Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ipo nusu kaputi, Mbowe hataki kupambana na Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mabadiriko ni muhimu sana, vinginevyo tutakuwa kama nyani tu, alivyoishi babu hata kitukuu kinaishi kama babu. Kama dunia inabadilika lazima watu, mifumo, tabia , taratibu na mbinu zibadirike ili kufikia malengo kulingana na mshindani wako
 
Nimesikiliza hayo mahojiano ila sikusikia chadema ipo nusu kaputi.
Maybe i overlooked.
#CRITICAL THINKER.
 
Muulize lissu anackuwa controlled na msigwa QUOTE="CHIEF PRIEST, post: 52249981, member: 658193"]
Wewe jamaa ni mpuuzi huyu Msigwa labda ni basha wako unamsifia sana atakuwa anakupiga mashine.
[/QUOTE]
 
Lissu ndiye mwenyekiti wa CHADEMA ajaye, tumechoka kuongozwa na kilaza.
 
Siungi mkono mbowe kuendelea na uenyekiti lakini naona pia hatari kubwa ya Lisu kuwa mwenyekiti.
 
Lissu na machine kubwa ,angekuwa ni mwanachama mwingine nadhani Mzee Mbowe angekuwa ameshachuka hatua za kumfukuza kwenye hii kampuni yake.Hakika mzee Mbowe kayakanyaga,
πŸ€ͺπŸ€ͺπŸ€ͺπŸ€ͺπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€ͺπŸ€ͺ
 
Yote ni sawa. Ninachopinga ni "the way he went about it". Alichokifanya ni badala ya kuonyesha tatizo lilikuwa CCM amemgeuza Mbowe kuwa ni tatizo. Sasa hivi kelele ni Mbowe must go sio CCM must go. Ukimya wake kwenye suala hili kunaashiria anakubalia hizo kelele.

Wakati John McCain alikuwa anagombea urais alijizolea sifa alipomzima shabiki wake aliyekuwa anamsemea ovyo Obama. Lissu anatakiwa kuweka wazi kuwa tofauti yake na Mbowe ni approach na sio personal. Kama bado anamheshimu Mbowe angeliweka hili wazi. Lakini kama hamheshimu na anamuona ni mwizi n.k. aende full blast kama walivyofanya wakina Lijualikali, Msigwa n.k. Ni vigumu kuamini kuwa hakuhusika katika fujo alizokuwa akizifanya Msigwa kabla ya kuondoka.

Labda anayofanya sasa hivi ni pre emptive ili ikiwekwa wazi uhusika wake katika kumchimba Mbowe ionekane anafanyiwa hivyo kwa sababu amediriki kuona sumu.

Kwangu mimi baada ya Slaa, Halima na Msigwa hamna kitakacho nishangaza.

Amandla...
 
Hapana.
Kwa kukufahamu kwa michango yako humu JF, niseme tu kwamba, kwa heshima kubwa sikubaliani na wewe katika hili la Mbowe kuwa 'pragmatic'. Kuna zaidi ya 'pragmatism' inayo tawala akili zake baada ya hayo mazungumzo ya Maridhiano na mtu aliye mlaghai kwa uwazi kabisa na kumchota akili zake.
Tabia ya Mbowe na namna yake ya uongozi baada ya hayo mazungumzo ilibadilika kabisa na wala haijarudia tena kama ilivyo kuwa huko siku za nyuma.
Nasema hivyo kwa dalili mbali mbali alizo onyesha Mbowe mwenyewe.
Kwa mfano, mara yangu ya kwanza kabisa kumtilia mashaka Mbowe ni ile hotuba yake aliyo itoa na ikawekwa humu JF, wakati alipo tembelea huko ughaibuni na kuzungumza na wanao itwa diaspora. Maelezo yake kwenye hotuba ile yalionyesha kabisa kuwa yeye ni mtu wa Samia moja kwa moja na asinge penda watu waseme chochote kumhusu huyo mama. Hiyo hotuba itakuwa mahali, humu humu JF. Ikilazimu kuitafuta tutafanya hivyo.

Pili, kuna swala la COVID-19 Bungeni. Mbowe hata siku moja hajawahi kuwa muwazi jinsi hao mabinti walivyo ingia bungeni. Kama swala hili alisha litolea msimamo, basi inawezekana sikuupata. Hii ni aina ya uongozi usio tofautiana sana na huu tunao ushuhudia ndani ya CCM, siyo uongozi wa kuwa 'pragmatic.'.

Hata baada ya Samia kudhihirisha waziwazi jinsi alivyo mwacha kwenye mataa; wakati alipo amua wazi kuwa hakuna mabadiliko yoyote ya maana juu ya waliyo kuwa CHADEMA wakiyadai, e.g., Tume Huru ya Uchaguzi na Marekebisho ya sheria muhimu za kufanya chaguzi ziwe na maana, Mbowe hajasimama kama yule Mbowe alivyo kuwa kabla ya kuwekwa mfukoni na mama wa Kizimkazi. Kama kuna hotuba yoyote aliyo itoa Mbowe juu ya jambo hili, naomba unikumbushe; binafsi sijawahi kumsikia kinaga ubaga, kama ilivyo kuwa kawaida yake huko zamani.

Pamoja na kwamba Samia katumia njia za ulaghai na hadaa huko mwanzo wa utawala wake, ili aonekane kuwa ni tofauti na Magufuli; lakini matendo yake yote matokeo yake hayakutofautiana na aliyo kuwa akifanya Magufuli. Lengo limekuwa ni lile lile la kuidhoofisha CHADEMA
Lakini hata Samia mwenyewe alipoona arudie njia zile zile za Magufuli za kutesa na kuua wanachama na wapenzi wa CHADEMA, umemsikia au kumwona Mwenyekiti wa chama akisimama mbele kama zile siku za Magufuli? Hii 'pragmatism' imekuwa ni tatizo?

Mwisho mkuu 'Fundi Mchundo', kwa maoni yangu ni kama nina muelewa Mwenyekiti Mbowe katika mabadiliko yake haya ya uongozi chini ya serikali ya mama Samia Suluhu Hassan na CCM anayo iongoza. Nadhani 'pragmatism' unayo izungumzia wewe, chimbuko lako litakuwa hapa. Mwenyekiti Mbowe ni muumini mkubwa wa mtindo wa uchumi anao usimamia Samia Suluhu Hassan. Kwa upande huo sioni namna Mbowe anavyo weza kupingana na Samia. Yale mazungumzo ya mardhiano, bila shaka yalijikita zaidi kwenye maswala wanayo kubaliana upande huu na kukubaliana kuwa watakuwa upande mmoja. Na pengine, ni kweli Samia alikuwa amenuia kulegeza kidogo kwenye eneo la kuwasulubu CHADEMA, hadi ilipo bainika kuwa huko ndani ya CHADEMA kulikuwa na vichwa ngumu ambao Mbowe hakuonekana kuwa na uwezo wa kuwadhibiti. Na kwa upande wa Samia mwenyewe, lile kundi la Magufuli na wahafidhina wengine likawa linamzidi nguvu Samia mwenyewe na mipango yake na mwenzie wa CHADEMA. Sote tume shuhudia alivyo babaika huyu mama kwa teuzi na tenguzi zisizo na kikomo.
Bila shaka kukawa na mipango ya kuyaepuka makundi haya kwa pande zote mbili; kwamba CCM ya Samia na CHADEMA ya Mbowe washirikiane wakati mahususi utakapo wadia ili waungane mithili ya yale tunayo yaona kila mara huko nchi jirani yakitokea wakati wa chaguzi zao.
Kwa hiyo, wakati sahihi ndio huu. Kwa CHADEMA, mnyukano ndio huo, kuelekea kwenye Mwenyekiti kuiwasilisha CHADEMA yake kwa Suluhu Hassan. Lisilo julikana bado, ni kama kwenye hili pia Mwenyekiti anaweza kuwa kaingizwa choo cha kike? Maana ule uchafuzi wa serikali za mitaa sioni kama Samia atamhitaji Mbowe kwa sababu yoyote ile.

Mwenyekiti Mbowe amekengeuka, na asipo stuka, CHADEMA ndiyo hivyo inaanza msambaratiko. Sioni jinsi Mbowe atakavyo weza tena kuisimamizsha na kuwa imara aking'ang'ania kuwa Mwenyekiti wa chama hicho.
 
Na hapa ndipo tatizo linapoanzia. Chadema wameiga mambo mengi sana ya ccm, na hivyo kukifanya chama hiki kisiwe na tofauti kubwa sana na ccm kiutendaji na mwenendo wake.
Kuna mazuri ya kuiga, toka huko CCM, lakini naona CHADEMA hawayafanyi hayo. Kwa mfano Namna CCM ilivyo jiimarisha hadi huko mitaani kwenyewe. Muundo huu wange utilia nguvu CHADEMA; hata hiyo Dola inayo tegemewa na CCM kuwabakisha madarakani isinge mudu kudhibiti nguvu za wananchi nchi nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…