Lissu: Nitarejea Tanzania endapo yafuatayo yatafanyika

Sasa Lissu hat asiporudi kwani tunakosa Nini
HiviI anajionaje hasa
Mbona anajiona yeye NI Bora Sana kuliko watanzania wengine
 
Sioni ni kivipi hayo yote aliyoyataja kama yanatekelezeka!

..nadhani tatizo ni UZITO wa wahusika waliotaka kumuua TL.

..angekuwa ameshambuliwa na wahuni au vibaka zingefanyika juhudi kubwa kuwakamata ili " kung'arisha " legacy za watu fulani.

..key FACT ktk shambulizi lile ni kuondolewa kwa walinzi ktk eneo aliloshambuliwa TL.

..Wachunguzi wafuatilie mtiririko wa amri ya kuondolewa walinzi wa area D siku ya tukio. Naamini watafika mahali watampata mhusika aliyepanga tukio lile la kinyama.
 

GJ Malisa, BAK n MAg3 wanasemaje?😂😂😂

Mungu anamuumbua Lissu, alisema JPM anamuwinda kaondoka

kwani anaogopa kuuliwa na nani??
 
GJ Malisa, BAK n MAg3 wanasemaje?😂😂😂

Mungu anamuumbua Lissu, alisema JPM anamuwinda kaondoka

kwani anaogopa kuuliwa na nani??

..Nani anaweza kutoa amri walinzi waondolewe area D ili kupisha walenga shabaha wamuue TL?

..Na kwanini mtu huyo anakingiwa kifua mpaka leo?
 
..Nani anaweza kutoa amri walinzi waondolewe area D ili kupisha walenga shabaha wamuue TL?

..Na kwanini mtu huyo anakingiwa kifua mpaka leo?

Uko tayari kuambiwa mshaambiwa mwaka wa tatu sasa tatizo hamuelewi

Hata Lissu anajua ukweli wote kabisa na bado watamtafuta tu

Katika dunia ya forces duniani kuna clean cops na dirty cops

waliotaka kumuu Lissu ni wahuni waku kodiwa tu na baadhi ya viongozi wachafu ambao may be walitaka kujikomba kwa JPM na wakashindwa.JPM angetoa amri ya kuuawa yule asingepona...unless haujui capability ya polisi, TISS na jeshi letu...dont think too low kwa emotion

mbona samia nae ashawahi kusema hapa??



JPM anaweza kulaumiwa kukilea hiki kikundi na kutotaka kuchukua hatua, ila hakuna presidential order Lissu auawe, it was bad timing, na nani anaua vile? hakuna snipper?

Kuwa eti cctv ziliondolewa ni utoto sana kwa TZ ambako bado unaweza kwenda kagera ukajifanya daktari na ukapokelewa!!!

wewe unaona Tanzania tuna ulinzi wa maaba kwenye facilities zetu?

why JPM hakuchukua hatua??? hii iko kwa Lossu sasa na tabia zake za ajabu,alipopigwa tu risasi mkasema JPM hapo hapi sio? sasa mlitaka afanye nini tena na mtu alikuwa mbishi vile!!!!?

Tuache hii maada
lissu arudi tu sasa aache mashart

Na kama assumption ya dirty copy haiko sahihi, basi kuna third part, wanamsubiri...yeye anajua hilo, kuwa Lissu hana kabisa maadui wengine wa kutaka kumuua? mwanasheria? think

Mimi naishia hapa mkuu

Revisit your fact taratibu sio kwa muono wa wengi, watu wanakufa kwa risasi moja na sio 16....there was so many technique za kumuua mtu na sio mchana risasi 16..wauaji walitaka sifa kwa nani??? serikali inataka sifa?

Lissu akaenda hospitali, kisha ikulu ikaruhusu aende nairobi sio??😂😂😂😂
 
Kama unaona mazingira sasa ni bora kwako kuishi tz, basi urudi tu, hamna wa kumpa masharti, na siamini kama kunamtu unawasiliana nae hatimize hayo masharti. Kama hali imerejea kuwa shwari njoo, kama haujiamini basi endelea kukaa huko!
 

..maelezo yako ni very thoughful.

..tukio lolote linalofanywa na wanadamu lina chances fulani za ku-fail.

..huwezi kuchukulia kufeli kwa tukio lile kama kigezo cha ku-rule out au kuwahusisha watu fulani fulani.

..hujawahi kusikia daktari mahiri bingwa anayesifika aliyeokoa magonjwa wa kila aina akafanya kosa lisilotarajiwa ktk kazi yake?

..hujawahi kusikia taasisi kubwa mahiri duniani kwa ufanisi zimefanya makosa ktk shughuli zake?

..maelezo ya Mama Samia yalilenga hadhira aliyokuwa akizungumza nayo. Mimi na wewe tuna uwezo wa kufikiria na kuchambua kwa mapana na marefu zaidi.

..waliohusika na tukio lile wanasutwa na FACT moja ndogo, lakini muhimu sana.

..Ni nani aliondoa walinzi wa area D? Alitumwa na nani? Kwanini anakingiwa kifua?

NB.

..kuhusu ndege kuruhusiwa kwenda Nairobi, walijua ule ni mzoga utawafia njiani, lakini MUNGU aliamua vingine.

Cc Mmawia
 
We baki huko huko,maana nchi kama nchi haikuitajii kiivyo
 
yaani unatoa na masharti unadhani Samia ni mkeo?

kwa hio yasipotimia unazira kurudi Tanzania tukome kabisa?
 
Acha upumbavu wako. Huyo ni mtu anatejijua na siyo mjinga kama wewe ambaye unaweza kugeuzwa upande wowote kwa sababu unadhani wewe siyo chochote.
 
Lissu anaongea kama mtu aliyeshika switch ya tanesco, kwamba akishindwa kurudi anazima umeme nchi nzima
Kuna watu wajinga sana. Na wewe ni mmoja wapo. Unadhani mpaka uwe na uwezo wa kumfanyia mtu jambo fulani ndiyo utadai haki zako? Ndiyo maana mnagezwa kama nyumbu kwa sababu mnadhani hamna cha kuwafanya wanaowageuza.
 
Urudi kuijenga nchi yetu, ndugu yetu Lissu, Mama Samia hataki dhuruma na matendo yeyote ya kukanyaga demokrasia, zaidi anawahitaji sana great thinkers of your nature. Nilitamani uwepo ktk kikao na wapinzani ambacho amekisema ktk hotuba yake.
 
Aweke risiti tuzione.
 
Lisu ni nani mpaka anaweka masharti ya namna hiyo,anaumuhimu upi kwenye taifa letu mpaka atuwekee masharti?
Akae huko atumtaki hana jipya.
Kamuulize dereva aliyetumbukia mtaroni na roli, anaujua mchakamchaka aliomkimbiza kikamanda nyakati za kampeni.
 
Hata shujaa alikua kwenye dozi ya Lithium au umesahau alikua na bipolar ?
 
Ukomavu n kusimamia haki za wengine akiwemo na yeye,kwa nilivyoelewa,kesi za wafungwa kwa makosa ya kisiasa(kipindi cha kampeni & uchaguzi mkuu),watu wamebambikiwa.
Tatizo Lissu anaamrisha kuwa yafanywe hayo yasipofanywa yeye haludi ndio tunapojiuliza yeye ni nani mpaka atoe amri kama hiyo?

Rais Samia mpaka sasa ameshaonyesha kutaka maridhiano na ndio maana yupo tayari kukaa na viongozi wa vyama vya upinzani na kutatua baadhi ya kero ili Nchi ifanye siasa za kistaarabu tofauti na utawala uliopita

Sasa yeye anapoibuka huko alipo na kutoa masharti yake kwa Rais maana yake nini? Amwache Mheshimiwa kwanza afanye mambo yake pale tutakapomuona Mheshimiwa anakosea ndio aanze kubwabwaja ila kwa sasa ni kama anatupigia kelele na kutaka kumtoa Mama kwenye njia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…