Pre GE2025 Lissu: Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu nikamwambia "Shenzi, kahonge wanaohongeka"

Pre GE2025 Lissu: Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu nikamwambia "Shenzi, kahonge wanaohongeka"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lisu anaongea mambo mengi ya maana kwenye hiyo mikutano yake, hizi chombeza ndogo ndogo kwenye mikutano yake msiziripoti maana hazina tija sana, ripotoni mambo yenye tija anayoongea.
 
Live kutoka viwanja vya stendi ya zamani Singida mjini, kipenzi cha watu na rais wa wananchi Tundu Antipas Lisu amefunguka na kusema alimtimua Abdul alipompelekea rushwa na kumwambia "shenzi kahonge wanaohongeka".

View attachment 3012128

Hakika Lisu ni mwadilifu mno huyu mwamba. Anastahili kuwa rais 2025. Na njia iko wazi kwake.
Muongo huyo bahatu nzuri kakutana na rais full of hekima na mweledi vinginevyo angepigwa risasi kama jpm alivyomkosa kosa kwa uongo wake
 
To become a Medical doctor or Engineer you need to have a good brain and good education, to become MWANASIASA you just need to be a good liar.
 
Live kutoka viwanja vya stendi ya zamani Singida mjini, kipenzi cha watu na rais wa wananchi Tundu Antipas Lisu amefunguka na kusema alimtimua Abdul alipompelekea rushwa na kumwambia "shenzi kahonge wanaohongeka".

View attachment 3012128

Hakika Lisu ni mwadilifu mno huyu mwamba. Anastahili kuwa rais 2025. Na njia iko wazi kwake.
Aisee machawa kwa hii clip watalala na viatu
 
Lissu aache siasa za kitoto aweke ushahidi wa kufikiwa na Abdul na kutaka kuhongwa, lakini pia apeleke TAKUKURU Ili wachukue hatua
Takukuru hii hii au nyingine? Ule ushahidi wa kina mnyeti kutoka kwa Nassari ulifanyiwa kitu gani ulipopelekwa tena video kabisa? Kama mlifungua DVR kwenye gari yake na CCTV kwenye alipigwa risasi mnapata wapi uhalali wa kudeal na haya mambo?
 
Lissu aache siasa za kitoto aweke ushahidi wa kufikiwa na Abdul na kutaka kuhongwa, lakini pia apeleke TAKUKURU Ili wachukue hatua
Unamuongelea wakili nguli.
Unafikiri hajui consequence ya kauli yake?
Unadhani hana ushahidi to back it up?
Mwenye jukumu ni takukuru,wao ndio wanatakiwa wamfate Lissu awape ushahidi,i doubt kama wanaweza kufanya hivyo.
 
“Abduli aliniletea rushwa nyumbani kwangu nikamwambia "Shenzi" kahonge hao wanaohongeka.”

Mh.Tundu Lissu
Leo Jumamosi
Saa 17:25
Singida Mjini
 
Attachments

  • VID-20240609-WA0108.mp4
    11.7 MB
Ulimuona huyo Abdul akienda kwa Lisu? Na Lisu Katoa ushahidi upi akiongea wa kuhibitisha kuwa Abdul alienda Kwake?

Kifupi Lisu anachofanya ni wasoni kupoteza Imani naye kama layman tu wa mitaani ambaye hayuko professional kwenye hotuba zake kageuka kuwa. Mswahili mumbeya tu wa barabarani anayetunga vitu vya uongo asivyoweza kuongwa kwa ushahidi kuithibitishia hadhira anayoihutubia
Ushahidi hutolewa mahakamani we bush lawyer.
Huyo Abduli aende mahakamani atapewa ushahidi.Anaogopa nini?
 
Back
Top Bottom