Lissu ni Kiongozi sahihi, lakini kwa nchi isiyo sahihi

mnapigana kaba wenyewe kwa wenyewe hadi huruma


hakuna mTanzania anweza kubabaika na porojo za huyo kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi
Ndio maana nikasema aondoke awaachie nchi yenu. Halafu ukiulizwa ni kibaraka wa nani huwezi kusema.
 
Hii ya kuchumbiwa upo serious au ndio hizo ropo zako za kisiasa? Kama sio siasa tueleze alichumbiwa na nani.
Gentleman,
sina sababu hata moja ya kupindisha ukweli ndani au nje ya jukwaa hili la kisiasa.

hayo mengine unaweza kuandika uzi mahususi na hatimae utapata ukweli humo
 
Ndio maana nikasema aondoke awaachie nchi yenu. Halafu ukiulizwa ni kibaraka wa nani huwezi kusema.
aondoke,
asiondoke that's none of Tanzanians business. It's up to himself, na nchi yetu haiwezi kubabaishwa na kibaraka yoyote wa mabwenyenye ya magharibi
 
Very true
 
Kweli kabisa mkuu. Watanganyika ndipo walipofail kabisa.
 
Umeongea maneno mazito mkuu. Ninayaunga mkono kabisa.
 
Lowassa aliletwa na Mbowe, alichofanya Lisu ni collective responsibility. Usichanganye kuwa consistance na kuwa perfect.
Kweli kabisa. Mbowe ndio alimleta Lowassa kwa Njia ya kubadilisha gia angani. Lissu alikubali kuwa na party alliegience na kutekeleza maamuzi ya chama .
 
Wanasiasa ni wale wale , angeenda tu kugombea Belgium ..
Mwanasiasa Gani amewahi kulimwa risasi 16? Ni mwanasiasa gani kafukuzwa ubunge akiwa kwenye matibabu? Ni mwanasiasa gani hii Tanzania alisababisha mtandao kuzimwa kwa wiki nzima tangu siku ya kupigwa kura 2020?

Nimeshangaa Leo unamwita Lissu mwanasiasa wakati Kila mara mnamwita mwanaharakati. Ila ushauri wako ni mzuri. Lissu aombe uraia aende kuishi Ubelgiji, atuachie Tanzania tuendelee kuwashabikia watu wasio julikana.
 
Lissu yupo nchi sahihi
Ila ni wapuuzi wachache wanaoharibu nchi,
Hao Viongozi unaowaita Viongozi wa watu, hakuna watu waliowachagua.
Na kama wapo, ni asilimia 1 katika 100.
Hao wamejiweka wenyewe.
 
Awa ndio Demokrasia Kwao Chadema tu

Ndio wale Samia must go Aleluyaaaaa Samia must go Aleluyaaaaa Samia must go Aleluyaaaaa

Demokrasia kwao inatokea kwa Kiongozi wa kiroho😂
sio kisiasa ✍️
Kwanza punguza udini. Aleluya inakujaje hapo? Mimi sio mtu wa madini yenu. Tafadhali.
 
Sawa, hongera nyie mlizonazo. Tunashuhudia jinsi mnavyoijenga dunia
Bora Lissu atakumbukwa na vizazi vijavyo kama shujaa, sio nyie ambao Makamu wa Rais anafukuzwa kama mbwa mnabakia kucheka tu.
 
Sawasawa. Naona mwenzangu umeshajiandaa: wako watakukumbuka kwa kumuunga mkono lissu anayeungwa mkono na wazungu wanaoupigania ushoga, au sio?
Wazungu Gani hao wanaopigania ushoga wanaomuunga mkono Lissu? Taja hata wawili tu
 
Kama Kiongozi anapimwa kwa kumiminiw risasi basi Mwl. Nyerere na Mzee Nelson Mandela hawakuwa viongozi sahihi.
Wewe wasema. Kila Kiongozi ana historia yake binafsi. Ila kitendo cha kutaka kumuua Lissu kilimaanisha hanunuliki na hayumbishwi.
 
Pombe , dini za kitapeli shuhuda za uongo unafiki, uchawa music, umbea wa mitandaon na wanasanii vichwa maji
Ndo watanzania wanapenda yani mpira wizi, ndo maana kila siku vitu haviendi yani
Wewe ndio unawajua Sasa Watanzania walivyo. Watanzania wanapenda hivyo vitu ulivyotaja sana. Ila waulize bajeti ya mwaka huu inasemaje kuhusu kilimo hawajui au sera ya mambo ya nje kuhusu usalama wa nchi utapata wachache sana wanajua kuhusu hilo.
 
Lissu yupo nchi sahihi
Ila ni wapuuzi wachache wanaoharibu nchi,
Hao Viongozi unaowaita Viongozi wa watu, hakuna watu waliowachagua.
Na kama wapo, ni asilimia 1 katika 100.
Hao wamejiweka wenyewe.
Nimekuelewa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…