Lissu ukirudi Tanzania zingatia hili, kumkashifu Baba wa Taifa ni off limits

Lissu ukirudi Tanzania zingatia hili, kumkashifu Baba wa Taifa ni off limits

Nyerere, Yesu, and Muhamad walikuwa binadamu tu! Ni pilitics push ndiyo zikawafanya wafikie hapo walipo! Mwisho wa siku ni FK them all
 
Kukosoa sera za mtu ni kumkashifu? Hili taifa lina wajinga wengi
CCM kuna wajinga wengi sana
JamiiForums1389173211.jpg
 
..unawezaje kuikosoa na kuichambua Katiba ya 1977 bila kumkosoa na kumchambua Mwalimu Nyerere muasisi wa katiba hiyo?

..au unaweza vipi kuukosoa muungano na jinsi ulivyoasisiwa bila kuwa umewagusa waasisi wa muungano Mwalimu Nyerere na Sheikh Karume?

..naamini Lissu ni kati ya wasomi ambao wanaweza kutoa mchango wenye tija kwa Watanzania wote tunapoelekea kuandika Katiba Mpya na kuunda Tume Huru ya uchaguzi.

..tumpe uhuru Lissu afundishe kuhusu Katiba bora na kutoa elimu ya uraia kwa faida ya Watanzania wote.
SAWA.

Na ninakubaliana nawe kuhusu nafasi ya Lissu, hasa nyakati hizi za leo.

Yaliyofanyika wakati wa Mwalimu mengi yalikuwa na sababu za kufanyika yalivyofanyika kwa wakati huo, kwa hiyo tunapojadili upungufu unaoonekana leo katika hali ya leo, tusisahau 'context' hiyo.

Muungano ulio asisiwa haukuwa kamilifu ulipoanzishwa, hilo linajulikana na lilizungumziwa waziwazi.

Makosa mengi yaliyoendelea kujitokeza na mengine kuongezwa, ni mapungufu ya walioendelea kuulea muungano huo, wakiutumia kwa manufaa yao. Hawakushughulika tena na kuuboresha muungano, bali kuwaridhisha/kuwahonga wapiga kelele waliotishia muungano, wakidhani kelele zitakwisha kwa hongo.
 
......Looh, Jidu La Mabambasi hapa una lipi la kusema ndugu yangu? Ulikuwa unawaza nini kuleta hoja ya ajabu kama hii hapa jukwaani?

.....Hii iko chini ya kiwango cha fikra na ufahamu wako. Hukustahili kuja na propaganda ya hovyo kiasi hiki!

....Tundu Lissu ni mtu mzuri sana, Hana unafiki na husema ukweli mtupu ambao ni mwiko kwa CCM na hiyo ndiyo kashfa kwa wana CCM wa sampuli yako Jidu La Mabambasi

....hivi nyie huko CCM ni watu wa namna gani msiotaka kukosolewa? Tangu lini kukosoana ikawa kashfa au matusi jamani?

Mimi nahisi kinachowakera kwa Tundu Lissu, ni lugha ambayo huitumia ktk kutoa hoja zake. Huwa halembi eti

.....Anapokosoa hutumia lugha kali, ya kukera na yenye mamlaka. Hili huwaudhi sana watawala.

....Kwangu mimi Hili ni jema sana pale mtu anaporekebisha mambo na makosa yaliyofanywa na manunda wa ujinga huko CCM
Mada niliyoileta iko wazi, na inaeleweka vizuri sana.
Kuna kukosoa sera na kukashifu mtu.
Mtu kama Lissu kwa kupenda sifa za kijinga aliwahi kuchagua kukashifu, tena vibaya.
Hilo halikubaliki.
Kumkashifu kiingizi na muasisi wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Lissu akirudia tena, si tu hataeleweka, lakini ataoata madhara asiyoyatarajia.
Lissu pamoja na wenzake wanatakiwa walete sera mbadala za kiuchumi na kijamii ili kuimarisha Taifa.
 
..Na wanaomtukana Lissu matusi makubwa-kubwa inakubalika? Mtawachukulia hatua gani?
 
Unasema sera na msingi iko pale pale wakati NYAKATI zinabadilika ! eg. Huwezi ukaleta sera na misingi ya ujamaa nyakati hizi tukakuelewa maana ata waasisi wa ujamaa China na Urusi wameachana nao.

Pia ni ujinga kufikiri kwamba kukosoa ni kukashifu,au hauelewi maana ya kashfa na kukosoa?

Tuache ujinga na umbumbumbu,tutamkosoa yoyote maana hakuna Mungu mtu Tanzania.

By the way nchi imeundwa na wakoloni,pia kuna wengi tu walisaidia kuleta uhuru wa kisiasa na sio Nyerere pekee
Ni kweli ni vzr kukosoana maana ndio kujenga, bila challenges hakuna maendeleo,na kumkosoa mwl.Nyerere sio kosa kabisa.Mm nadhani sisi kama watanzania tungejihoji maswali ya msingi labda yangetusaidia sana na labda tungetoka na fikra za juu zaidi maana lalamiko letu kubwa kabisa ni Umaskini wa watanzania na afrika kwa ujumla wake ambao kila mtanzania na mwafrika anaumizwa nao.labda tungejiuliza yafuatayo.
1.kwa nn nchi za Afrika na Tanzania ikiwemo bado ni tegemezi kwa asilimia 90 pamoja na kuwa na rasilimali nyingi.
2.Mwalimu nyerere alijitahi kulinda rasilimali kwa manufaa ya watanzania lkn kwa nn rasilimali hizo haziwasaidii watanzania.
3.kwa nini sisi waafrika wa leo na watanzania ni waoga kutetea mambo tunayoyaamini kwa manufaa yetu wenyewe.
4.kwa nini tumekuwa na akili ngumu ya kuwatambua wanasiasa tulionao.
5.kwa nini wanasiasa wetu hawajali wafuasi wao ambao wanapoteza uhai kwa ajili yao wakiwapigania na wako rahisi kabisa kujiunga au kurudi
kwenye vyama hasimu.
6.kwa nn baadhi ya watanzania wachache na wanasiasa wanadhani tutafanikiwa kuiondoa CCM jirahisi kutoka mamlakani.
7.Leo tunampokea mtoto wetu na ndugu yetu mtanzania Tundu Antipas Lissu akitokea Ubelgiji alikokuwa amekimbilia swali je anaweza kutukomboa katika hali ngumu yoyote tunayoweza kupitia.
8.Je mkombozi wa kweli ktk Taifa ni nani? Ni mtanzania mwenyewe au ni nani?
9.Je ni vizuri kuwashabikia wanasiasa wanaokimbilia ughaibuni na kuwadharau hawa wanaobaki nchini na kupambana na kila hali inayotokea ktk Taifa.
NB.Kwa tulipofika watanzania tunahitaji kutumia akili zaidi kuliko Elimu tuliyonayo,maana akili itatupa utambuzi zaidi.
 
Tundu Lissu karibu Bongo.

Nchi hii imeundwa, na walioiunda wengi wametangulia mbele za haki. Lakini sera, misimamo na misingi yao ya haki na maendeleo kiuchumi, kijamii kwa ujumla mustakabali kitaifa iko pale pale.

Misingi ya umoja wa kitaifa ndio umeijenga nchi inayoitwa Tanzania.

Kinara wa utaifa wa nchi hii bado ni Mwalimu Nyerere. Hapo nyuma Lissu uko on record kumkashifu na kumtukana kisiasa Mwalimu.

Tatizo kubwa hukuwa na sera, taratibu na itikadi mbadala kupitia chama chako.

Kama kuna kitu kitakurudisha Ulaya ni kumkashifu Mwalimu kwa mara nyingine.
Ww huna akili, kumkosoa Nyerere si kunitukana, hata Nyerere alijikosoa mwenyewe, kasome kitabu Cha TUJISAHIHISHE Cha Mwalimu mwenyewe

Alafu mie pia binafsi, sikubalian na Sera ya ujamaa, yaan hamna kitu sipend Kama UJAMAA
 
Ulivyo na kutu kichwani hujui hata mada inasemaje.
Soma tena au kama hujui kusoma tafuta mtu akusomee na akueleze tofafauti kati ya kukashifu na kukosoa.
 
......Looh, Jidu La Mabambasi hapa una lipi la kusema ndugu yangu? Ulikuwa unawaza nini kuleta hoja ya ajabu kama hii hapa jukwaani?

.....Hii iko chini ya kiwango cha fikra na ufahamu wako. Hukustahili kuja na propaganda ya hovyo kiasi hiki!

....Tundu Lissu ni mtu mzuri sana, Hana unafiki na husema ukweli mtupu ambao ni mwiko kwa CCM na hiyo ndiyo kashfa kwa wana CCM wa sampuli yako Jidu La Mabambasi

....hivi nyie huko CCM ni watu wa namna gani msiotaka kukosolewa? Tangu lini kukosoana ikawa kashfa au matusi jamani?

Mimi nahisi kinachowakera kwa Tundu Lissu, ni lugha ambayo huitumia ktk kutoa hoja zake. Huwa halembi eti

.....Anapokosoa hutumia lugha kali, ya kukera na yenye mamlaka. Hili huwaudhi sana watawala.

....Kwangu mimi Hili ni jema sana pale mtu anaporekebisha mambo na makosa yaliyofanywa na manunda wa ujinga huko CCM
Unamzungumzia Tundu huyu aliyesema Serikali itafungwa jela sababu ya makinikia...Tundu huyu anayetetea ushoga..au Kuna mwingine
 
Back
Top Bottom