Lissu: Sheria na Tamaduni za kitanzania haziungi mkono mapenzi ya jinsia moja, mimi pia siungi mkono jambo hilo

Lissu: Sheria na Tamaduni za kitanzania haziungi mkono mapenzi ya jinsia moja, mimi pia siungi mkono jambo hilo

Lissu ameyasema hayo baada ya kuulizwa swali kwenye kipindi cha Clouds 360 ambapo mtangazaji alimuuliza Lissu yupo upande gani sababu mahasimu wake wa kisiasa wamekuwa wakimtuhumu kuwa supporter wa mapenzi ya jinsia moja kwakuwa anakaa ulaya.

Lissu amesema hizo ni siasa za maji taka na kwamba hajawahi kusema popote kuwa anaunga mkono mapenzi ya jinsia moja.

Anasema jambo hili liliibuliwa alipojibu swali kwenye kipindi cha Hard Talk BBC ambapo alisema mambo ya faragha serikali haitakiwi kuingilia na kwamba nchi ina katiba inayosema serikali hairuhusiwi chumbani.

Akielezea msimamo wake juu ya jambo hili Lissu amesema, "Watu wenye utamaduni huo waendelee na utamaduni wao, sisi wenye utamaduni tofauti tuendelee na utamaduni wetu, sheria na tamaduni zetu haziruhusu ushoga hivyo tuendelee na utamaduni wetu, siungi mkono ushoga."

View attachment 2504788
Amejibu ili mradi na ashawaambia ntajibu wanavyotaka kuwazuga watz
 
Ni kweli amejibu kwa umakini mkubwa na nadhani alichosema hakina tofauti na alichowahi kusema huko nyuma.

Kama Mkatoliki na pia Mwanasheria mahiri najua alichokifanya hapa.
Lissu is so bright
 
Alipokua huko kwao alisema vile, na amerudi hapa kwetu amesema hivi.
Nikama anacheza na wakati na hii ndio maana halisi ya siasa...😂
Mleta mada, kathibitisha Kwa kuweka video na sauti ya Tundu Lissu mwenyewe..

Na wewe thibitisha Kwa kuweka video au hata sauti basi ya Tundu Lissu akisema hivyo kuwa anaunga mkono mapenzi ya jinsia moja..

Vinginevyo, NYAMAZA KIMYA na acha uzushi na uongo usio kuwa na uthibitisho!!!
 
Punguza makasiriko mkuu...🤣
 
Back
Top Bottom