We sio wa level yake hivyo weka makalio chini subiri upewe chochote.Ukisikia hivi ujue anaomba kazi kiujanja..."mbwa akiona chatu hukunja mkia huku anamfuata akilia"
Hili jiwe limekugonga ukiwa wapi?Wewe Tundu Lissu hufai, unaropoka ropoka tu. Suala la Ngorongoro unalichukulia juu juu. Kumbe hata urais ulikuwa hufai, nafuu ulishindwa maana nchi ingeongozwa mtu wa ajabu ajabu yaani haelewi hata mambo ya UNESCO, yaani unataka Ngorongoro iharibike, kwani wamasai wakienda Longido au Karatu kuna shida gani? Hatungeweza kuwa na rais wa ovyo kama Lissu, ana mawazo mabovu ya ki-activitism. Hafai Lissu, bora Mbowe.
Unataka wapambane vipi mkuu, si unaona badala ya kupambana na CCM wanapambana na polisi? Watapitia wapi hadi wawafikie CCM wakati kuna mitutu ya bunduki na jela na mahakama, n.k., wanavyotakiwa kupambana navyo kabla ya kuwafikia CCM ili wapambane nao ana kwa ana. Au wewe huko uliko huyaoni hayo mkuu?Thank you.
Ni vile hakuna chama kinachoweza kupambana na CCM,vilivyopo vimeunga mkono juhudi.
Na ukitazama sana utatambua yajayo yanafurahisha.
EeenHeee. Una maana mama ana hati miliki au siyo?Kwanza kabisa mama anatakiwa awatrain aone utendaji kazi kama watafaa awaruhusu kwenda chama chao.
Kwahiyo anahalalisha hawa walioko serikalini kutowasemea wananchi kwa kumuogopa aliyewateua!Akihojiwa na mtangazaji wa Star Tv bwana Odemba, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh. Tundu Lissu amesema endapo Rais Samia atamteua kushika nafasi yoyote katika serikali basi atajua kuwa hampendi.
Kwa kifupi Tundu Lissu amesema hawezi kukubali uteuzi wowote ndani ya serikali kwa sababu atakuwa amezibwa mdomo kwa kutoa mawazo mbadala. Amesema yeye hawezi kuwa ndani ya serikali ili abaki huru kusema mazuri na mabaya ya serikali!
Akihojiwa na mtangazaji wa Star Tv bwana Odemba, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mh. Tundu Lissu amesema endapo Rais Samia atamteua kushika nafasi yoyote katika serikali basi atajua kuwa hampendi.
Kwa kifupi Tundu Lissu amesema hawezi kukubali uteuzi wowote ndani ya serikali kwa sababu atakuwa amezibwa mdomo kwa kutoa mawazo mbadala. Amesema yeye hawezi kuwa ndani ya serikali ili abaki huru kusema mazuri na mabaya ya serikali!
Huo ndiyo ukweli waliyopo serikalini wanamuogopa aliyewateua.Kwahiyo anahalalisha hawa walioko serikalini kutowasemea wananchi kwa kumuogopa aliyewateua!
Lakini pia ni kwamba naye anatuambia Hajiamini au ni mwenye kuyumbishwa msimamo kwa hofu ya mteule wake?
Na, je ndio kusema yeye anastahili tu kuwa Mteuzi wa wengine na si nafasi nyingine? Aje kama chama chake kitashika dola na mgombea asiwe yeye?
Kwani anashindwa kufanya kazi yake ya uwakili vizuri? Unataka kumlinganisha Lissu na hawa majaji wa michongo, wee vipi?Ana ubongo uliosheheni criticisms bila practical solutions to problems. Ni mtu bure kabisa! Kama hawezi kuonesha umahiri wake wa uongozi kwa vitendo, si bora anyamaze awaache wenzake wafanye kazi?
Kwani anashindwa kufanya kazi yake ya uwakili vizuri? Unataka kumlinganisha Lissu na hawa majaji wa michongo, wee vipi?
Nimesoma hoja yako! Uwezo wa Lissu usipime na wala usimlinganishe na vilaza walioko serikalini!
Hao ni wale waliojaa majalalani huko kwenu kijaniUkisikia hivi ujue anaomba kazi kiujanja..."mbwa akiona chatu hukunja mkia huku anamfuata akilia"
Sasa sijui angeshinda urais na kuwa rais ni angepata wapi nafasi ya kukosoa.Huyu lisu niliwai mskia akisema yeye ni born rebel,
Hata chadema ikiingia ikulu anahis hata enjoy tena itabd ahamie upinzni tena ili aweze kukosoa..
Au alivyopambana Zitto chadema.Kupambana ndani ya jeshi ni kama alivyopambana Ndugai.
Ni kweli kabisa, wanahitajika watu kama akina Prof Assad wengi ambao hufanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya kazi bila kuteteleka.Mtu anayekuteua ni udhihirisho wa kukupenda. Asingempenda asingemtembelea Nairobi na kukutana naye Ubelgiji. TL angesema hawezi kufanya kazi chini ya mifumo mibovu ya serikali pasipo mabadiliko au katiba mpya!
Hata hivyo, aliyeko serikalini hazuiwi kukosoa mabaya na kupongeza mazuri. Akubali kuteuliwa pasipo kuacha misimamo yake ya kutetea haki na kuinyoosha serikali.
Ndivyo alivyo Othman Masoud na ndivyo alivyokuwa Maalim Seif.