PreGE2025 Lissu ameiweka Chadema kwenye mtego mbaya sana. Oneni hapa

PreGE2025 Lissu ameiweka Chadema kwenye mtego mbaya sana. Oneni hapa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
If care is not taken.

Jina : Tundu Antipus Lissu.
Umri: Miaka 57.
Occupation: Mwenyekiti Chadema.
Idadi ya wabunge: Sifuri.
Idadi ya madiwani: Sifuri.
Idadi ya wenyeviti serikali za mitaa: O.

.. ..........

Jina : Zitto Kabwe.
Umri : 49.
Kazi : Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chama : ACT.

Idadi ya wabunge Tz Bara: 47.

Madiwani : 659.

Mameya : 10.

,.........

Lissu kaiweka Chadema pabaya mno kuliko wanavyo fikiri
Ndoto za alinacha
 
20250411_134158.jpg
 
👉Chadema hawatoshiriki uchaguzi wa mwaka 2025 huku vyama vingine vyote Viki shiriki.

👉 CCM wataitumia hii situation kama fursa ya kuiua nguvu ya Chadema kwa kutengeneza "Chama Kikuu Cha Upinzani".

👉 Chama hicho kitakuwa ni ACT Wazalendo. Kitapewa viti vya kutosha bungeni na kwenye udiwani. Sababu itakuwa ni kuionyesha dunia kwamba Uchaguzi ulio fanyika Tanzania ni wa huru na haki. Hoja ya Tume Huru ya Uchaguzi utazikwa rasmi kwa sababu itaonekana haina mashiko.

👉 Kwa miaka yote mitano Chadema haitosikika kwenye majukwaa rasmi ya kisiasa( Bungeni etc) . Wakati huo huo kwa kushirikiana na CCM kimkakati, watatengenezwa wabunge machachari kutoka ACT ambao watakuwa wanaibua hoja nzito ambazo zitakuwa zinafanyiwa kazi.

👉 Wa Tanzania wengi watavutiwa na ACT kwa kuiona chama chenye mipango na mikakati inayo tekelezeka.

PICHA LITAANZA RASMI MWAKA 2030.
....................

1. Kwanza kabla ya yote wakati huo Lissu atakuwa na miaka 62.

2. Hakutakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi( Anayo itaka Lissu) na badala yake tume itakuwa hii hii.


NGOMA ITAKUWA HAPA? 👇👇👇
.................................

👉 Chadema ili kuendelea kujiheshimisha kwa wafuasi wao ( Yericko Nyerere anawaita wanaharakati wa mitandaoni) itabidi iendelee kushikilia msimamo wake wa kutoshikiriki uchaguzi.

👉 Tume ya uchaguzi haitobadilishwa.

👉 Chadema hawatoshiriki tena uchaguzi. Uchaguzi utafanyika. So Chadema wataendelea kuwa nje ya ulingo wa siasa rasmi kwa miaka mingine mitano. Wakiendelea na msimamo huu maana yake Chadema yenye wabunge, madiwani, mameya etc, itakuwa ndo imekufa hivyo.

👉 Hiyo mwaka 2030 Chadema wakisema washiriki uchaguzi bila mabadiliko ya Tume wanayo yataka wao, wataonekana hawana msimamo na hawajui wanacho kitaka wala kukisimamia jambo ambalo litawaondolea credibility ya kisiasa kwa wananchi. Mtego mkubwa kweli huu.

USHAURI WANGU :

Chadema walipaswa kujifunza mbinu za kijasusi jinsi ya kushinda uchaguzi na kuchukua dola, kupitia tume hii hii iliyopo. Kama. Wana watu smart, Inawezekana!!.
Kwa hiyo hayo yanafanyika kwa maslai ya nani ? Watu wanataka mambo yanayo fanyika kwa maslai ya wananchi siyo vinginevyo tatizo lenu wapumbavu mnadhani siasa ni ushabiki kama wa simba na yanga
 
Sema wanachadema watahamia vyama vingine na kushinda ubunge,

Then vyama vingine vitapata nguvu na chadema itasahaulika rasmi
100% Fact.


Lissu ameiua Chadema.

Wakati mwingine busara ni bora kuliko sheria
 
Back
Top Bottom