PreGE2025 Lissu ameiweka Chadema kwenye mtego mbaya sana. Oneni hapa

PreGE2025 Lissu ameiweka Chadema kwenye mtego mbaya sana. Oneni hapa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
CDM wameamua kupigania haki na sio kushiriki kwenye sinema za kuwahadaa Watanzania.

Bora CDM Ife kuliko kushiriki kwenye dhambi ya kudhulumu haki za watu.
Aisee
 
NO REFORMS NO ELECTION ndo mpango mzima.
Hao wenye ndoto za kuwa vyama vikuu vya upinzani
watasubiri sanau Tusiongee mengi tusubiri ifike oktoba.
wenye ccemu yao wameichoka,sasa hao wanaosubiri kuokota mizoga wataipata wapi wakati simba
anayejua kukamata na kuua nyati kauwawa?
Hakuna chama cha kuwa chama kikuu cha upinzani wakati vyote nvingine ni ccm
 
👉Chadema hawatoshiriki uchaguzi wa mwaka 2025 huku vyama vingine vyote Viki shiriki.

👉 CCM wataitumia hii situation kama fursa ya kuiua nguvu ya Chadema kwa kutengeneza "Chama Kikuu Cha Upinzani".

👉 Chama hicho kitakuwa ni ACT Wazalendo. Kitapewa viti vya kutosha bungeni na kwenye udiwani. Sababu itakuwa ni kuionyesha dunia kwamba Uchaguzi ulio fanyika Tanzania ni wa huru na haki. Hoja ya Tume Huru ya Uchaguzi utazikwa rasmi kwa sababu itaonekana haina mashiko.

👉 Kwa miaka yote mitano Chadema haitosikika kwenye majukwaa rasmi ya kisiasa( Bungeni etc) . Wakati huo huo kwa kushirikiana na CCM kimkakati, watatengenezwa wabunge machachari kutoka ACT ambao watakuwa wanaibua hoja nzito ambazo zitakuwa zinafanyiwa kazi.

👉 Wa Tanzania wengi watavutiwa na ACT kwa kuiona chama chenye mipango na mikakati inayo tekelezeka.

PICHA LITAANZA RASMI MWAKA 2030.
....................

1. Kwanza kabla ya yote wakati huo Lissu atakuwa na miaka 62.

2. Hakutakuwa na Tume Huru ya Uchaguzi( Anayo itaka Lissu) na badala yake tume itakuwa hii hii.


NGOMA ITAKUWA HAPA? 👇👇👇
.................................

👉 Chadema ili kuendelea kujiheshimisha kwa wafuasi wao ( Yericko Nyerere anawaita wanaharakati wa mitandaoni) itabidi iendelee kushikilia msimamo wake wa kutoshikiriki uchaguzi.

👉 Tume ya uchaguzi haitobadilishwa.

👉 Chadema hawatoshiriki tena uchaguzi. Uchaguzi utafanyika. So Chadema wataendelea kuwa nje ya ulingo wa siasa rasmi kwa miaka mingine mitano. Wakiendelea na msimamo huu maana yake Chadema yenye wabunge, madiwani, mameya etc, itakuwa ndo imekufa hivyo.

👉 Hiyo mwaka 2030 Chadema wakisema washiriki uchaguzi bila mabadiliko ya Tume wanayo yataka wao, wataonekana hawana msimamo na hawajui wanacho kitaka wala kukisimamia jambo ambalo litawaondolea credibility ya kisiasa kwa wananchi. Mtego mkubwa kweli huu.

USHAURI WANGU :

Chadema walipaswa kujifunza mbinu za kijasusi jinsi ya kushinda uchaguzi na kuchukua dola, kupitia tume hii hii iliyopo. Kama. Wana watu smart, Inawezekana!!.
Mbona inasemekana ACT ni CCM B?
 
Hakuna Chama Chochote kitakachokuja kuwa na nguvu Kama Chadema hapa Tanzania .

Chadema ni taasisi kubwa ambayo haitegemei ubunge , udiwani au ruzuku ili kujiendesha .

Chadema ipo mbali Sana
 
Back
Top Bottom