Lissu ni Kiongozi sahihi, lakini kwa nchi isiyo sahihi

If to do were as easy as to know what were good to do, chapels had been churches, and poor men’s cottages princes’ palaces. It is a good divine that follows his own instructions: I can easier teach twenty what were good to be done, than be one of the twenty to follow mine own teaching.
William Shakespeare, The Merchant of Venice
 
Napenda nitoe maoni yangu kuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Tundu Lissu. Kwangu namuona kama Kiongozi sahihi, lakini kwa nchi isiyo sahihi.

Nitafafanua kwanini nasema hivyo.

1. Lissu kama Kiongozi sahihi.
Mh. Lissu ni Kiongozi sahihi kwa sababu amejipambanua msimamo wake, tangu awali. Amekuwa mstari wa mbele kupigania haki tangu utawala wa Mkapa, utawala wa Kikwete, utawala wa Magufuli na kwa sasa utawala wa Samiah. Ni viongozi wachache huwa na msimamo usiyoyumba kwa kipindi kirefu cha miaka Zaidi ya ishirini na sita (26). Viongozi wengi huyumba misimamo ila Lissu amekuwa consistent.

Kwanini nasema Lissu ni Kiongozi sahihi?. Lissu amejipambanua kama Kiongozi asiyekata tamaa. Hii nisifa kubwa kwa Kiongozi ya kwamba usikate tamaa hata kama kifo kipo mlangoni Pako.

Kwa mfano, tangu amiminiwe risasi, afukuzwe ubunge, uchaguzi uharibiwe 2020 na Sasa kesi ya uhaini. Hajawahi kukata tamaa. Mwingine kwa zile risasi angekimbia nchi milele na wala asirudi. Au angekubali yaishe Moja kwa Moja akaenda CCM na kujisalimisha ili asiendelee kusumbuliwa.

Pia Lissu sio fisadi. Naamini Lissu angekuwa anajihusisha na ufisadi au biashara, serikali ingeingia kati ili kumlipua mbele ya umma. Hivyo ni Kiongozi msafi na Hana doa sifa ambayo viongozi wengi Tanzania wamekosa.

Hivyo, Lissu anastahili sana kuwa Kiongozi wa Taifa la Tanzania maana amekuwa na msimamo usio yumba, sio fisadi na anahimili changamoto zozote dhidi yake.

2. Nchi isiyo sahihi
Pamoja na Lissu kuwa Kiongozi sahihi lakini changamoto ni kwamba yupo kwenye nchi isiyo sahihi. Naona Tanzania kama nchi isiyo sahihi kwa Lissu kuwa Kiongozi wake.

Kwanza, Tanzania inapenda viongozi wanafiki na waongo. Ukiwa mkweli unakuwa adui wa umma. Sasa Lissu ni mkweli hivyo ukweli wake unachukiza watu wengi wakiwemo viongozi na wananchi kwa ujumla. Kwa mfano, Lissu kasema mfumo wa uchaguzi ni mbovu tangu zamani na kudai kama mfumo hautabadilishwa atakinukisha. Kwa kauli hiyo kapewa kesi ya uhaini.

Pili, Tanzania haina mfumo bora wa uchaguzi. Kutokana na mfumo wetu wa uchaguzi kupata viongozi wazuri ni kazi sana. Mfumo wetu unaruhusu viongozi wenye pesa, Mafisadi, connection, undugu, uccm kupata nafasi za uongozi. Hivyo mtu kama Lissu ambaye sio fisadi, hana connection, sio CCM , hajajilimbikizia mali , mfumo wa uchaguzi wa Tanzania utamptapika.

Tatu, Tanzania ina wananchi ambao hawana interest na mambo ya siasa. Watanzania kwa ujumla wao wana interest na mambo ya dini, mpira na muziki. Hivyo vitu vitatu ndivyo vinapata sana uungwaji mkono Tanzania. Hivyo wengi wanaweza kuona harakati za kisiasa za Lissu hazina maana kwao. Watanzania hawajali kile ambacho Lissu anakipigania maana sio interest yao. Hii ingekuwa tofauti kama Lissu angekuwa Ghana, South Africa, Kenya, Marekani etc,

Nne, Tanzania imemtesa sana Lissu. Tangu aanze harakati za siasa na kupigania haki ni mateso juu ya mateso. Fikiria amepigwa risasi Tanzania, akiwa kwenye matibabu akafukuzwa ubunge, akiwa nje ya bunge hakulipwa stahiki zake, na hata aliporudi kugombea urais alifanyiwa vitimbi ikiwemo uchaguzi wa 2020 kuporwa kabisa. Na kwa Sasa ana kesi ya uhaini ambayo mwisho wa siku akipatikana na hatia atangongwa hadi kufa.

Nihitimishe kwa kusema kama ilivyokuwa kwa Patrice Lumumba wa DRC, Lissu ni Kiongozi sahihi kuongoza taifa la Tanzania ila nchi ya Tanzania sio nchi sahihi kwake kupata uongozi.
Wakati Lissu si kiongozi sahihi kwa nchi utakuta wengine wanawaza Samia, Ndejembi, Makonda, Mwigulu, Ridhwani, Abduli, n.k ni viongozi sahihi kwa nchi!
Huyo Lissu anayewa-elimisha WaTanganyika wengi kuhusu umuhimu wa Tanganyika yao hafai kuwa kiongozi wa Tanganyika!
 
Nakubaliana na wewe kwa mengine yote, isipokuwa kusema kuwa YUKO KATIKA NCHI ISIYO SAHIHI, hilo hapana, TUNDU LISSU YUKO KATIKA NCHI SAHIHI SAWASAWA NA KUSUDI LA MUNGU LA KUMLETA DUNIANI...

Mungu muumba hakosei, hajawahi kufanya makosa na hatakuja kufanya makosa milele katika kila afanyalo. Hata wewe kuzaliwa ulikozaliwa na kuwa hapo ulipo, ni si kwa makosa...

Mtu binafsi hajipangii kuwa azaliwe katika nchi fulani. Mungu ndiye aliyepanga kila kitu kwa ajili ya kutimiza kusudi lake..

Kwa taarifa yako na kwa wengine wote wasiojua, ni kuwa;

👉Tundu Lissu alizaliwa Tanganyika ili akabiliane na nyakati kama hizi na watu kama hawa kwa sbb amepewa zana zote za kuwamudu..

👉Tundu Lissu alizaliwa Tanganyika ili kufanya kazi Moja tu - kubadlisha fikra za watu (people's mindset) kutoka kufikiri hivyo wanavyofikiri na kuanza kufikiri tofauti..

👉And as we speak now, he has fully succeeded doing that. Amebadilisha fikra za watu wengi aisee. Wamebaki hawa wanaomuwinda..
================​
Hebu jaribu kufikiri juu ya manabii na mitume mbalimbali waliokuja duniani na kuzaliwa ktk nchi zao walikofanyia kazi zao..

Karibu wote walipitia nyakati ngumu sana katika kujaribu kubadili fikra za watu. Wengine waliteswa na kuuwawa kikatili sana...

Ni mmoja tu aliyekuja na kubadili jumla mwenendo na fikra za watu wa ulimwengu huu, huyo si mwingine bali ni Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai..

Naye alipitia njia ngumu sana ya mateso, kutukanwa, kudharaulika hadi kufa kifo cha aibu cha kutundikwa msalabani hadharani juu ya kilima ili kila mtu amuone na kumdhihaki. Lakini ndio ilikuwa njia ya kuelekea ushindi na ikawa hivyo...

Kusudi lake la kuletwa duniani, ilikuwa ni lazima apitie njia hiyo ya MAUTI YA MATESO NA AIBU na ilikuwa hivyo ili kulitimiza kusudi la kuja kwake..

Tunazaliwa mahali si kwa bahati mbaya. Ni mpango wa Mungu mwenyewe kwa ajili ya kutimiza kusudi hilo..

Tundu Lissu anajua hilo ndio maana hatetereki, haogopi na hayumbi kwa kuwa anajua afanyalo na anamtambua na kumjua aliyemtuma, Mungu Yehova aliye juu..

Tundu Lissu HATAKUFA KIFO CHA KUTAKIWA NA BINADAMU MABARADHULI NA HAYAWANI.

Tundu Lissu ataishi ili dunia ipate kusimulia matendo makuu ya Mungu Yehova aliye hai.

Tundu Lissu ataondoka duniani kwa wakati na kwa njia iliyoamuriwa na BWANA MUNGU YEHOVA muumba wa mbingu na nchi..

MUNGU NA AMBARIKI NA KUMLINDA TUNDU LISSU. Ameeen🙏🙏🙏🙏
 
Napenda nitoe maoni yangu kuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Tundu Lissu. Kwangu namuona kama Kiongozi sahihi, lakini kwa nchi isiyo sahihi.

Nitafafanua kwanini nasema hivyo.

1. Lissu kama Kiongozi sahihi.
Mh. Lissu ni Kiongozi sahihi kwa sababu amejipambanua msimamo wake, tangu awali. Amekuwa mstari wa mbele kupigania haki tangu utawala wa Mkapa, utawala wa Kikwete, utawala wa Magufuli na kwa sasa utawala wa Samiah. Ni viongozi wachache huwa na msimamo usiyoyumba kwa kipindi kirefu cha miaka Zaidi ya ishirini na sita (26). Viongozi wengi huyumba misimamo ila Lissu amekuwa consistent.

Kwanini nasema Lissu ni Kiongozi sahihi?. Lissu amejipambanua kama Kiongozi asiyekata tamaa. Hii nisifa kubwa kwa Kiongozi ya kwamba usikate tamaa hata kama kifo kipo mlangoni Pako.

Kwa mfano, tangu amiminiwe risasi, afukuzwe ubunge, uchaguzi uharibiwe 2020 na Sasa kesi ya uhaini. Hajawahi kukata tamaa. Mwingine kwa zile risasi angekimbia nchi milele na wala asirudi. Au angekubali yaishe Moja kwa Moja akaenda CCM na kujisalimisha ili asiendelee kusumbuliwa.

Pia Lissu sio fisadi. Naamini Lissu angekuwa anajihusisha na ufisadi au biashara, serikali ingeingia kati ili kumlipua mbele ya umma. Hivyo ni Kiongozi msafi na Hana doa sifa ambayo viongozi wengi Tanzania wamekosa.

Hivyo, Lissu anastahili sana kuwa Kiongozi wa Taifa la Tanzania maana amekuwa na msimamo usio yumba, sio fisadi na anahimili changamoto zozote dhidi yake.

2. Nchi isiyo sahihi
Pamoja na Lissu kuwa Kiongozi sahihi lakini changamoto ni kwamba yupo kwenye nchi isiyo sahihi. Naona Tanzania kama nchi isiyo sahihi kwa Lissu kuwa Kiongozi wake.

Kwanza, Tanzania inapenda viongozi wanafiki na waongo. Ukiwa mkweli unakuwa adui wa umma. Sasa Lissu ni mkweli hivyo ukweli wake unachukiza watu wengi wakiwemo viongozi na wananchi kwa ujumla. Kwa mfano, Lissu kasema mfumo wa uchaguzi ni mbovu tangu zamani na kudai kama mfumo hautabadilishwa atakinukisha. Kwa kauli hiyo kapewa kesi ya uhaini.

Pili, Tanzania haina mfumo bora wa uchaguzi. Kutokana na mfumo wetu wa uchaguzi kupata viongozi wazuri ni kazi sana. Mfumo wetu unaruhusu viongozi wenye pesa, Mafisadi, connection, undugu, uccm kupata nafasi za uongozi. Hivyo mtu kama Lissu ambaye sio fisadi, hana connection, sio CCM , hajajilimbikizia mali , mfumo wa uchaguzi wa Tanzania utamptapika.

Tatu, Tanzania ina wananchi ambao hawana interest na mambo ya siasa. Watanzania kwa ujumla wao wana interest na mambo ya dini, mpira na muziki. Hivyo vitu vitatu ndivyo vinapata sana uungwaji mkono Tanzania. Hivyo wengi wanaweza kuona harakati za kisiasa za Lissu hazina maana kwao. Watanzania hawajali kile ambacho Lissu anakipigania maana sio interest yao. Hii ingekuwa tofauti kama Lissu angekuwa Ghana, South Africa, Kenya, Marekani etc,

Nne, Tanzania imemtesa sana Lissu. Tangu aanze harakati za siasa na kupigania haki ni mateso juu ya mateso. Fikiria amepigwa risasi Tanzania, akiwa kwenye matibabu akafukuzwa ubunge, akiwa nje ya bunge hakulipwa stahiki zake, na hata aliporudi kugombea urais alifanyiwa vitimbi ikiwemo uchaguzi wa 2020 kuporwa kabisa. Na kwa Sasa ana kesi ya uhaini ambayo mwisho wa siku akipatikana na hatia atangongwa hadi kufa.

Nihitimishe kwa kusema kama ilivyokuwa kwa Patrice Lumumba wa DRC, Lissu ni Kiongozi sahihi kuongoza taifa la Tanzania ila nchi ya Tanzania sio nchi sahihi kwake kupata uongozi.
Pumbavuuuuu ilio kuu
 
Wanasiasa ni wale wale , angeenda tu kugombea Belgium ..
 
S

Sio lazima uropoke kwa kila thread ya Lissu na upinzani.

Kunyamaza ni hekima pia.
relax,
nafahamu ukweli ulivyo mchungu gentleman,
jifunze kuvumilia na kuuzoea na itapendeza zaidi,
huyo kibaraka anaweza tu kua rais wa jamii niliyoieleza huko alikochumbiwa na wa jinsia yake mwingine 🐒
 
Machoko akili zilishaishia kupigwa miti
 
Back
Top Bottom