Licha ya Rais kujitahidi kuchapa kazi lakini bado Wananchi hawamuelewi!

Angekuwa siyo mtu wa dhulma asingekuwa anafanya teuzi za watu wa hovyo

Asingekuwa anawakumbatia wabunge feki 19 wanaolipwa mishahara kwa kodi zetu
 
Alisema yeye na JPM kitu kimoja lakini alipoingia tuu akaanza kufyeka watu wa JPM kuanzia kule Madawa ya kulevya, Kalemani, Polepole, Bashiru, mpaka kina.mbuge. wengi hapo ndio waliposhindwa kumuelewa falsafa yake ni ipi
Tukutane 2025 maneno mengi ya nini?
 
Raisi Samia kwa muda mfupi tu amejidhihirisha kuwa ni hodari ila Tozo zinatufyeka.
Sio kazi ya Rais Samia kutafuta cheap politics,huzo tozo haziendi Burundi..

Hapa ndipo napomkubali Rais Samia kamatia hapo hapo,umchukie au umpende she is focused hata akitoka madarakani ataonesha maelfu ya miradi aliyofanya kwa mda mfupi kabisa.
 
Nasema hivi nyie wa mitandaoni ndio mnahangaika na cheap politics kama hamuamini tukutane 2025.
 
Ngojeni mumuharibie huyu Mama ili muweke mtu wenu.
Raia hawezi kuharibiwa,akiharibiwa utakayeumia ni wewe na mimi yeye hata akiacha Urais saizi atapata stahiki zake 80% ya stahiki za sitting president Kwa hiyo hana hasara yeyote๐Ÿ‘‡
 

Attachments

  • 20220817_170011.jpg
    92 KB · Views: 2
Angekuwa siyo mtu wa dhulma asingekuwa anafanya teuzi za watu wa hovyo

Asingekuwa anawakumbatia wabunge feki 19 wanaolipwa mishahara kwa kodi zetu
Kasome tena Katiba pengine itakuongezea hekima. Uteuzi ni haki yake kadri ya anavyoona mtu atamfaa. Unayemuona wewe hafai siyo lazima na yeye amuone hafai.

Wabunge Feki 19 wa CDM ni suala Kiko Mahakamani. Kwa nini unataka Rais aingilie hii mihimili miwili? Huo ndiyo UDIKTETA ambao tuliukataa kwa mtangulizi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ