Pre GE2025 Lissu anaenda kumshinda Mbowe kwenye huu uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwa wajumbe gani mkuu? Hawa hawa waliomsindikiza leo kuchukua fomu? Au kuna wengine?
 
Kama kweli Mbowe kalamba asali ya Abdul na hataki kuonekana kumgeuka sponsor kama bado anakipenda chama chake na kuthamini imani ya Watanzania basi hapa kwenye uchaguzi ndio chance yake ya kumwaga sponsor na kustaafu japo sio kwa heshima ambayo angepewa kama asingegombea.
 
Mkuu imani yako ,ipo deep sana ,naungana na wewe
 
Lussu hawezi kupata 15% labda mdude na yule Askofu wa mchongo wapige kura mara 500.
 
Andiko linatia moyo team lissu. Je atashinda mbele ya mwamba mbowe mwenye chama? Lissu ana misimamo imara kuhusu mambo muhimu ya kitaifa, unathani system watakubali ashinde na kuja kumpa mgombea wa ccm alazimike kufanya kampeni kubwa nchi nzima wakati kina mbowe, lipumba ni wepesi sana mbele ya mama? Lissu ana shughuli pevu kumshinda mbowe
 
Mbowe atashinda kwa kishindo kwa sbb mpaka sasa wenyeviti karibu wote wa kanda ni team mbowe. Wapiga kura waliowachagua wenyeviti kanda ndio haohao wana kuja kumchagua mwenyekiti Taifa.
 
Kwa taarifa yako kabla, wakati na baada ya uchaguzi CCM wapo na Mbowe kwa asilimia karibu zote. CCM wanamwogopa Lissu kwa sababu ana Akili kubwa hivyo:-
1. Hawezi kurubuniwa kwa vyovyote vile.
2. Hawezi kuhongwa kwa namna yoyote ile.
3. Siku akianzisha mapambano ya kudai kwa mfano Katiba mpya hawezi kurudi nyuma mpaka itakapokuwa imepatikana.

Tofauti na Mbowe. Mbowe anazungumzika kwa CCM. Ukitaka kuthibitisha hilo ni kwamba, Lissu alipotangaza tu nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti, alianza kupata vitisho, lakini Mbowe hajawahi kupata vitisho vyovyote. Mtu anayepata vitisho ni yule aliye tishio kwa mfumo.

Lissu alipigwa risasi kwa sababu alikuwa tishio kwa mfumo.

Mbowe si tishio kwa CCM hata kidogo ndo maana hajawahi kupigwa risasi wala kutishiwa. Mbowe anazungumzika na CCM.

Chini ya uenyekiti wa Mbowe, hakuna siku Tanzania itapata either Katiba mpya au Sheria bora za Uchaguzi, never.
 
Lissu nilitamani sana ashinde lakini haitakuwa vyepesi. Kilichofanyika serikali za mitaa kinaenda kufanyika kwenye huu uchaguzi wa ndani wa Chadema.

System inamtaka Mbowe kuliko Lissu na katika uchaguzi huu pesa inaenda kutembea haijawahi kutokea. Lissu kukiwa na uwazi na uchaguzi huru anamgalagaza Mbowe asubuhi na mapema kwasababu watu wengi wamechoka na namna ambavyo Chadema inaendeshwa kwa sasa na Mbowe mwenyewe ni aidha amechoka kuwa upande wa upinzani au ameshafika bei na anataka uenyekiti ili kumrahisishia Samia kushinda uchaguzi wa mwakani.
 
Hakuna uchaguzi hapo, ukiona pesa haramu za CCM zimepenyezwa mahali ujue hakuna haki yoyote itatendeka.

Ashukuriwe Lissu amekuwa muwazi tumeijua Chadema na mamluki wake.
 
Lissu hawezi kwenda ACT maana anaijua ni Ccm B kama atafanyiwa mizengwe ataamua tu kuachana na siasa na kutumikia taaluma yake au anaweza kuamua kuishi nje ya nchi.
 
TAL ashinde asishinde, ila kaonyesha njia, uthubutu. Napenda mtu anayepigania anachokiamini na kujaribu. Kuna wanafiki wanatamani kugombea, ila wakiwaza watakwazana na Mbowe wanaacha.
#Ulipotupo
#TunaendanaLissu
#Lissukwaukwelinauwazi
 
Lissu hafiki popote. Niko pale Kimara Kibo niite mbwa
 
Chadema ni wakati wa kufungua macho, fikiria kwa makini, mpeni mtu atakaesimama kama "mpinzani wa kweli " mpaka sasa ninaona upinzani kama kichekesho tu.
 
Chadema ni Mbowe na Mbowe ni Chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…