CCM na idara zake mwaka huu wanapata tabu sana, haiwezekani mtu asubiri kibali muda wote huo wasikitoe, huu ni mchezo mchafu unaofanywa na mamlaka ya anga Tanzania.
Wakati wa tension kama huu mambo ya kijinga kama haya hayatakiwi kuwepo, ndio yanazidisha chuki na hasira, halafu mwishowe watu wakidai haki zao wanapigwa risasi bila sababu huku mkiimba wimbo wenu wa amani...amani!.
Idara za serikali hata kama zinatumika na CCM ziache uzembe usiokuwa na sababu za msingi kuepusha maafa, msisubiri mpaka mtu alalamike ndio mchukue hatua, timizeni wajibu wenu.