Lissu: Rais Magufuli haonekani kanisani wala mitaani, Msemaji wa Serikali atujuze

Lissu: Rais Magufuli haonekani kanisani wala mitaani, Msemaji wa Serikali atujuze

Miaka ya nyuma kabla ya mitandao rais unaweza usimuone kwenye magazeti wala akihutubia kwa miezi kabisa
 
Lissu ale bata tu huko majuu.
Mambo ya bongo hayamhusu.

Mzee JPM kaamua kusali ndani kwake kwani kuna tatizo?
Padre we!
 
Kwani ni lazima tujue kila mahali alipo?
We jamaa tunamzungumzia Rais wa nchi hana siri na mambo yake huyu tunamlipia kodi ale avae aline atibiwe asafiri why tusijue aliko au hulipi kodi wewe
 
Umekwenda kazini kwake ukamkosa?

Umekwenda nyumbani kwake ukamkosa?

Umempigia simu hajapokea?

Acha ushamba. Deal na mambo yako.

Unauliza eti Rais yuko wapi, anakuhusu nini wewe?

Ukijua alipo utakuwa umepata faida gani?
 
Huyu tayari kashasusa kwenda kanisani katoliki kisa wanatofautiana naye kwenye Corona, mzee wa visirani katika ubora wake, ataanza kusali kwa Gwajima.
 
Punguza mihemko lakini ujifunze kutafakarisha ubongo.

Kwanza si rahisi mtu ku tweet bila sababu na ndio maana hata ukifuatilia wachangiaji wanajihoji nini kipo nyuma labda tusichokifahamu ambacho kimemfanya muhusika kuandika hivyo na hicho ndicho watu wanahitaji kukijua.

Tutumie ubongo kujifikirisha kuliko kukumbatia mapungufu ya wengine.
 
Huyu tayari kashasusa kwenda kanisani katoliki kisa wanatofautiana naye kwenye Corona, mzee wa visirani katika ubora wake, ataanza kusali kwa Gwajima.
Anaingia popote Rais, iwe Katoliki, kwa Mwamposa, kwa Gwaji na hata Msikitini.
Ila kabadili style tuu
 
Huyu tayari kashasusa kwenda kanisani katoliki kisa wanatofautiana naye kwenye Corona, mzee wa visirani katika ubora wake, ataanza kusali kwa Gwajima.
Kwani Gwajima bado anaendelea na ibada zake?

Vipi waumini wanafika ama wananchi tu wajimbon kwake.
 
Liso keshakuwa Ni mpumbavu na mpayukaji asiye Maana!!

Kwani ni Lazima kila wiki mtu uende kanisani??
Hizo sala za kuishinda corona unafanyia chumbani peke ako.

Kwa hiyo yeye anasisitiza nini naye anafanya nini.

Always lead by example.
 
Thanks Tundulisu kwa Taarifa.
 
Maaskofu wanataka waumini wao wazingatie kuwa kuna corona wachukue tahadhari.
Basi rais akiwa muumini wa kanisa hili ameamua achukue tahadhari kwa kumuomba Mungu wake bila kwenda kanisani.
Bila barakoa huingii kanisani. Na jamaa etu hataki kabisa hizi mambo.

Yupo fit anapitia mafaili..na kumtrain katibu mkuu kiongozi.
 
Nyungu muhimbili ni 5000 unapigwa na nguo zako ukitoka unaendelea na maisha yako.
Akina mbunge msukuma yao wanafanya bure.

Yaani serikali yetu bana. Hadi kujifukiza mamoshi na mamvuke tu utoe buku 5.

Kazi tunayo. Hii wangefanya bure tu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Lissu keshakuwa beberu mdogo!! Hana manufaa kwa Taifa letu!! Ninamhurumia kwa yaliyompata lakini asiposamehe atathirika mwenyewe!!
 
Kosa langu nini? Kosa la Lissu nini?
Atuambie yeye inaelekea anajua kitu fulani. Atakuwa mshitakiwa wa kwanza kama ikidhihirika kuna madhara yoyote! Anataka ajue alipo Rais wetu kwani anataka kumfanyia nini?? Hii kauli ya Lisu ichunguzwe wala isipuuzwe!
 
Asipo kuelewa piga kofi
Mtanzania ni vigumu kumwekea dhamana. Usilogwe ukamlia yamini. Imekula kwako. Uelewa unawapiga chenga. Tena mambo ya msingi sana. Leo ukimuuliza hizi picha za rais kanisani .za nini? Atakujibu kuwa ni kwa sababu ni rais. Kesho ukimuuliza mbona Jumapili hii hajaonyeshwa kasali kanisa gani? Jibu atalotoa ni kuwa masuala ya kwenda ibada ni mambo binafsi. Mambo ya mtu na Mungu wake( Rebecca akisikitika)?

Amesahau kabisa aliyosema Jumapili iliyopita. Rais anatoa bulungutu la kekundu. Apandaye sana anavuna sana. Sharti ni kama mbegu ilikuwa yake. Ikiwa yale mabulungutu yanatoka hazina yetu na si mfukoni kwake, ameumia. Mchungaji gani hapendi hizo nyekundu?

Wako tayari kumwachia madhabahu ilmradi bulungutu limebaki kanisani. Hata akiwananga. Tusi lenyewe halivunji mfupa. Tunamiss mahubiri ya Makonda! Rais alimwambia Chakwera: I can preach like you but I cannot reach you. Chezea phd wewe?
 
Daah hatari kweli aisee na hii ishu tuliopo ndani hatuwezi kuuliza maana unaona kila kukicha Dr Abbas akisisitiza kutotoa taarifa hovyo za Serikali...mimi mwenyewe siulizi nauliza gemu ya maarabu na Vita iliishaje?
 
Back
Top Bottom