Linasubiriwa tukio lolote litokee nchini Iran ili liunganishwe na shambulizi la Israel

Linasubiriwa tukio lolote litokee nchini Iran ili liunganishwe na shambulizi la Israel

Umeandika kishabiki sana, yaani Iran iwe na uwezo wa kuipiga Israel? Ni Marekani au UK ndo walimuua Ismael Haniyeh ndani ya Iran? Ni Marekani ndo waliua viongozi wote wa Hezbollah?
Acha kujidanganya wewe.
Kwani hakuipiga?
Au wewe ndio unaongea kishabiki sasa
 
Ikiwa hataki ushirikiano kwanini anawapiga mkwara majirani kuipa nafasi Israel wakati wa kumtwanga? Kwani kuomba na kutisha kutotoa ardhi na anga sio kulazimisha ushirikiano?
Avatar uliyoweka haiendani na udogo wa akili yako. Ni afadhali ungeibadilisha ili uweke ya Netanyahu ambae mnalingana udogo wa akili, hiyo iliyopo itoe kwa heshima ya uliemuweka.

Hivi umesoma vizuri ulichoandika? Eti kwanini anawapiga mkwara majirani zake kuipa nafasi Israel wakati wa kumtwanga? Kwani mwenye nguvu hawezi kumtwanga mtu bila kuomba nafasi kwa mtu? Mbona Iran huwa inavurumisha makombora kutoka kwake hadi Israel bila kupewa nafasi na nchi yoyote na bado yanafika yalipolengwa? Na tena wakati huo huwa inafanyika juhudi kubwa za kuzuiwa na majirani hao wakishirikiana na Marekani, Uk, Ujerumani, Saudia, Jordan nk lakini bado mzigo unapenya na kwenda kuwaangamiza mashoga.

Kama Netanyahu ana ubavu huo kwanini na yeye asifanye kama mwenzake avurumishe tu kuanzia Israel yaende moja kwa moja hadi Iran badala ya kujificha katika kichaka cha kupewa sehemu apige?
BTW vita kukurupuka kama kurusha maanda maandazi kwenye ndoo ya plastic na mabeseni. Vita ni mipango utekelezaji ni kitu kidogo sana. Subiri muda ufike.

Wataimba
Free Iran.
Mbona kwa wanyonge Hamas walikurupuka? Ulichoandika ni upuuzi wa kujaribu kuwatetea hao wajinga. Uwezo wa kuipiga Iran hawana, na hawatokuwa nao milele hata waje kundi zima. Wao kila siku watakuwa wanapigiwa kwao tu mpaka watapoomba poo.
Sasa hivi wanaimba Israel inashambulia wanawake na watoto Gaza. Kwani Octoba 7, 2023 Hamas walishambulia, kuua na kuteka wanaume pekee?
Wewe kweli galasa. Yani unafananisha vita ya kikundi cha vijana wasiozidi elf 20 ambao wanatumia migobore na rocket wanazounda na petrol dhidi ya nchi yenye wanajeshi zaidi ya million plus na wengine wa akiba huku wakipokea maelfu ya silaha kutoka Marekani, UK, Ufaransa, Ujerumani, Canada nk ili kupambana na kakikundi hako alafu wewe unakuja kuwasifu kweli?

Kisheria kwa vile Hamas sio jeshi la kitaifa basi walitakiwa wadhibitiwe na polisi tu wa kawaida ambao wapo sawa na idadi yao. Lakini pia kwa vile Hamas hawana silaha za maana, basi ilitakiwa polisi hao wa Israel wawe na silaha za kawaida tu kulingana zile walizonazo Hamas ili kuwadhibiti.

Lakini kwa vile Israel haina mbinu mbadala, ndio maana inatumia jeshi zima la taifa, midege ya kijeshi, mivifaru, mimeli ya kivita kupambana na kikundi kidogo kisichomiliki hata kifaru. Yani ni sawa na serikali itumie jeshi na silaha zote za kijeshi kupambana na panya road ambao wanatumia mapanga, halaf wewe uje ujisifu eti tuna jeshi bora kwa vile limewapiga panya road na wake zao na watoto wao 😂😂😂😂
Dhambi ya ubaguzi na udini ni kitu kibaya sana. Kujiona Mwarabu, Myahudi, mkristo au muislam ni bora kuliko wengine ni upumbavu uliopitiliza
Wewe ndio mbaguzi namba moja, kwa sababu ulichoandika hapa hakiendani na uzi wangu. Au kuna sehem uzi huu umembagua mtu kwa sababu ya dini yake, rangi yake, kabila lake au jinsia yake?

Kama ipo naomba unioneshe, na kama haipo basi wewe ndio mbaguzi na umekimbilia kuandika comment yako kwa sababu za kibaguzi.
 
Iran inajiamini sana, ndomaana haina muda wa kushirikiana na nchi nyingine kuitwanga Israel. Mwenye nguvu huwa hashirikiani na mtu yoyote kumchapa mnyonge.

Lakini mnyonge ni kawaida kushirikiana na watu wengine kumchangia mwenye nguvu.
Basi usilalamike, makamanda wanauliwa
 
Niaje waungwana,

Waungwana najua wengi humu mnashauku kubwa sana ya kutaka kujua ni kwanini Israel mpaka leo tar 10/10 haijaishambulia Iran, licha ya kusema na kuapa kuwa itaishambulia na kuiangamiza Iran from day one ya shambulizi lile la pili la Iran nchini Israel ambalo lililenga shabaha iliyokusudiwa na washambuliaji (Iran), kwa kulenga tu kambi za jeshi na ofisi za mosad (sio nyumba za raia) hata kama wanajua kuwa kina Netanyahu na genge lake wana utaratibu ule ule wa kujificha katika nyumba za watu wa kawaida ili kukwepa angamizo ambalo linaweza kusababishwa na shambulizi lolote la Iran (kivita hilo linafahamika).

Sasa kinyume na matarajio ya wengi kuhusu kauli zilizotolewa na kina Netanyahu, mpaka leo hii hakuna kilichofanyika. Sio kwamba Israel haitaki kuishambulia Iran ili angalau kulipiza kisasi cha shambulio lile, bali kwanza ili wakamilishe hilo ni lazima wapate backup kubwa kutoka Marekani, UK, EU na baadhi ya nchi za NATO kama vile Canada nk. Bila nchi hizo kuwa nyuma ya Israel kimipango, silaha na fedha kiukweli Israel haiwezi kufanya chochote kwa Iran NEVER, NEVER and NEVER again. Ndiomaana mara usikie Netanyahu kaongea na Biden kwenye sim, mara usikie Biden kamwambia asishambulie vinu vya nyuklia na visima vya mafuta, mara sijui mkuu wa jeshi la Marekani kaenda Israel kukutana na mkuu wa jeshi la Israel nk. Huku kote ni katika kuhaha, kuhenya henya na kuhangaika, maana wanajua fika kwamba Israel yenyewe haiwezi kujibizana na Iran kijeshi, hivyo ni lazima wakae chini wajadili madhara yatakayotokea endapo Israel itapewa tafu na mabeberu wake kuishambulia Iran alaf Iran ijibu kwa nguvu hali itakuaje!!

Iran ikitaka kufanya shambulizi huwa haihitaji kwenda kuomba msaada au ruhusa yoyote. Wao wanatwanga tu halaf wanasubiri mpumbavu ajibu wamuoneshe.

Lengo la Iran sio kushambulia raia, bali jeshi na mifumo mingine ya serikali. Ila ikitokea Israel ikashambulia makazi ya raia wa Iran kama afanyavyo huko Lebanon na Gaza, basi bila shaka na yeye hatokuwa na njia nyingine zaidi ya kulipiza kisasi ili na wao waone uchungu waupatao wenzao. Sasa hilo ndio linalowaumiza kichwa maadui wote wanaopanga kumsaidia Israel kupambana na Iran.

Wanajua kwamba mifumo ya Israel huwa haina shabaha katika vita, ndomaana mara usikie wamekosea wakalipua mpaka ofisi za UN, mara wameuwa waandishi wa habari, mara raia nk. Sasa wakikosea na shabaha ya huko Iran wakapiga raia, kisasi chake kitakuaje. Unaweza kutumia kichwa chako kutafakari vizuri kwamba kama mifumo ya ulinzi wa anga na wa jeshi Iron dome imeshindwa kuzuia makombora kupenya, vipi nyumba za kawaida za raia zilizojengwa kiholela kama vibanda vya wamachinga pale Karume Complex. Maafa yake si yataishangaza dunia.

Hivyo basi ili kuepusha hayo yasitokee ni lazima kuangalia strategy fulan itayoisadia Israel na Marekani zifute aibu yao. Sasa wameshaona kuwa shambulizi lao linaweza kusababisha hasara zaidi kwa Israel, maana kina Netanyahu wote makazi yao yanajulikana hata wakimbilie chini ya udongo watafuatwa tu na kombora. So ili kuepusha majanga hayo kutokea ni kutafuta tukio lolote ili liunganishwe na shambulizi kwa njia ya imani au kawaida. Mfano ikitokea soko au au uwanja hata wa mpira umepata hitilafu ya umeme na kuungua moto, basi tukio hilo haraka kupitia vyombo vya habari vya magharibi litatangazwa kama ni shambulizi la kimya kimya lililofanywa na Israel katika nchi hiyo yenye nguvu kubwa katika mashariki ya kati. Hili litaenda sambamba na kauli ya Biden kwamba alikuwa ameikataza Israel kufanya mashambulizi Iran, ila yenyewe imeamua kushambulia 😂😂😂

Nafikiri kila mtu anakumbuka lile shambulio la kwanza lilivyotengenezewa tukio. Kimya kilikuwa kingi kama hivi. Siku ambayo radi ilipiga ili mvua inyeshe, wazee wa kazi wakaliunganisha lile tukio ghafla na kisasi cha Israel. So na hili shambulizi litalipwa kwa njia ya tukio au kuvizia viongozi wa hezbullah wataoenda Iran kutembea, ila Netanyahu kufanya shambulizi kama anavyofanya huko Lebanon, Syria, Yemen na Gaza hana uwezo huo.
Uzi wa KINOKO hauna lolote
 
Wapige vile vinu vya Nyuklia
Hahaha waajemi ni akili kubwa sana ndomaana toka miaka ya 70 mpaka leo wanawatoa kamasi wazungu. Fikiria vikwazo vyote walivyowekewa, lakini jamaa bado ana uwezo wa kutengeneza silaha zake ambazo zina uwezo wa kufika eneo lolote la Israel na dunia kwa ujumla kwa sekonde kadhaa.

Hivyo vinu vya nyuklia kwa sasa ni kama bisheni tu kuuhadaa umoja wa mataifa. Lakini silaha ya nyuklia imeshatengenezwa kitambo na kuhamishwa pasipojulikana. Ndomaana unaona nchi za magharibi zinagwaya kuingia vitani na Iran. Maana wanajua jamaa hawatoweza kumdhibiti tena kwa vile kila silaha walionayo na yeye anayo. Na hicho ndo kinachompa kiburi cha kupambana na nchi zote hizo bila kuhofia kuvamiwa.
 
Huwa mnamwaibisha sana Allah wenu mlivyo na akili kiduchu😂😂
Mimi siamini katika imani za waarab, wazungu, wayahudi wala wachina.

Mimi naamini katika kile walichokuwa wanaamini babu zangu kabla ya bara letu halijavamiwa na hao waliowaletea miungu yenu.

Kitabu chao kishasema kabisa kuwa mungu wao ni mungu wa yakobo na tena ni mungu wa Israel. Halaf wewe mhehe na vizaka vyako unadai kuwa na wewe unahusika na mungu huyo wa yakobo na wakati hakulitaja jina lako wala Kabila lako katika kitabu chake. Sasa hiyo akili au kinyesi.
 
Umeandika kishabiki sana, yaani Iran iwe na uwezo wa kuipiga Israel? Ni Marekani au UK ndo walimuua Ismael Haniyeh ndani ya Iran? Ni Marekani ndo waliua viongozi wote wa Hezbollah?
Acha kujidanganya wewe.
Kama Hamas waliweza kuingia Israel wakauwa makumi ya wanajeshi wenye silaha na maelfu ya raia. Kisha kama hio haitoshi wakatoka na mamia ya watu kutoka Israel hadi Gaza bila kutambulika na mtu yoyote.

Sasa hauoni kwamba nchini humo hakuna mtu yoyote anaeweza kuwa salama including Netanyahu mwenyewe?

Pia kama raisi wa Marekani anashambuliwa mara mbili na vijana wadogo tu wasiokuwa na shabaha wala mafunzo yoyote ya kijeshi tena mbele vyombo vyote vya ulinzi na usalama, hauoni kwamba hakuna mtu yoyote ambae yupo salama Marekani?

Kama swala hilo liliweza kufanyika Marekani kwa raisi tena mbele ya vyombo vya ulinzi vyote vya usalama, basi usishangae kuwa linaweza kufanyika popote pale. Kikubwa na target tu na malengo.

Ukweli ni kwamba Israel haina uwezo wa kuipiga Iran hata ipewe ghala lote la silaha na Marekani.
 
Ata nzi akifa Iran awa vibwetele utasikia mossad kazin mtu anakupigia kwako jamaaa comedy ile mbayaa. Ingekuwa Iran ndio anapiga kigaid afu Israel ndio anapiga live heeee jF ingekuwa chungu lkn ivyo jamaa wao kaishiwa nguvu kutoka vita siku6 adi mwaka na mambo tu kutoka kushambulia kiume kama uko Syria anavyofanya adi kuwa gaid wazi wazi. Unamvia mtu kalala ndio unamshtukiza. Afuu wajinga uku kwetu wanasifia ugaid. Rkn duniani kwasasa habari ni Iran jamaa sasa anakubalika kapiga kiume ume adi na Leo Israel anajitafuta anagundua atosh kenge maji kasaza tuli. Aibu tupu domo kubwa nguvu una ww domo tu. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
😁😁😁😁😁😁
 
Kwanini Israel aombe nchi fulani impe space ili ashambulie Iran?

Hama uwezo wa kutuma vyuma moja kwa moja vikatua Tehran kama alivyofanya mbabe halisi Iran alirusha vyuma kwa ustadi mkubwa kutoka Iran hadi miji ya Israel bila kukosea target?

Israel is overrated lakini kiuhalisia ni mweupe mithili ya theluji. Mikwara mingi utekelezaji sifuri.
😁😁😁 Jamaa wako overrated mpaka Wana kera this time Iran imewaacha uchi
 
Mkuu kifo ni kifo tu, alisikika mama yetu mmoja akituasa:

Marekani na Israel ni mataifa tofauti yenye baadhi ya siri za pamoja, bila kulijua hilo, Iran au yeyote dhidi yao, ni mfu atembeaye!

Ukweli mchungu hii ni vita ya Marekani na Iran, Israel ni kikaragosi tu:

Palestina ni wahanga, Iran na Israel hawachekani, ila Marekani wapewe maua yao

Kwamba Iran atapigwa pigo moja kali, litakalomwacha mfu au kilema asiweze hata kurusha hata ngumi punde baada ya hapo? Mbona itakuwa ni kupaka rangi hewa kutotaka kulijua hilo?

Kwamba kuna mwenye shauku na eti popote alipo anashangazwa na chelewa chelewa ipi?

View attachment 3121392

Kwani hujui kulikuwa na kimbunga Milton huko Kwa mwenye vita vyake ewe ndugu unayedhani vita ni kama burudani ya kabumbu?
Ni hatari sana 😀😀😀
 
nahisi wanachofanya israel ni kutengeneza mifumo ya kujilinda zaidi kupunguza adhari za vita kwao..na ili kuweza kupigana na iran inabidi uwanja wa vita uwe iran au jirani na iran...wanatafuta uwanja huo uwe lebanon rejea ramani ya middle east...vita hapigani nyumbani kwake israel anakufuata huko ulipo sawa na amrekani..kwa hio akishaikamata lebanoni kama ilivyo gaza leo..lazima akiwashe na iran...na iran kama anataa vita salama kwake aingie ajiunge na hezbula kwenye uwanja wa vita hapo lebanon..
Utetezi wako hauna maana. Israel imekuwa ikidanganya watu kuwa ina silaha zinazoweza kufika eneo lolote la Iran. Sasa silaha hizo ziko wapi? Kwanini wasizitumie kujibu shambulizi? Yani mpaka wawe karibu na Iran ndo waweze kushambulia, mbona Iran inashambulia kutoka Iran hadi Israel?

Tena kwa shabaha halisi ya kulenga kambi za jeshi, headquarter ya MOSSAD nk bila kugusa nyumba yoyote ya raia wasiokuwa na hatia?

Mkubali tu kwamba Israel ina pewa promo isiyowa nayo na media za west, ila kiuhalisia jamaa hawana uwezo wa kupambana na Iran. Dunia ilikuwa hailijui hili, sasa ukweli umeanza kujidhihirisha wenyewe. Kumbuka ukweli na uongo huwa havichangamani. Hata vikae pamoja miaka 100, kuna siku vitatengana na ukweli utajulikana tu kama hivi.
 
Nilishasema NUCLEAR RODS zitakuwa overheated na kusababisha mlipuko mkubwa sana kwenye vinu vya kinyuklia. Serikali ya IRAN itajitokeza na kusema ni ajali ya kawaida kumbe ndani yake kuna jasusi la mossad linafanya kazi hapo hapo. Hence mission accomplished.


Namba 2. Sumu ya BOTOX au CYANIDE itatumika anywhere any point for massive caussalties in TEHRAN

Mind yu hapo BEIRUT kemikali ya AMMONIUM NITRATE iliyokuwa imetunzwa kwenye mapipa ya MELI iliyosajiriwa PANAMA ilimaliza mamia ya watu.

MOSSAD have ten thousand ways of reacting
Ni mpumbavu pekee anaeweza kuifananisha nchi isiyokuwa na uwezo wa kutengeneza hata sindano ya kushonea Lebanon na Iran ambayo imemsaidia hata mrusi silaha ya ndege zake zisizokuwa na rubani bure ili aitwange Ukraine na NATO kwa pamoja. Yani kwa mfano uliotoa sidhani kama ulifika elimu hata ya darasa la 4.

Ogopa watu ambao wanatengeneza silaha zao wenyewe na kuzitumia katika vita mbali mbali huko Syria, Lebanon, Iraq na Ukraine bila kuomba msaada hata wa sindano au viatu vya jeshi kutoka Marekani, UK nk.

Mtu asiekuwa na uwezo wa kutengeneza silaha na muombaji muombaji wa silaha za watu ili zimsaidie vitani ni muisrael peke yake na bado silaha hizo zinashindwa kumsaidia kulipiza kisasi maana hazitofika.
 
Back
Top Bottom