Lisu anaongelea tu majimbo kujiamulia mambo ila haelezi gharama za uendeshaji jimbo litatoa wapi
Anaeleza kijanja janja huku akificha kuwa uendeshaji jimbo unatakiwa uendeshwe kwa pesa za ndani ya jimbo ikiwemo miradi ya maendeleo
Chukulia Singida tegemeo lake kuu la uchuimi ni kuuza vidumu vya mafuta ya alizeti.hivyo vyaweza jenga barabara za lami? Kilomita moja tu ya lami inasoma Gharama ya bilioni moja .Hivyo vidumu vya alizeti vyaweza jenga barabara na kulipa mishahara ya wafayakazi wa jimbo?
Afafanue pia kuhusu gharama za kuendesha jimbo asilaghai tu ohh mujiamulie wenyewe!!!
Ukimsikiliza uaona kabisa mlaghai kwenye gharama Za uendeshaji na za miradi ya maendeleo zitakako toka hagusi anahamia hoja nyingine mbio
Nadhani lazima utambue kuna miundombinu ya kitaifa na ile ya kijimbo
Ile ya kitaifa ikiwa chini ya TANROAD
Na ya kijimbo chini ya TARULA
Ya kitaifa lazima serikali kuu ishughulike nayo
Hizi za kijimbo utaratibu ukiwekwa vizuri inawezekana kabisa.
Singida na mikoa mingine unayoona haitakuwa na vyanzo vizuri vya uchumi , ni kwa sababu tu ya elimu yako ndogo na mawazo finyu ya wazee wa ccm.
Kuna namna nyingi za kufungua fursa katika maeneo hayo na yakawa potential kuliko hayo unayodhani.
Hii ni mifano michache tu
1. Serikali ya kijimbo inaweza ikawekeza kwenye kilimo na kukikuza zaidi kwa upande wa mazao yanayokubali mkoa huo kama alizeti na vitunguu.
Hapa itahakikisha miundombinu ya umwagiliaji na matractor yanasaidia kukuza shughuli za kilimo jimboni.
2. Lazima serikali hii ifanye bidii kujenga viwanda vikubwa zaidi vya ukamuaji mafuta vitakavyo wanufaisha wakulima na sio vile vya wanyonyaji wafanya biashara
3. Hapa vinaweza kuwekwa viwanda mbali mbali ambavyo uendeshaji wake hauhitaji matumizi makubwa ya maji kwa kuanzia mfano cement, ili vilete ajira na kodi kwa jimbo
Lakini pia tafiti za vyanzo vya maji ya chini (underground water sources) zifanywe.
4. Jimbo lihamasishe kilimo cha nyuki na kuwasomesha wataalamu wengi wa asali ili wawasaidie wakulima namna ya kuendesha shughuli hii kwa faida
5. Jitihada zifanywe kufungua viwanda vitakavyozalisha vifaa maalumu vya uvunaji asali kwa mahitaji ya kitaifa sio kulenga singida tu. Hii itasaidia kushusha gharama za uzalishaji wa asali kushuka ili soko la asali yao liwe juu na kwa bei affordable.
Hata hivyo tafiti ziendelee kufanywa ili vyanzo vingi zaidi vya kiuchumi viendelee kugundulika kwa manufaa ya watu wa mikoa hiyo
Maana tafiti hizo ndizo zilizofanya kanchi kadogo na jangwani kama israel kufanya vizuri kwenye uzalishaji wa chakula
Huu ni mfano kwetu tujifunze