Sasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema
Kunielewa hebu turudi kidogo nyuma kipindi cha Magufuli mambo yalivyokuwa
Kipindi cha Magufuli, siasa za CCM vs Chadema, zilikuwa ni siasa extreme sana, CCM na Chadema ilikuwa kama makundi ya Wahutu na Watusti kule Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari
Kuna kipindi Wabunge wa CCM walipewa onyo kali kumtembelea mbunge mwenzao Lema gerezani alipowekwa rumande kwa miezi kadhaa
Wabunge wa CCM wakapigwa marufuku kumtembelea Lissu hospitalini alipopigwa risasi, na Lazaro Nyalandu mbunge pekee wa CCM aliyemtembelea Lissu aliingia matatizoni na chama chake kwa kufanya jambo hilo hadi ikambidi kuhama
Wananchi nao wakaambiwa waziwazi hawatatatuliwa shida zao kwa sababu walichagua wabunge wa upinzani
Bado kulikuwa na visa vingi vya kesi za kisiasa, kutekwa, mauaji hadi wapinzani akiwemo Lissu na Lema kukimbia nchi.
Fast Forward leo hii, Rais Samia pamoja na mapungufu yake ameondoa siasa hizo za extremism
Samia ameweka mbele kuwa sisi wote ni Watanzania kwanza kabla ya kuwa CCM ama Upinzani
Ndio maana hata Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema akahudhuria, alikutana na viongozi wa Chadema, kufuta kesi, waliokuwa wamekimbia wakaambiwa warudi, mikutano imeruhusiwa na mengine mengi
Sasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema
Anasema pia anakusudia kumshtaki Samia kwa kuweka picha aliyopiga na viongozi wa Chadema kwenye bango
Hizi siasa za kuonana maadui kutokana tu na tofauti ya vyama vyetu tukirudi tena huko waathirika wakubwa ni Chadema, sio CCM, actually kundi kubwa la CCM linatamani turudi huko kwa sababu wao wanaweza kufanya lolote kwa upinzani bila kufanywa chochote kama tulivyoona kipindi cha Magufuli
Ni muda sasa viongozi wa Chadema wakamuonya Tundu Lissu