Pre GE2025 Lissu: Sijui ilikuwaje CHADEMA tukamualika Rais Samia, ila mbeleni tutaelezana

Pre GE2025 Lissu: Sijui ilikuwaje CHADEMA tukamualika Rais Samia, ila mbeleni tutaelezana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema

Kunielewa hebu turudi kidogo nyuma kipindi cha Magufuli mambo yalivyokuwa

Kipindi cha Magufuli, siasa za CCM vs Chadema, zilikuwa ni siasa extreme sana, CCM na Chadema ilikuwa kama makundi ya Wahutu na Watusti kule Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari

Kuna kipindi Wabunge wa CCM walipewa onyo kali kumtembelea mbunge mwenzao Lema gerezani alipowekwa rumande kwa miezi kadhaa
Wabunge wa CCM wakapigwa marufuku kumtembelea Lissu hospitalini alipopigwa risasi, na Lazaro Nyalandu mbunge pekee wa CCM aliyemtembelea Lissu aliingia matatizoni na chama chake kwa kufanya jambo hilo hadi ikambidi kuhama

Wananchi nao wakaambiwa waziwazi hawatatatuliwa shida zao kwa sababu walichagua wabunge wa upinzani
Bado kulikuwa na visa vingi vya kesi za kisiasa, kutekwa, mauaji hadi wapinzani akiwemo Lissu na Lema kukimbia nchi.

Fast Forward leo hii, Rais Samia pamoja na mapungufu yake ameondoa siasa hizo za extremism
Samia ameweka mbele kuwa sisi wote ni Watanzania kwanza kabla ya kuwa CCM ama Upinzani
Ndio maana hata Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema akahudhuria, alikutana na viongozi wa Chadema, kufuta kesi, waliokuwa wamekimbia wakaambiwa warudi, mikutano imeruhusiwa na mengine mengi

Sasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema
Anasema pia anakusudia kumshtaki Samia kwa kuweka picha aliyopiga na viongozi wa Chadema kwenye bango

Hizi siasa za kuonana maadui kutokana tu na tofauti ya vyama vyetu tukirudi tena huko waathirika wakubwa ni Chadema, sio CCM, actually kundi kubwa la CCM linatamani turudi huko kwa sababu wao wanaweza kufanya lolote kwa upinzani bila kufanywa chochote kama tulivyoona kipindi cha Magufuli

Ni muda sasa viongozi wa Chadema wakamuonya Tundu Lissu
CCM na Chadema ni kama Yesu na Shetani
 
Akiwa mkoani Iringa katika mkutano wa hadhara Lissu amesema hajui ilikuwaje CHADEMA ikamualika mama kwenye mkutano wa CHADEMA maana huwa hawaji wenyewe ni mpaka waalikwe.

Aidha Lissu amewatahadharisha wanaCHADEMA kuwa makini maana kwenye uchaguzi wa ndani ya Chama kuna hela nyingi inatumika ambapo Lissu amesema fedha hiyo ni ya Abdul na Mama yake maana chadema hawana hela hata kufanya mikutano huwa inakuwaga ni shida kwasababu ya fedha ila cha ajabu watu wanapewa fedha kwenye uchaguzi wa ndani.

Lissu ameamua kufanya swala la Uchaguzi wa ndani wa CHADEMA kuwa swala la Umma.
Tanzania kuna vituko kweli. Sasa hapo chuki ziko wapi? Usishangae wakikutana wanakunywa chai pamoja. Kwa nchi zingine za Africa siasa anafanya lissu ndo siasa yao. Zoeeni siasa ya aina ya lissu. Siasa za kubembelezana zimeshaisha.
 
Yuko sahihi ile ilikuwa n kujipendekeza tu kwa samia, hakuna ccm yeyote mpk huyo mzanzibar hakuna anayewapenda chadema, we unampendaje mtu aliyedhamilia kukutoa madarakani. Ccm wapo tyr hata leo viongoz wote wa chadema wauawe if possible so yuko sawa.
Ni kwa ajili ya kujenga taifa sio kwa ajili ya hilo lichama lenu.

Samia hahitaji kujipendekeza kwa Chadema ambao hawana hata mbunge mmoja na waliokuwa wamejifia na kukimbia nchi
 
Wewe unapenda Yesu na Shetani washirikiane?🐼
Shetani hakwenda kwa Mungu kujadiliana naye mambo ya Ayubu??

Hivi devo hakupiga stori na jizaz kule mlimani kumshawishi ageuze jiwe liwe mkate!?

Ushasahau mara hii kuwa Bi Mkubwa Hawa kabla ya kula tunda la mti wa kati ya bustani alikuwa anapiga stori na Devo wakati Mzee mzima Adam anakata mitaa?

Kama Ayatollah Khamenei anawasiliana na Marekani ndiyo itakuwa Mbowe na Samia!??
 
Jalalani ni nyumbani kwa wendawazimu!!!

1. Jamii yoyote yenye kubagaza wasomi wake ni jamii ya ki wenda wazimu.

Ule Moto wa nyika wa migomo Marekani, wapindukia Canada!

2. Wasomi ni tunu na ndiyo pekee watakao tukomboa!

3. Wajinga, wapumbavu wenye macho kwenye maokoto, ubunge na udiwani ni Laana!

Migomo vyuo vikuu imeangusha serikali; Marekani siyo kisiwa, la sasa halimwachi salama!

4. Haipo shaka, Proved, Zawadini Lissu ana wakati mgumu sana Chadema.

5. Lissu huru asingeacha kumpa Biden vidonge vyake lakini siyo hizi mbuzi zingine!
 
Shetani hakwenda kwa Mungu kujadiliana naye mambo ya Ayubu??

Hivi devo hakupiga stori na jizaz kule mlimani kumshawishi ageuze jiwe liwe mkate!?

Ushasahau mara hii kuwa Bi Mkubwa Hawa kabla ya kula tunda la mti wa kati ya bustani alikuwa anapiga stori na Devo wakati Mzee mzima Adam anakata mitaa?

Kama Ayatollah Khamenei anawasiliana na Marekani ndiyo itakuwa Mbowe na Samia!??
Basi mshaurini Lisu awe muelewa
 
Aisee sikujua Tundu Lissu ana chuki hivi hadi awamu hii ya Samia....Kwa hiyo Samia kualikwa kwenye mkutano wa Chadema kuna na akahudhuria ameona ni shida kubwa, anataka zile siasa za Kihutu na Kitutsi na sio siasa za kuona CCM na Chadema wote ni watanzania
Haya mambo tuliyaonja kidogo kipindi cha Magufuli na Lissu alikuwa mhanga, ila ndio anayatamani?
Lakini pia hiki ni kitu cha ajabu kidogo ni sawa na Simba wawaalike Yanga kwenye mkutano wao mkuu unajadili jinsi ya kuchukua ubingwa.
 
Sisi tunajua Mbowe ni serikali, na fedha kapewa na Samia..... Lissu maswali gani haya?
 
Lakini pia hiki ni kitu cha ajabu kidogo ni sawa na Simba wawaalike Yanga kwenye mkutano wao mkuu unajadili jinsi ya kuchukua ubingwa.
Kwani Samia alialikwa kwenye mkutano gani wa kimkakati ndani ya CHADEMA?

Maana naona wapotoshaji mnaipeleka mada kusiko!!
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Wenyewe huwa wanaona wanatetea "status quo" kumbe siyo Kila wakati ni wa vita.

Hapa Iringa kuna Siasa zinageuzwa za kitaifa kumbe ni za kwetu sisi wenyewe wanyalukolo.

Mwembetogwa mara kadhaa imetumika kuharibu urari wa Siasa za Iringa.

Hapo alilengwa Msigwa ambaye wapinzani wake ndiyo wanamtuhumu kutumia Hela za mama Abdullah.

Ukiwaambia walete ushahidi HAWANA.
 
Aisee sikujua Tundu Lissu ana chuki hivi hadi awamu hii ya Samia....Kwa hiyo Samia kualikwa kwenye mkutano wa Chadema kuna na akahudhuria ameona ni shida kubwa, anataka zile siasa za Kihutu na Kitutsi na sio siasa za kuona CCM na Chadema wote ni watanzania
Haya mambo tuliyaonja kidogo kipindi cha Magufuli na Lissu alikuwa mhanga, ila ndio anayatamani?
Niliandika kuwa waTanzania sio watu wa kuongozwa ni watu tuliozea kutawalia iwe na mkolni au machifu ,tukiaachiwa huru tutahadaika na kiza na ndio ukaona baadhi ya wanasiasa wanaharisha njiani.
 
Back
Top Bottom