......Looh,
Jidu La Mabambasi hapa una lipi la kusema ndugu yangu? Ulikuwa unawaza nini kuleta hoja ya ajabu kama hii hapa jukwaani?
.....Hii iko chini ya kiwango cha fikra na ufahamu wako. Hukustahili kuja na propaganda ya hovyo kiasi hiki!
....Tundu Lissu ni mtu mzuri sana, Hana unafiki na husema ukweli mtupu ambao ni mwiko kwa CCM na hiyo ndiyo kashfa kwa wana CCM wa sampuli yako
Jidu La Mabambasi
....hivi nyie huko CCM ni watu wa namna gani msiotaka kukosolewa? Tangu lini kukosoana ikawa kashfa au matusi jamani?
Mimi nahisi kinachowakera kwa Tundu Lissu, ni lugha ambayo huitumia ktk kutoa hoja zake. Huwa halembi eti
.....Anapokosoa hutumia lugha kali, ya kukera na yenye mamlaka. Hili huwaudhi sana watawala.
....Kwangu mimi Hili ni jema sana pale mtu anaporekebisha mambo na makosa yaliyofanywa na manunda wa ujinga huko CCM