ila mtu akifa wala naona kaondoka kwenye matatizo.

Babu yangu ana miaka karibia 100 ,ila analazimisha tu maisha maana hata ladha ya chakula hasikii , anatumia masaa 20 kulala kila siku ..Mengine ni mda wa kula na kunywa dawa ,anajisaidia hapo hapo ila naona anateseka ni mwaka wa tano sasa.

Anatolewa nje kuanikwa kama nusu saa hivi lile jua la Asubuhi ,sioni faida kabisa ya maisha .
 
Matatizo ni asili hauwezi kuyaondoka , takwimu zinaonesha hata mabara ya ulaya , America na Asia kwamba maisha ya zamani yalikuwa bora na walizaliana vizuri ila sasa mambo ni magumu na yatazidi kuwa magumu.
 
Inaonekana jamii zote za viumbe hai zinahitaji utambuzi wa hali ya chini ili ziendelee kuwepo ila hazipo tayari kukubali kupokea utambuzi wa hali ya juu ili kuhama kwenye hili gereza.
Ni wachache sana huweza kuhimili kupokea ukweli ndani ya fahamu zao
 
Haiwezekani katu wakagoma wote....mtagoma wachache tu
Tatizo hilo , tatizo kubwa ni ubinafsi wa kupenda kuwa juu ili watoto wawe kama watumwa wako.Kuzaana ni sawa na biashara ya watumwa tu.
 
Inaonekana jamii zote za viumbe hai zinahitaji utambuzi wa hali ya chini ili ziendelee kuwepo ila hazipo tayari kukubali kupokea utambuzi wa hali ya juu ili kuhama kwenye hili gereza.
Ni wachache sana kuhimili kupokea ukweli ndani ya fahamu zao
Well said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…