Pre GE2025 Lissu: Sijui ilikuwaje CHADEMA tukamualika Rais Samia, ila mbeleni tutaelezana

Pre GE2025 Lissu: Sijui ilikuwaje CHADEMA tukamualika Rais Samia, ila mbeleni tutaelezana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Machadema kipindi kile yalifikiri yanafanya vile ili kumkomoa marehemu. Lakini sasa mambo ni tofauti!

Kwanza maccm yakatumia ile kama gia ya kuuza bandari zetu.

Yani maccm yalichekelea sana kuona machadema yajipeleka yenyewe kibra
 
Sasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema

Kunielewa hebu turudi kidogo nyuma kipindi cha Magufuli mambo yalivyokuwa

Kipindi cha Magufuli, siasa za CCM vs Chadema, zilikuwa ni siasa extreme sana, CCM na Chadema ilikuwa kama makundi ya Wahutu na Watusti kule Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari

Kuna kipindi Wabunge wa CCM walipewa onyo kali kumtembelea mbunge mwenzao Lema gerezani alipowekwa rumande kwa miezi kadhaa
Wabunge wa CCM wakapigwa marufuku kumtembelea Lissu hospitalini alipopigwa risasi, na Lazaro Nyalandu mbunge pekee wa CCM aliyemtembelea Lissu aliingia matatizoni na chama chake kwa kufanya jambo hilo hadi ikambidi kuhama

Wananchi nao wakaambiwa waziwazi hawatatatuliwa shida zao kwa sababu walichagua wabunge wa upinzani
Bado kulikuwa na visa vingi vya kesi za kisiasa, kutekwa, mauaji hadi wapinzani akiwemo Lissu na Lema kukimbia nchi.

Fast Forward leo hii, Rais Samia pamoja na mapungufu yake ameondoa siasa hizo za extremism
Samia ameweka mbele kuwa sisi wote ni Watanzania kwanza kabla ya kuwa CCM ama Upinzani
Ndio maana hata Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema akahudhuria, alikutana na viongozi wa Chadema, kufuta kesi, waliokuwa wamekimbia wakaambiwa warudi, mikutano imeruhusiwa na mengine mengi

Sasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema
Anasema pia anakusudia kumshtaki Samia kwa kuweka picha aliyopiga na viongozi wa Chadema kwenye bango

Hizi siasa za kuonana maadui kutokana tu na tofauti ya vyama vyetu tukirudi tena huko waathirika wakubwa ni Chadema, sio CCM, actually kundi kubwa la CCM linatamani turudi huko kwa sababu wao wanaweza kufanya lolote kwa upinzani bila kufanywa chochote kama tulivyoona kipindi cha Magufuli

Ni muda sasa viongozi wa Chadema wakamuonya Tundu Lissu
Mkuu it's better turudi huko kuliko kupeana ahadi hewani. Kuumia ni sehemu ya maisha. Huu unaoitwa uungwana hauna maana kama madai ya msingi hayatekelezwi.
 
..mtaruhusu ushoga muda si mrefu.

..hamjasikia kuna anayetuhumiwa usagaji na ana madaraka makubwa?
Hicho chama chenu kitaendelea kuonekana kama kikundi cha wahuni tu kama watu wenyewe ndio ninyi
 
Mkuu it's better turudi huko kuliko kupeana ahadi hewani. Kuumia ni sehemu ya maisha. Huu unaoitwa uungwana hauna maana kama madai ya msingi hayatekelezwi.
Anachokihubiri Tund Lissu ndio wafuasi wa Magufuli wanakitaka, sababu wanajua siasa hizo zinawafanya waweze kuwafanyia wapinzani kitu chochote na wasifanywe chochote

Actually ukichunguza kwa makini utaona mashabiki wa mwendazake wanamshangilia Tundu Lissu japokuwa hawampendi, wanajua atawapa wanachotaka
 
..kingekuwa ni kikundi cha wahuni msingekiandama kiasi hiki?
Nadhani wafuasi wa Chadema mnachokosea mnadhani kila anayeikosoa Chadema ni mfuasi wa CCM anayetaka upinzani ufe, wengine hatuna hata vyama, bali tunataka nchi yenye siasa safi za kujenga

Kwa siasa zenu hizi za kudandia na kushabikia wapuuzi kama akina Mange na Kigogo mna safafi ndefu sana ya kuaminiwa kama watu serious mnaoweza kuongoza nchi
 
Anachokihubiri Tund Lissu ndio wafuasi wa Magufuli wanakitaka, sababu wanajua siasa hizo zinawafanya waweze kuwafanyia wapinzani kitu chochote na wasifanywe chochote

Actually ukichunguza kwa makini utaona mashabiki wa mwendazake wanamshangilia Tundu Lissu japokuwa hawampendi, wanajua atawapa wanachotaka

..hatupaswi kurudi kwenye utekaji na mauaji.

..tunatakiwa tuweke mfumo wa haki ktk siasa na chaguzi zetu.

..Rais Samia amepiga chenga hoja ya Tume Huru, na Katiba Mpya.

..Chadema wana haki ya kumlaumu Rais Samia kwani hayo ni madai yao ya msingi ktk suala zima la kuleta maridhiano nchini.
 
shida ya Lissu ni political extremist. Aelewe siasa ni mchezo wa mapambano na maelewano kufikia malengo ya kushika dola.it is both kulingana na mazingira ingawa hoja zake kuhusu kukataliwa maridhiano ina mashiko,kutokuamiana ndilo tatizo la CDM na CCM hawatakaa wajenge jambo moja.Alipokuja kujiunga na vikao tu mambo yakaharibika.Ni hardliner mno hafai kwenye negotiation.
Maridhiano hayakuvunjika kwa sababu ya Lissu bali ni sababu ya CCM kuogopa wakifanya uchaguzi huru hawatarudi madarakani.
 
Nadhani wafuasi wa Chadema mnachokosea mnadhani kila anayeikosoa Chadema ni mfuasi wa CCM anayetaka upinzani ufe, wengine hatuna hata vyama, bali tunataka nchi yenye siasa safi za kujenga

Kwa siasa zenu hizi za kudandia na kushabikia wapuuzi kama akina Mange na Kigogo mna safafi ndefu sana ya kuaminiwa kama watu serious mnaoweza kuongoza nchi

..hivi umewahi kukosoa au kukemea wana Ccm wanaotukana na kuwadhalilisha viongozi na wafuasi wa Chadema?

..huyo Kigogo si alikuwa mtu wa Ccm akitukana viongozi wa Chadema? Je, serikali ilimchukulia hatua zozote?

..Nadhani tatizo lenu Ccm ni kujiona nyinyi ni binadamu wa daraja la juu kuliko walioko ktk vyama mbadala. Mmelelewa kuamini kwamba wapinzani wanastahili kutukanwa, kutekwa, kuuwawa, wakati nyinyi anastahili kuishi kwa heshima,kinga, na ulinzi.
 
Aisee sikujua Tundu Lissu ana chuki hivi hadi awamu hii ya Samia....Kwa hiyo Samia kualikwa kwenye mkutano wa Chadema kuna na akahudhuria ameona ni shida kubwa, anataka zile siasa za Kihutu na Kitutsi na sio siasa za kuona CCM na Chadema wote ni watanzania
Haya mambo tuliyaonja kidogo kipindi cha Magufuli na Lissu alikuwa mhanga, ila ndio anayatamani?
Lissu anataka siasa za ushindani na haki. Unataka awe kama Zitto anayeweka tumbo lake mbele?
 
Nadhani wafuasi wa Chadema mnachokosea mnadhani kila anayeikosoa Chadema ni mfuasi wa CCM anayetaka upinzani ufe, wengine hatuna hata vyama, bali tunataka nchi yenye siasa safi za kujenga

Kwa siasa zenu hizi za kudandia na kushabikia wapuuzi kama akina Mange na Kigogo mna safafi ndefu sana ya kuaminiwa kama watu serious mnaoweza kuongoza nchi
Huu sasa ndiyo huwa naita ujinga wa nguchiro. Hivi unadhani CHADEMA wanapigania mabadiliko kwa faida yao na watoto wao? Wengine hatuna vyama lakini tunataka chaguzi ziwe huru na haki ili tupate viongozi bora bila kujali wanatokea CCM au chama kingine. Wewe umeshajivika ujinga wa kudhani kuwa Mbowe au Lissu ndiyo watafaidi iwapo kutakuwa na mabadiliko.
 
Anachokihubiri Tund Lissu ndio wafuasi wa Magufuli wanakitaka, sababu wanajua siasa hizo zinawafanya waweze kuwafanyia wapinzani kitu chochote na wasifanywe chochote

Actually ukichunguza kwa makini utaona mashabiki wa mwendazake wanamshangilia Tundu Lissu japokuwa hawampendi, wanajua atawapa wanachotaka
Acha iwe hivyo boss, hata huyo Magufuli na siasa zake hatukuwahi kumpigia magoti, hiyo ilimfanya atumie nguvu kubwa kupiga propaganda anakubalika, lakini ukweli alijua Kuna kundi kubwa halikuwa linamkubali, labda sana sana kumuogopa na hilo lilikuwa jambo la muda tu. wale walioshindwa walienda kuunga juhudi.

Na kwa kukusaidia tu huyu mama Samia hafanyi wema kwa kujifanya yuko tofauti na Magufuli, bali yeye sio mkatili kama Magufuli. Hata kama angechukua madaraka mikononi mwa kikwete, bado hiki afanyacho ndio angekifanya. Kuna nyie mnaotaka kupotosha kuonyesha kuwa anafanya hivyo kumprove wrong Magufuli kitu ambacho sio kweli. Kama angetaka tumuone tofauti na Magufuli, angeruhusu katiba mpya, na tume huru ya uchaguzi. Tuko tayari kuishi katika siasa zile za Magufuli maana ndio zitaleta mabadiliko ya kweli baada ya machafuko, kuliko hizi siasa za danganya toto.
 
..hatupaswi kurudi kwenye utekaji na mauaji.

..tunatakiwa tuweke mfumo wa haki ktk siasa na chaguzi zetu.

..Rais Samia amepiga chenga hoja ya Tume Huru, na Katiba Mpya.

..Chadema wana haki ya kumlaumu Rais Samia kwani hayo ni madai yao ya msingi ktk suala zima la kuleta maridhiano nchini.
Kujenga mfumo wa haki hakufanywi kwa kuhubiri siasa za utengano na chuki mzee, unajenga ushawishi na sapoti ya wananchi, wasomi mnashinikiza
Kinachofanywa na huyo jamaa yenu Lissu mtu independent mwenye akili timamu hawezi kukiunga mkono, labda nyie wafuasi wake wa kila kitu ndio mzee, kama manyumbu
 
..hivi umewahi kukosoa au kukemea wana Ccm wanaotukana na kuwadhalilisha viongozi na wafuasi wa Chadema?

..huyo Kigogo si alikuwa mtu wa Ccm akitukana viongozi wa Chadema? Je, serikali ilimchukulia hatua zozote?

..Nadhani tatizo lenu Ccm ni kujiona nyinyi ni binadamu wa daraja la juu kuliko walioko ktk vyama mbadala. Mmelelewa kuamini kwamba wapinzani wanastahili kutukanwa, kutekwa, kuuwawa, wakati nyinyi anastahili kuishi kwa heshima,kinga, na ulinzi.
Mimi sio CCM mzee, mbona nishakueleza, tatizo mnakariri kila mtu anayekosoa hao viongozi wenu wakikengeuka ni CCM, mnataka kila mtanzania awe nyumbu wa kushangilia kila utumbo wa Chadema

Nimekosoa sana uonevu wa serikali ya CCM dhidi ya wapinzani, Ninemkosoa sana Magufuli kwa aliyokuwa akifanya kwa upinzani na nakosoa legacy yake hadi leo, nimemkosoa sana Samia kipindi amemfungulia Mbowe kesi ya ugaidi, Labda hunijui hapa jukwaani sababu tupo wengi,

Huyo Lissu nilimchangia na kuhamasisha kuchangiwa fedha za matibabu kipindi amepigwa risasi, sipendi uonevu ila sina loyalty kwa mtu kama akileta ujinga
 
Back
Top Bottom