Lissu: Nitarejea Tanzania endapo yafuatayo yatafanyika

Lissu kama hutaki kuja wewe baki tu ndugu
 
Hana mchango wowote nchini, kwa kifupi hatumuhitaji.
 
Sioni ni kivipi hayo yote aliyoyataja kama yanatekelezeka!
 
Anatoa masharti kama nani katika nchi hii?
 
Baki Tu huko alipo
 
anadeka utafikiri hatuwezi kuishi bila yeye. tangu aondoke kwenda nje, akatusemea kwa mabepari wakatunyima misaada tukaishi kwa maisha magumuuuuu miaka 6 kwasababu ilipunguza mzunguko wa pesa, sasaivi anafikiri tu namhitaji? kwa sasaivi habari ni mama Samia. Lisu hata asiporudi milele hatuhusu. na kama ana kesi, akirudi azimalizie kwanza.
 
Umri huu nilionao niludi shule nikafanye nini changamoto nilionayo ya kuwasomesha wadogo zako kwangu ni shule tosha kama umenielewa na ujumbe wangu umefika hizo tofauti za r na l si kitu kwangu
Hakika kabsa kama huna lakucomment kaa kimya
 
Lisu ni nani mpaka anaweka masharti ya namna hiyo,anaumuhimu upi kwenye taifa letu mpaka atuwekee masharti?
Akae huko atumtaki hana jipya.
 
Na asirudi kabisa.
Asije akaiharibu jamii kwa mtazamo na sera zake za kuhusudu 'ushoga' na kutoamini kuwa tunaweza kujikwamua kiuchumi na kimaendeleo, hata bila kutegemea hand-outs kutoka mataifa ya kibepari ya nje, au kutapanya raslimali zetu asili kwa mabeberu.
 
ivi lissu hajasikia hotuba ya rais jana bungeni?,mwambieni awai kurudi au atapitwa na vikao vya rais na vyama vya wapinzani.na kama amenogewa na maisha ya ubelgiji akae tu .
 
Hakuna mtego hapo

Lissu thinks he is one of the most important people in the country

And he is not

Awepo , asiwepo hakuna impact
Hiyo ni haki yake anastahili kupewa, alikuwa mbunge mpaka alivyoshambuliwa akalazwa, then Ndugai anamuondoa bungeni kwa utoro wakati anajua fika alikuwa hospital akitibiwa na Rais wa sasa ni shahidi wa hilo, Lissu kulipwa stahiki zake ni haki yake, kama sio shambulio dhidi yake angeendelea kuwa mbunge mpaka muda wake uishe.

Ndio maana nasema mwezi mtukufu huu, Mh. Rais afanyie kazi hili suala ni dogo sana kwake, ndani ya masaa tu anamaliza huo mchezo wote.
 
Amri hizo za Lissu hazitekelezeki kama anataka kurudi arudi na kama hataki abaki huko huko huwezi kumuamrisha Rais achie wafungwa ndio wewe uludi kwani wewe ni nani katika Nchi hii.
Ukomavu n kusimamia haki za wengine akiwemo na yeye,kwa nilivyoelewa,kesi za wafungwa kwa makosa ya kisiasa(kipindi cha kampeni & uchaguzi mkuu),watu wamebambikiwa.
 
Mimi nilikuwa shabiki mkubwa wa Tundu Lissu lakini lazima niseme ukweli ulio moyoni mwangu huyu jamaa amefeli kisiasa kabisa hakuwa na mipango mizuri wala mshauri mzuri., Kwa sababu kama haya anayodai sasa kuhakikishiwa usalama wake ndio aje swali ni mbona uchaguzi alikuja hivyo hivyo kugombea hakujali kuhakikishiwa usalama wala chochote alikuja tu,

Ulipomaliza uchaguzi akadai anataka kuuliwa na mtu aliyemtumia sms akakimbilia ubalozi lakini mbona hakukua na na chochote ule mpango kama ulipita na upepo tu wala hakuna anayezungumza tena sio nje huko aliko wala Tz ni kama vile alijaribu kutaka kutengeneza issue lakini haikuwa na vidhibiti angalau vimuweke katika mazingira mazuri zaidi, alifeli

Umemaliza uchaguzi hakuvumilia ata wiki moja kuonyesha wapiga kura wake kote alikotembelea angalau kuwambia chochote, alienda ubalozi na kutimkia belgium na hata alipofika kule belgum hakuwambia chochote wanachadema ni kama vile alikuja kwa shida ya kusaka urais tu bas ndio iliyokuwa shida yake hakujali wananchi wake., sijuwi alifeli wapi angalau angemsoma maalim seif na vitisho alivyofanyiwa lakini hakuwa mbali na wazanzibari.

Ile kupigwa risasi ilitokea lakini je kwa dunia ilivyoliona lile kweli angepigwa tena marisasi kiongozi aliyetoka kugombea urais?

Huko youtube na twitter anaona ndio jukwaa lake la kisiasa anadhan inatosha? Watanzania wangap hawaelewi twitter wala youtube, jana tumeambiwa watu milioni 8 tu tanzania ndio wanaotumia internet hawa watu wengi waliobaki atawafikia vipi kwa twitter na youtube?

Ndio mana nimesema amefeli sana
 

Mfano asiporudi ss kama taifa tunapata hasara gani?
 
Kwani wewe nani hadi uhoji mtazamo wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…