Lissu: Rais Samia akiniteua katika Serikali yake atakuwa hanipendi

Mmmh yuko sure atakataa🤣🤣🤣
teuzi ni level nyingine my friend.

Mama Samia natamani sana awape vyeo tuone utendaji wenu.
Utendaji wa WanaCHADEMA chini ya Rais wa CCM?
 
Unajuaje ndani ya moyo wake,je siku akipewa teuzi akakubali utafuta hii comment?
Wanasiasa usiwaamini sana.
Hata Samia hawezi kufikiria hilo; amteue Lissu katika serikali yake? Hajipendi?
 
Kitila Mkumbo alimshauri Hayati Dr Magufuli aache kuteua Wana taaluma wa Vyuo vikuu ili wabaki kufundisha vyuoni…alipoteuliwa Yeye akitokea Udsm akashukuru sana na hata zile tuhuma zake za kufoji cheti Makonda zikaisha
Acha kumlinganisha Lissu na watu waliofika bei!
 
Pole. Chama kinapendekeza, rais anateua na kuapisha. Na hoja yake TL ni kuzibwa mdomo na si uteuzi endapo umesoma vizuri maudhui.
Shuleni ulisomea ujinga? Rais ana- endorse matakwa ya chama na kama hataki atatoa sababu ambazo lazima zikubaliwe na chama vinginevyo kutakuwa na mgogoro wa kikatiba.
 
Shujaa ni anaepambana ndani ya jeshi

Ukiwa nje kuitwa muasi ni rahisi
Siyo kweli ukiwa ndani ndio muasi, na kumbuka kiapo Cha mawaziri sitatoa Siri za baraza la mawaziri. Au mfano mzuri ni Mrema alipotimuliwa na Mzee Mwinyi kabla ya kutimkia NCCR.
 
Wewe Tundu Lissu hufai, unaropoka ropoka tu. Suala la Ngorongoro unalichukulia juu juu. Kumbe hata urais ulikuwa hufai, nafuu ulishindwa maana nchi ingeongozwa mtu wa ajabu ajabu yaani haelewi hata mambo ya UNESCO, yaani unataka Ngorongoro iharibike, kwani wamasai wakienda Longido au Karatu kuna shida gani? Hatungeweza kuwa na rais wa ovyo kama Lissu, ana mawazo mabovu ya ki-activitism. Hafai Lissu, bora Mbowe.
 
Angekuwa anazihitaji angezipata siku nyingi!
Mtazamo dhaifu mno kutoka Kwa naibu waziri mstaafu! Haiyumkini ulizaliwa ili uwe mtumwa na mtwana! Endelea kujipendekeza na sahau teuzi!
 
Tena Lissu ni maarufu kuliko hata PM
 
Wewe dada una matatizo makubwa sn
 
Ss kama hawatak kuingia serikalin wanagombeaga kiti cha urais cha nn kama wanafurahia kuendelea kuwa upinzan
Kauli za lissu na mbowe hv karibn zinafikirisha
 
Tamko hilo linaweza kuwa na pande mbili. Upande mmoja unaweza kuwa unamwonyesha kama mtu asiyeweza kushawishi kwa kujenga hoja bali anataka kupambana tu. mtu akiwa ndani ya system an uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo fulani yatekelzwe kuliko aliye nje.

Upande wa pili unaweza kumwonyesha kama mtu anyetaka naye afikiriwe na mama kwenye nafasi za kuteuliwa ila anaanza kwa kusema sizitaki mbichi hizi.

Msingi mmoja wa busara ni kutokujibu maswali hypothetical.
 
Shuleni ulisomea ujinga? Rais ana- endorse matakwa ya chama na kama hataki atatoa sababu ambazo lazima zikubaliwe na chama vinginevyo kutakuwa na mgogoro wa kikatiba.
Naamini wewe ni mstaarabu haufanani kabisa na wenye kutukana hata kama umesoma kuwazidi. Naheshimu maoni yako na utu wako hata kama tunatofautiana.

Aidha, najua kuwa hakuna anayesomea ujinga na kusoma sana si kuelewa kila kiu! Hongera uliyesoma, ila mimi bado najifunza na kamwe sitahitimu elimu ya maisha - naendelea kujifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…