johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mtanikumbuka πππππHuyu mtu wenu angeachwa afe tuu maana Sasa habebeki.
Unalala kwenye matope mtu apite asichafuke then Asema kwanza ulilala vibaya π€£π€£
Ndio maana hapa Duniani usijifanye mwema sana,ubinadamu ni kazi
CCM na Chadema ni kama Yesu na ShetaniSasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema
Kunielewa hebu turudi kidogo nyuma kipindi cha Magufuli mambo yalivyokuwa
Kipindi cha Magufuli, siasa za CCM vs Chadema, zilikuwa ni siasa extreme sana, CCM na Chadema ilikuwa kama makundi ya Wahutu na Watusti kule Rwanda kabla ya mauaji ya kimbari
Kuna kipindi Wabunge wa CCM walipewa onyo kali kumtembelea mbunge mwenzao Lema gerezani alipowekwa rumande kwa miezi kadhaa
Wabunge wa CCM wakapigwa marufuku kumtembelea Lissu hospitalini alipopigwa risasi, na Lazaro Nyalandu mbunge pekee wa CCM aliyemtembelea Lissu aliingia matatizoni na chama chake kwa kufanya jambo hilo hadi ikambidi kuhama
Wananchi nao wakaambiwa waziwazi hawatatatuliwa shida zao kwa sababu walichagua wabunge wa upinzani
Bado kulikuwa na visa vingi vya kesi za kisiasa, kutekwa, mauaji hadi wapinzani akiwemo Lissu na Lema kukimbia nchi.
Fast Forward leo hii, Rais Samia pamoja na mapungufu yake ameondoa siasa hizo za extremism
Samia ameweka mbele kuwa sisi wote ni Watanzania kwanza kabla ya kuwa CCM ama Upinzani
Ndio maana hata Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema akahudhuria, alikutana na viongozi wa Chadema, kufuta kesi, waliokuwa wamekimbia wakaambiwa warudi, mikutano imeruhusiwa na mengine mengi
Sasa Tundu Lissu anataka turudi kwenye zile siasa za chuki, kwenye mikutano yake huko Iringa anahoji kwa nini Samia alialikwa kwenye mkutano wa Chadema
Anasema pia anakusudia kumshtaki Samia kwa kuweka picha aliyopiga na viongozi wa Chadema kwenye bango
Hizi siasa za kuonana maadui kutokana tu na tofauti ya vyama vyetu tukirudi tena huko waathirika wakubwa ni Chadema, sio CCM, actually kundi kubwa la CCM linatamani turudi huko kwa sababu wao wanaweza kufanya lolote kwa upinzani bila kufanywa chochote kama tulivyoona kipindi cha Magufuli
Ni muda sasa viongozi wa Chadema wakamuonya Tundu Lissu
Lisu awe makini sana na mwenyekiti wake maana huyo ndio anaendekeza hizo pesa chafu za ccm.
Tanzania kuna vituko kweli. Sasa hapo chuki ziko wapi? Usishangae wakikutana wanakunywa chai pamoja. Kwa nchi zingine za Africa siasa anafanya lissu ndo siasa yao. Zoeeni siasa ya aina ya lissu. Siasa za kubembelezana zimeshaisha.Akiwa mkoani Iringa katika mkutano wa hadhara Lissu amesema hajui ilikuwaje CHADEMA ikamualika mama kwenye mkutano wa CHADEMA maana huwa hawaji wenyewe ni mpaka waalikwe.
Aidha Lissu amewatahadharisha wanaCHADEMA kuwa makini maana kwenye uchaguzi wa ndani ya Chama kuna hela nyingi inatumika ambapo Lissu amesema fedha hiyo ni ya Abdul na Mama yake maana chadema hawana hela hata kufanya mikutano huwa inakuwaga ni shida kwasababu ya fedha ila cha ajabu watu wanapewa fedha kwenye uchaguzi wa ndani.
Lissu ameamua kufanya swala la Uchaguzi wa ndani wa CHADEMA kuwa swala la Umma.
Ni kwa ajili ya kujenga taifa sio kwa ajili ya hilo lichama lenu.Yuko sahihi ile ilikuwa n kujipendekeza tu kwa samia, hakuna ccm yeyote mpk huyo mzanzibar hakuna anayewapenda chadema, we unampendaje mtu aliyedhamilia kukutoa madarakani. Ccm wapo tyr hata leo viongoz wote wa chadema wauawe if possible so yuko sawa.
Ndivyo Magufuli na Tundu Lissu na wafuasi wao wanavyotaka iweCCM na Chadema ni kama Yesu na Shetani
Jalalani ni nyumbani kwa wendawazimu!!!Allen Kilewella, denoo JG mnakwitwa huku
Wewe unapenda Yesu na Shetani washirikiane?πΌNdivyo Magufuli na Tundu Lissu na wafuasi wao wanavyotaka iwe
Shetani hakwenda kwa Mungu kujadiliana naye mambo ya Ayubu??Wewe unapenda Yesu na Shetani washirikiane?πΌ
Jalalani ni nyumbani kwa wendawazimu!!!
Basi mshaurini Lisu awe muelewaShetani hakwenda kwa Mungu kujadiliana naye mambo ya Ayubu??
Hivi devo hakupiga stori na jizaz kule mlimani kumshawishi ageuze jiwe liwe mkate!?
Ushasahau mara hii kuwa Bi Mkubwa Hawa kabla ya kula tunda la mti wa kati ya bustani alikuwa anapiga stori na Devo wakati Mzee mzima Adam anakata mitaa?
Kama Ayatollah Khamenei anawasiliana na Marekani ndiyo itakuwa Mbowe na Samia!??
Lakini pia hiki ni kitu cha ajabu kidogo ni sawa na Simba wawaalike Yanga kwenye mkutano wao mkuu unajadili jinsi ya kuchukua ubingwa.Aisee sikujua Tundu Lissu ana chuki hivi hadi awamu hii ya Samia....Kwa hiyo Samia kualikwa kwenye mkutano wa Chadema kuna na akahudhuria ameona ni shida kubwa, anataka zile siasa za Kihutu na Kitutsi na sio siasa za kuona CCM na Chadema wote ni watanzania
Haya mambo tuliyaonja kidogo kipindi cha Magufuli na Lissu alikuwa mhanga, ila ndio anayatamani?
Kina Petro kwenye kila kundi huwa hawakosekani... Yesu akamwambia, rudisha jamvia lako alani...ππBasi mshaurini Lisu awe muelewa
Kwani Samia alialikwa kwenye mkutano gani wa kimkakati ndani ya CHADEMA?Lakini pia hiki ni kitu cha ajabu kidogo ni sawa na Simba wawaalike Yanga kwenye mkutano wao mkuu unajadili jinsi ya kuchukua ubingwa.
ππππππππKina Petro kwenye kila kundi huwa hawakosekani... Yesu akamwambia, rudisha jamvia lako alani...ππ
Wenyewe huwa wanaona wanatetea "status quo" kumbe siyo Kila wakati ni wa vita.ππππππππ
Niliandika kuwa waTanzania sio watu wa kuongozwa ni watu tuliozea kutawalia iwe na mkolni au machifu ,tukiaachiwa huru tutahadaika na kiza na ndio ukaona baadhi ya wanasiasa wanaharisha njiani.Aisee sikujua Tundu Lissu ana chuki hivi hadi awamu hii ya Samia....Kwa hiyo Samia kualikwa kwenye mkutano wa Chadema kuna na akahudhuria ameona ni shida kubwa, anataka zile siasa za Kihutu na Kitutsi na sio siasa za kuona CCM na Chadema wote ni watanzania
Haya mambo tuliyaonja kidogo kipindi cha Magufuli na Lissu alikuwa mhanga, ila ndio anayatamani?