Pre GE2025 Lissu: Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu nikamwambia "Shenzi, kahonge wanaohongeka"

Pre GE2025 Lissu: Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu nikamwambia "Shenzi, kahonge wanaohongeka"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Uadilifu wa Lisu unaishia kwenye Acacia na MIGA

Tafuta katika Dunia nzima, hakuna mahali popote ambapo Lisu amewahi kituhumiwa kwa rushwa, iwe ni kuhonga au kuhongeka.

Sifa kubwa za TAL
1) Mtu mkweli katika mazingira yote bila ya kujali kitakachompata.

2) Mtu aliye na ujisiri wa pekee katika kuunena ukweli.

3) Asiyehonga wala kuhongeka kwa rushwa wala cheo.

4) Mtu aliyenyoka kwa kauli na matendo.

Watu wa namna hiyo, ni wachache sana Duniani na ni vigumu kuwapata. Ndiyo maana kwa wiki 2 mfululizo, baada ya kupigwa risasi, ndiye mtu aliyeandikwa na vyombo vingi vya habari vya Dunia kuwazidi watu wote Duniani.
 
Live kutoka viwanja vya stendi ya zamani Singida mjini, kipenzi cha watu na rais wa wananchi Tundu Antipas Lisu amefunguka na kusema alimtimua Abdul alipompelekea rushwa na kumwambia "shenzi kahonge wanaohongeka".

View attachment 3012128

Hakika Lisu ni mwadilifu mno huyu mwamba. Anastahili kuwa rais 2025. Na njia iko wazi kwake.
Huyu Abduli anapewa na nani hizo fedha?
 
sasackana ni hivyo mbona mnamloga?
Lisu anazungumza mambo ambayo yanafahamika na watu wote.

Ila tofauti yake ni kuwa yeye kama mwanasiasa hiyo ndio platform yake kuyazungumza.

Lakini hana maajabu yoyote ya kupewa rushwa.
 
Lisu anazungumza mambo ambayo yanafahamika na watu wote.

Ila tofauti yake ni kuwa yeye kama mwanasiasa hiyo ndio platform yake kuyazungumza.

Lakini hana maajabu yoyote ya kupewa rushwa.
Sasa unadhani kwanini Hangaya alimtuma Abdul?
 
Sasa unadhani kwanini Hangaya alimtuma Abdul?
Siwezi thibitisha ukweli wa hili jambo.

Pia sipo kwenye kichwa cha huyo "hangaya" na "abdul" kuweza kujua waliamua nini.

Hizi zitabakia tu kuwa story za kufurahisha genge.

Lakini uhalisia ni kuwa mwananchi wa kawaida anateseka kwa ukali wa maisha.
 
Vitu vya kufikirika ambavyo hata ueue ushahidi hajatoa hata wa picha tu anaishi kizanani kuwa anayeona nimemsena aende mahakamani

Ana Mambo ya kitoto ya law class 101 mwaka wa kwanza kipindi Cha kwanza
Naona wewe hujui lengo lake ni nini hapo, ndiyo maana huelewi. Hiyo ya "law class 101" naona hata wewe mwenyewe huamini kuwa kweli umeandika hivyo ili uonekane unajibu hoja!
 
Sasa unadhani kwanini Hangaya alimtuma Abdul?
Ulimuona huyo Abdul akienda kwa Lisu? Na Lisu Katoa ushahidi upi akiongea wa kuhibitisha kuwa Abdul alienda Kwake?

Kifupi Lisu anachofanya ni wasoni kupoteza Imani naye kama layman tu wa mitaani ambaye hayuko professional kwenye hotuba zake kageuka kuwa. Mswahili mumbeya tu wa barabarani anayetunga vitu vya uongo asivyoweza kuongwa kwa ushahidi kuithibitishia hadhira anayoihutubia
 
Nenda mahakamani
 
Aliyekwambia Lisu atakuwa mgombea Uraisi wa Chadema mwakani nani? Chadema Kuna mtu wanamwandaa

Lisu hata nafasi ya umakamu mwenyekiti safari hii hapati
sawa, ujue huyo mgombea wao wa suprising ataangukia pua nyuma ya mama samia kama wataleta mgombea asiye na mvuto
 
Wasomi wenyewe ndiyo kama wewe usiyejulikana hata na mzazi wake. Msomi uchwara. Unajifananisha na Lisu??
Lisu huyu anayeongea kama layman kuhusu Abdul na mama Abdul Bila kuweka ushahidi anapohutubia usomi hautaki hivyo
 
Ulimuona huyo Abdul akienda kwa Lisu? Na Lisu Katoa ushahidi upi akiongea wa kuhibitisha kuwa Abdul alienda Kwake?

Kifupi Lisu anachofanya ni wasoni kupoteza Imani naye kama layman tu wa mitaani ambaye hayuko professional kwenye hotuba zake kageuka kuwa. Mswahili mumbeya tu wa barabarani anayetunga vitu vya uongo asivyoweza kuongwa kwa ushahidi kuithibitishia hadhira anayoihutubia
Sasa kama ni hivyo unavyo fikiria wewe, tatizo liko wapi?
Kwa vile watu anaohutubia watamwona kuwa na sifa hizo unazodai, si hiyo ndiyo itakuwa nafuu kwenu, au unatakaje?
 
Wasomi wenyewe ndiyo kama wewe usiyejulikana hata na mzazi wake. Msomi uchwara. Unajifananisha na Lisu??
Kujulikana sana sio sifa kuwa uko Vizuri sana kichwani

Mfano hakuna mtanzania asiyejua mnyama aitwaye Mbwa

Lakini mbwa hajawahi kuwa mwanasiasa Wala kuhutubia popote na hatarajii lakini anajulikana sana
 
Back
Top Bottom