PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Mbowe ana wabunge wangapi kwa huo umakini wake? Uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji umempatia viongozi wangapi? Kutoka wangapi?Mbowe ni mwanasiasa, mwanasiasa makini hutumia hoja, dialogue, ballot box kushika dola na anaweza kuvumilia hata miaka 50, tofauti na mwanaharakati anayetaka shortcut kutimiza malengo yake iwe kwa mapambano au hata kumwaga damu.
Umeona huna cha kumfundisha wala kumshauri Lissu, umeamua kujaribu kumshauri ujinga na upumbavu.Lissu anatakiwa apate washauri wazuri wa siasa atofautishe siasa na uanaharakati, asijifananishe na akina Maria Sarungi ambao hawana dhamana ya wanachama wanaweza kusema chochote na wasihojiwe na yeyote.
Awe na uvumilivu, aambiwe hawezi kupambana na dola akabaki salama vile vile aambiwe huwezi kupambana na boss wako ukabaki salama.
Kumbuka nchi zote za Afrika zilipambana na dola za kikoloni kudai Uhuru. Zanzibar alikuwepo Sultani, watu wakapambana na kufanya mapinduzi.
Unataka kuongea kitu gani?