Mimi nafikiri ni lazima kuelewa muktadha kwanza ndio maana nikaanza na utangulizi jinsi ya siasa za nchi hii zilivyokua kabla ya Samia kuingia madarakani, kulikuwa na chuki na uhasama mkubwa sana hadi watu kukimbia nchi kwa kuhofia kuuawa,
Ili kuondoa hizo chuki na uhasama, ndio ikaja maridhiano, kuleta tena watanzania pamoja
Na ule haukuwa mkutano wa kupanga chochote ilikuwa ni siku ya wanawake duniani, sio kupanga kushinda uchaguzi
Sasa kama wapinzani wanataka siasa za uadui na vita, wahanga wakubwa watakuwa ni wao, sio CCM, CCM wana dola na wawaweza kufanya chochote wapinzani bila kuchukuliwa hatua yoyote