Pre GE2025 Lissu: Sijui ilikuwaje CHADEMA tukamualika Rais Samia, ila mbeleni tutaelezana

Pre GE2025 Lissu: Sijui ilikuwaje CHADEMA tukamualika Rais Samia, ila mbeleni tutaelezana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nani kakuambia Marekani ndio role model wetu kwenye kila kitu? Marekani wanaruhusu ushoga, so turuhusu ushoga kisa Marekani anaruhusu?

Marekani kulishatokea Rais kichaa kama Magufuli na kuvuruga nchi vile? Nchi ikivurugwa kwa misingi ya vyama kama alivyofanya Magufuli unadhani haihitaji kuileta pamoja tena?
Unazungumza ujinga mtupu..JPM alivuruga vipi au mlijivuruga wenyewe...msimsingizie...mliambiwa kama mlikuwa na ushahidi pelekeni Mahakamani hamsikii, mnabaki kupiga mayowe tu....inawasaidia nini..haya, JPM hayupo, aliyekuwa Makamu wake si ndio Rais wetu, anasema Kazi iendelee ileile kama walivyoanzisha na mtangulizi wake...CCM inaendelea kujiimarisha na kumtumikia wananchi mbelekwa mbele..mpo..!!!! Mmekaa kukenua meno tu kama sifi..au fisi..
 
Acha iwe hivyo boss, hata huyo Magufuli na siasa zake hatukuwahi kumpigia magoti, hiyo ilimfanya atumie nguvu kubwa kupiga propaganda anakubalika, lakini ukweli alijua Kuna kundi kubwa halikuwa linamkubali, labda sana sana kumuogopa na hilo lilikuwa jambo la muda tu. wale walioshindwa walienda kuunga juhudi.

Na kwa kukusaidia tu huyu mama Samia hafanyi wema kwa kujifanya yuko tofauti na Magufuli, bali yeye sio mkatili kama Magufuli. Hata kama angechukua madaraka mikononi mwa kikwete, bado hiki afanyacho ndio angekifanya. Kuna nyie mnaotaka kupotosha kuonyesha kuwa anafanya hivyo kumprove wrong Magufuli kitu ambacho sio kweli. Kama angetaka tumuone tofauti na Magufuli, angeruhusu katiba mpya, na tume huru ya uchaguzi. Tuko tayari kuishi katika siasa zile za Magufuli maana ndio zitaleta mabadiliko ya kweli baada ya machafuko, kuliko hizi siasa za danganya toto.
Labda wewe hukumpigia magoti lakini viongozi wengi sana wa chama chako walimpigia magoti Magufuli, wengine kukimbia nchi, Magufuli alivyokufa wakashukuru Mungu, maana ndio ilikuwa ahueni yao

Sijasema kuwa Samia yupo anataka kum prove wrong Magufuli, nilichosema ni kuondoka kwa zile extremist politics za awamu ya Magufuli ambazo naona Lissu anataka sana kuziamsha

Watanzania hawana uwezo wowote wa kufanya vurugu wa kupinga eti kiongozi katili, ndio kwanza watamshangilia kuwa ndio kiongozi aliyeiweza nchi....Ndio maana hata ukiweka poll hapa leo ya viongozi bora Tanzania, wengi watasema Magufuli alikuwa bora
 
Unazungumza ujinga mtupu..JPM alivuruga vipi au mlijivuruga wenyewe...msimsingizie...mliambiwa kama mlikuwa na ushahidi pelekeni Mahakamani hamsikii, mnabaki kupiga mayowe tu....inawasaidia nini..haya, JPM hayupo, aliyekuwa Makamu wake si ndio Rais wetu, anasema Kazi iendelee ileile kama walivyoanzisha na mtangulizi wake...CCM inaendelea kujiimarisha na kumtumikia wananchi mbelekwa mbele..mpo..!!!! Mmekaa kukenua meno tu kama sifi..au fisi..
Unaposema "mlijivuruga wenyewe" unamaanisha nini, maana mimi siwakilishi kundi lolote... Magufuli alivuruga nchi ndio maana viongozi wa vyama vyote CCM na upinzani walifurahia kifo chake, utakuwa mshamba sana kama hujui hili
 
Huu sasa ndiyo huwa naita ujinga wa nguchiro. Hivi unadhani CHADEMA wanapigania mabadiliko kwa faida yao na watoto wao? Wengine hatuna vyama lakini tunataka chaguzi ziwe huru na haki ili tupate viongozi bora bila kujali wanatokea CCM au chama kingine. Wewe umeshajivika ujinga wa kudhani kuwa Mbowe au Lissu ndiyo watafaidi iwapo kutakuwa na mabadiliko.
Sitegemei mabadiliko yoyote kwao, naowaona kama watu walio disorganized, hawana principle, hawana discipline na hawawezi kuleta mabadiliko chanya,
 
Sisi sote siyo watanzania. Ingekuwa hivyo Samia asingewavurumisha wamasai ili waarabu wapate sehemu.
Ni mtazamo tu, wengine wamekuaminisha ni kuwavurumisha wamasai, wengine wanaona ni kulinda ngorongoro, ila hiyo ni topic nyingine
 
Labda wewe hukumpigia magoti lakini viongozi wengi sana wa chama chako walimpigia magoti Magufuli, wengine kukimbia nchi, Magufuli alivyokufa wakashukuru Mungu, maana ndio ilikuwa ahueni yao

Sijasema kuwa Samia yupo anataka kum prove wrong Magufuli, nilichosema ni kuondoka kwa zile extremist politics za awamu ya Magufuli ambazo naona Lissu anataka sana kuziamsha

Watanzania hawana uwezo wowote wa kufanya vurugu wa kupinga eti kiongozi katili, ndio kwanza watamshangilia kuwa ndio kiongozi aliyeiweza nchi....Ndio maana hata ukiweka poll hapa leo ya viongozi bora Tanzania, wengi watasema Magufuli alikuwa bora
Nimekuambia aliyeshindwa hayo alienda kuunga juhudi, lakini Bado tuko wengi ambao. Watanzania hawawezi kufanya fujo Leo ama kesho, lakini hakuna uwezekano wa kutawala watu muda wote kwa mabavu.

Ni kweli Kuna watu walimkubali Magufuli, lakini hiyo haimaanishi wote tulimkubali. Watu wachache sana wangetosha kumuondoa mtu kama Magufuli. Nadani umeona Nini kilitokea. Tunataka mabadiliko ya kweli, sio uungwana wa kiongozi boss.
 
Sitegemei mabadiliko yoyote kwao, naowaona kama watu walio disorganized, hawana principle, hawana discipline na hawawezi kuleta mabadiliko chanya,
Kama ccm wako madarakani Hadi Leo mkuu nani atashindwa kuongoza nchi ya hivyo?
 
Lissu anataka siasa za ushindani na haki. Unataka awe kama Zitto anayeweka tumbo lake mbele?
Hawezi ushindani wowote, kashindwa kutengeneza hoja za kuvutia wananchi anaanza ku attack asili ya Samia kuwa ni Mzanzibari eti ndio maana anauza sijui ardhi...na nyie wafuasi wake mnakua kama manyumbu flani hivi kudhangilia kila uharo wake
 
Unaposema "mlijivuruga wenyewe" unamaanisha nini, maana mimi siwakilishi kundi lolote... Magufuli alivuruga nchi ndio maana viongozi wa vyama vyote CCM na upinzani walifurahia kifo chake, utakuwa mshamba sana kama hujui hili
Nyie mliotumbuliwa na vyeti feki na ufisadi ndio mlifurahia...fanya research basi kwa wananchi upate data...ndio maana hata Dr SSH anaendeleza yote na wananchi wamemwelewa.. kwa sabab mipango yote walipanga pamoja..Sasa wewe mtumbuliwaji endelea kukenua meno tu kwa ushamba
 
Hawezi ushindani wowote, kashindwa kutengeneza hoja za kuvutia wananchi anaanza ku attack asili ya Samia kuwa ni Mzanzibari eti ndio maana anauza sijui ardhi...na nyie wafuasi wake mnakua kama manyumbu flani hivi kudhangilia kila uharo wake
I seems that you are full of anger about Lissu. Samia ni mzanzibar au siyo mzanzibar? Samia kawafukuza wamasai na kwenye ardhi na kuwapa waarabu au hakuwapa? Kama ''unyumbu'' ni kusema ukweli, basi acha iwe hivyo. Kwanza huu muungano ni hasara kwetu Tanganyika na hautusaidii lolote. Inakuwaje kila rais anayetoka Zanzibar anauza mali zetu kwa waarabu?
 
Unaposema "mlijivuruga wenyewe" unamaanisha nini, maana mimi siwakilishi kundi lolote... Magufuli alivuruga nchi ndio maana viongozi wa vyama vyote CCM na upinzani walifurahia kifo chake, utakuwa mshamba sana kama hujui hili
Viongoz haohao wa upinzani walihamia CCM kwenda kupiga kazi we unatuambia nini jomba, hahahaha..utasema walinunuliwa, hivi mpinzani wa ukweli unawezaje kununuliwa...basi kama itakuwa hivyo nchi yetu Haina mpinzani wa kweli, maana wote wanaweza kununuliwa..ni jambo la wakati tu
 
Sitegemei mabadiliko yoyote kwao, naowaona kama watu walio disorganized, hawana principle, hawana discipline na hawawezi kuleta mabadiliko chanya,
Anzisha chama chako na basi. Utapata wafuasi wengi sana kwa jinsi ulivyo na mikakati.
 
Nimekuambia aliyeshindwa hayo alienda kuunga juhudi, lakini Bado tuko wengi ambao. Watanzania hawawezi kufanya fujo Leo ama kesho, lakini hakuna uwezekano wa kutawala watu muda wote kwa mabavu.

Ni kweli Kuna watu walimkubali Magufuli, lakini hiyo haimaanishi wote tulimkubali. Watu wachache sana wangetosha kumuondoa mtu kama Magufuli. Nadani umeona Nini kilitokea. Tunataka mabadiliko ya kweli, sio uungwana wa kiongozi boss.
Kwani ni nini kilitokea?
 
Sasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema

Kunielewa hebu turudi kidogo nyuma kipindi cha Magufuli mambo yalivyokuwa

Kipindi cha Magufuli, siasa za CCM vs Chadema, zilikuwa ni siasa extreme sana, CCM na Chadema ilikuwa kama makundi ya Wahutu na Watusti kule Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari

Kuna kipindi Wabunge wa CCM walipewa onyo kali kumtembelea mbunge mwenzao Lema gerezani alipowekwa rumande kwa miezi kadhaa
Wabunge wa CCM wakapigwa marufuku kumtembelea Lissu hospitalini alipopigwa risasi, na Lazaro Nyalandu mbunge pekee wa CCM aliyemtembelea Lissu aliingia matatizoni na chama chake kwa kufanya jambo hilo hadi ikambidi kuhama

Wananchi nao wakaambiwa waziwazi hawatatatuliwa shida zao kwa sababu walichagua wabunge wa upinzani
Bado kulikuwa na visa vingi vya kesi za kisiasa, kutekwa, mauaji hadi wapinzani akiwemo Lissu na Lema kukimbia nchi.

Fast Forward leo hii, Rais Samia pamoja na mapungufu yake ameondoa siasa hizo za extremism
Samia ameweka mbele kuwa sisi wote ni Watanzania kwanza kabla ya kuwa CCM ama Upinzani
Ndio maana hata Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema akahudhuria, alikutana na viongozi wa Chadema, kufuta kesi, waliokuwa wamekimbia wakaambiwa warudi, mikutano imeruhusiwa na mengine mengi

Sasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema
Anasema pia anakusudia kumshtaki Samia kwa kuweka picha aliyopiga na viongozi wa Chadema kwenye bango

Hizi siasa za kuonana maadui kutokana tu na tofauti ya vyama vyetu tukirudi tena huko waathirika wakubwa ni Chadema, sio CCM, actually kundi kubwa la CCM linatamani turudi huko kwa sababu wao wanaweza kufanya lolote kwa upinzani bila kufanywa chochote kama tulivyoona kipindi cha Magufuli

Ni muda sasa viongozi wa Chadema wakamuonya Tundu Lissu
Uko sahihi kwenye hoja zako ila kuna jambo CDM ililitegemea kutoka kwa MH.rais nalo ni real reform ya mifumo ya kisiasa kitu ambacho hakijafanyika na hakitofanyika chini ya uongozi wa CCM,hivyo kwa mtazamo wangu ninaona ile nia ya mwanzo ya rais ni either delay tactic au kupingwa na wenzake ndani ya chama
 
Akiwa mkoani Iringa katika mkutano wa hadhara Lissu amesema hajui ilikuwaje CHADEMA ikamualika mama kwenye mkutano wa CHADEMA maana huwa hawaji wenyewe ni mpaka waalikwe.

Aidha Lissu amewatahadharisha wanaCHADEMA kuwa makini maana kwenye uchaguzi wa ndani ya Chama kuna hela nyingi inatumika ambapo Lissu amesema fedha hiyo ni ya Abdul na Mama yake maana chadema hawana hela hata kufanya mikutano huwa inakuwaga ni shida kwasababu ya fedha ila cha ajabu watu wanapewa fedha kwenye uchaguzi wa ndani.

Lissu ameamua kufanya swala la Uchaguzi wa ndani wa CHADEMA kuwa swala la Umma.
Kwa hiyo tutarajie akina Abdul wengi Chamani🤔
 
Viongoz haohao wa upinzani walihamia CCM kwenda kupiga kazi we unatuambia nini jomba, hahahaha..utasema walinunuliwa, hivi mpinzani wa ukweli unawezaje kununuliwa...basi kama itakuwa hivyo nchi yetu Haina mpinzani wa kweli, maana wote wanaweza kununuliwa..ni jambo la wakati tu
Kuna ambao Walimfuata sababu walikuwa wakimumini na kuna ambao walimfuata sababu walikuwa wakiogopa, alikuwa na jeshi la kuwaua au kuwafunga na fedha za kuwapa..ni kama jambazi anakuvamia nyumbani kwako anakitishia kukuua akitaka umpe fedha, unaona bora kumpa fedha kuliko uhai, ndio alichokuwa akifanya Magufuli...Ila hatupo nae tena na tunashukuru
 
Back
Top Bottom