Hatuwezi kuishi kwenye nchi ya kipuuzi namna hii. Yaaani binadamu mwenzetu anaonewa kiasi hiki tena waziwazi na wala tusichukue hatua.
Walimpiga risasi wakitaka kumuua, akapona mauti ila wakamnyima matibabu, akapona kabis wakamvua ubunge na kukataa kumlipa hata kiinua mgongo kwa kipindi alichotumikia.
Sasa amegombea uraisi hawaachi figisu, mikoa ya kusini wamemzuia kufanya mikutano zaidi ya 10, na Mkoa wa Pwani pia, kisa magufuli ameshindwa kufanya kampeni kusini.
Sasa leo anakuja kufunga kampeni Dar wanamletea figisu tena kwa makusudi. Sasa tunasema imetosha!!!!
Kesho kwa hasira tunaenda kupiga kura nyingi kwa Lissu na tutalizilinda hakika kwa gharama ya damu zetu. Hata tukifa ila historia itatukumbuka.